Wagombea wa CHADEMA 166 waenguliwa Njombe

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,754
Freman-Mbowe-December8-2014.jpg

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Njombe kimelalamikia faulo zinazochezwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani hapa baada ya wagombea wake 166 wa vijiji na vitongozi kuenguliwa kwa hujuma.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Njombe, Alatanga Nyagawa, akizungumza na NIPASHE jana alisema kutokana na wagombea wa chama hicho kuenguliwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupigwa.

Nyagawa alisema wagombe hao wameenguliwa kwa madai kuwa awali walikuwa CCM na hivyo wakati wanahamia Chadema hawakuaga na kwamba katika nafasi ya uenyekiti vijijini ni 66 na vitongoji ni 100.

CCM alisema kuwa chama hicho kimeadhilika katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kutokana na wagombea wa nyazifa za uenyeviti ngazi ya vijiji 66 kuenguliwa, nafasi ya vitongoji 100 kutokana na hujuma zinazodaiwa zimefanywa na Chama cha Mapinduzi CCM.

"Wagombea wa Chadema katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe wameenguliwa kwa hujuma zinazofanywa na CCM, tutadai haki yetu hadi ipatikane,"alisema.

Alisema licha ya suala hili kufikishwa kwa Kamati ya Rufaa ya Mkoa ambayo ipo chini ya Katibu Tawara wa mkoa (RAS), lakini sababu zilizotolewa hazina msingi na hivyo kukintyima haki Chadema.

Nyagawa alisema mapingamizi mengine yamewekwa kimakosa na viongozi wa CCM badala ya wagombea kufanya kinyume na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Chanzo: Nipashe
 
Kinachonisikitisha ni CCM kulazimisha kushinda katika chaguzi hizi ni vema wakatambua kuwa Ngazi ya Vitongoji, Mitaa na vijiji ndio sehemu ambayo uongozi wa Serikali unaanzia kwa hiyo kulazimisha kuwepo na kiongozi ambae hakubaliki na wananchi kutasababisha kudhorota moja kwa moja shughuli za maendeleo za kiserikali kwani wananchi hawatakuwa tayari kutoa ushirikiano wowote kwa kiongozi ambae amepitishwa kinyume na matakwa yao kwa hiyo kwa hujuma hizi tutarajie kudorora kwa shughuli zote za maendeleo ambazo wananchi walikuwa wameishaanza kujitolea kwa nguvu na mshikamano.
 
hapo unawafanya wananchi kuelewa zaidi wanaposikia flaani kachakachua ubunge chuki hii itajibiwa 2015.kuna mabo mengi ambayo ingalikuwa rahisi tu kurekebisha si kungangania sheria nyingi katika ngazi hizo hu wananchi hatukuwapa elimu ya kutosha
 
Hata mkiwapa elimu wananchi lakini ikifika 2015 wanachagua kijani
 
kuna mambo mengne chadema wanakosea taratibu za wazi kabisa lakini bado wanalalamika kuhujumiwa. Kuna haja ya kujipanga vizuri wakati mwingne
 
Tutaheshimiana tu. ukiona mtu analalamika hata kabla ya mchezo basi ujue hakujiandaa vema. Hapa ndipo ninapolikumbuka bandiko la Chabruma
 
Donatila

Siamini gazeti laandika lugha mbovu namna hii. Safari nyingine andika hivi:
Kimeadhilika = Kimeazirika
Nyazifa = Nyadhifa
Tawara za mikoa= tawala
 
Last edited by a moderator:
nilishawambia mara nyingi sana kwamba chama chetu cha MAGAMBA ni nouuma. tuna mbinu nyingi balaa na zote hizi tumefundishwa na wachina. sasa tunajua nyie UKAWA mnapendwa na watu ko ili tuweze kumaliza game ni lazima tuchezee nje ya uwanja kwa kupandikiza fitina mbalimbali ili mradi tusonge na tuendelee kufuja mali zenu nyie msio jielewa. we fikiria mbinu ya kuhonga fedha, kanga, kofia, Tshirt, sukari zooote wadanganyika wameishashtukia ko tumebadili mbinu na hii ya pingamizi ni mbinu ya 9 kati ya kumi na nane mpaka tuje tumalize zoote mtakuwa mumenyampa vya kutosha. sie ndo CCM bwana kama hutaki unalo jambo
 
Wangekuwa wana huruma na ww wangekufanya ht umalize darasa la saba, uandikaji wako unaonesha umeishia Std3 or 4. Nyie ni mtaji mzuri sana kwa CCM na ht cku1 hawataki muelimike
 
Siamini gazeti laandika lugha mbovu namna hii. Safari nyingine andika hivi:
Kimeadhilika = Kimeazirika
Nyazifa = Nyadhifa
Tawara za mikoa= tawala

We sema mmeshindwa achana na gazeti halihusu
 
Ninawashangaa sana wanasiasa,wako busy kulalamika kwenye mitandao,njia rais ,nenda mahakamani weka pingamizi uchaguzi usitishwe,kwisha.

Sababu mtapiga kelele wee kwani kelele za mlango haziasi usingizi
 
Hizi rafu zinazochezwa zisiturudishe ukawa nyuma maana ccm waandaa kitanzi cha kujinyongea wenyewe 2015. Wananchi ndio wanaelewa majizi ya ccm kwa undani zaidi!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom