Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,409
- 20,766
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Njombe kimelalamikia faulo zinazochezwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani hapa baada ya wagombea wake 166 wa vijiji na vitongozi kuenguliwa kwa hujuma.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Njombe, Alatanga Nyagawa, akizungumza na NIPASHE jana alisema kutokana na wagombea wa chama hicho kuenguliwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupigwa.
Nyagawa alisema wagombe hao wameenguliwa kwa madai kuwa awali walikuwa CCM na hivyo wakati wanahamia Chadema hawakuaga na kwamba katika nafasi ya uenyekiti vijijini ni 66 na vitongoji ni 100.
CCM alisema kuwa chama hicho kimeadhilika katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kutokana na wagombea wa nyazifa za uenyeviti ngazi ya vijiji 66 kuenguliwa, nafasi ya vitongoji 100 kutokana na hujuma zinazodaiwa zimefanywa na Chama cha Mapinduzi CCM.
"Wagombea wa Chadema katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe wameenguliwa kwa hujuma zinazofanywa na CCM, tutadai haki yetu hadi ipatikane,"alisema.
Alisema licha ya suala hili kufikishwa kwa Kamati ya Rufaa ya Mkoa ambayo ipo chini ya Katibu Tawara wa mkoa (RAS), lakini sababu zilizotolewa hazina msingi na hivyo kukintyima haki Chadema.
Nyagawa alisema mapingamizi mengine yamewekwa kimakosa na viongozi wa CCM badala ya wagombea kufanya kinyume na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Chanzo: Nipashe