Wagombea wa Trump washinda uchaguzi Marekani

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,775
2,000
Chama cha Republican kimeshinda uchaguzi muhimu wa bunge la Congress katika jimbo la Georgia ulioonekana na wengi kuwa kura ya maoni dhidi ya utawala wa rais Donald Trump.

Huku kura zote ikiwa zimehesabiwa, mgombea wa Republican Karen Handel alishinda kwa asilimia 53 huku mgombea wa Democrat akijipatia asilimia 47.

Katika Jimbo la Carolina Kusini, mgombea wa Republican Ralph Norman alimshinda mgombea wa Democrat Archie Parnell katika ngome ya wahafidhina. Spika wa bunge Paul Ryan alimpongeza Bi Handel kwa ushindi huo mgumu. Chama cha Democrat kilishindwa kwa kura chache katika maeneo ya Kansas na Montana mwaka huu.

Katika jimbo la Georgia matumizi ya uchaguzi huo yalifikia dola milioni 56 ikiwa ndio uchaguzi uliogharamikiwa katika historia ya Marekani.

Bwana Ossoff alishindwa kupata asilimia 50 ya kura zilizohitajika ili kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jimbo la Atlanta mnamo mwezi Aprili, hivyobasi kulazimisha awamu ya pili ya uchaguzi dhidi ya Handel.

Democrats walitumai kutumia fursa ya kushuka kwa umaarufu wa Trump kushinda kiti cha Georgia.
bbc swahili
 

marcus rojo

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
1,499
2,000
Hata media wakifanya vipi atawashinda tu, pale ataondoka kwa impeachment la sivyo miaka saba na unusu inamuhusu WH
 

HELA

Senior Member
May 10, 2015
179
250
CCN wanatia huruma sana..
Kabla ya matokeo uchaguz wa Georgia walisema kuwa uta reflect uongoz wa Trump

Baada ya matokeo wanaaema huu haukuwa uchaguzi unaomuhusu Trump hata kidogo.
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,124
2,000
Media zinamtangaza Trump vibaya tu
Hilo ndilo tatizo, uzuri raia wa Marekani walio wengi wanajitambua si rahisi kuwarubuni kwa kupitia MSM zilizo sheheni habari ambazo ni fake - na bado!! Yaani jamaa huyu atashinda njama za maadui wake wote wanao julikana na wasio julikana kwa kuwa Trump ni chaguo la Mungu, Mungu wetu awezi kukabidhi nchi kwa binadamu wanao pigia debe ushoga na kupenda penda vita.
 

Raskazoni

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
244
250
CCN wanatia huruma sana..
Kabla ya matokeo uchaguz wa Georgia walisema kuwa uta reflect uongoz wa Trump

Baada ya matokeo wanaaema huu haukuwa uchaguzi unaomuhusu Trump hata kidogo.
"CCN" ndio shirika gani tena la utangazaji?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom