Wagombea wa CCM waweza kushinda bila ya uharamia na mchezo mchafu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea wa CCM waweza kushinda bila ya uharamia na mchezo mchafu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jun 22, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wagombea wa CCM waweza kushinda bila ya uharamia na mchezo mchafu?

  Imekuwa ni kawaida kwa CCM kwamba kila unapokuja uchaguzi (hata ule wa wao wenyewe ndani (internal party elections) huwa ni ghilba, umafia, uharamia na vitendo vingine vichafu havipaswi hata kuelezea.

  Maovu haya yanafanyika katika ngazi zote – yaani kuanzia uteuzi wa wagombea wao hadi uchaguzi wenyewe wakishindana na vyama vingine. Jee hii ndiyo imekuwa hulka ya CCM chama ambacho kinaimba wimbo wa kuwa wastaarabu hasa kwa vyama vingine?

  Kuna kutishana, hata pengine kutishia mauaji (kama vile vitisho vinavyotolewa na wakala wao mkuu Sheikh Yahya Hussein dhidi ya watakaompinga JK).

  Hivi sasa tunashuhudia yote haya, huku hatusahau mwaka miaka 5 iliyopita wakati wa uteuzi wa JK. Uharamia uliofanyika wakati ule kumpitisha huyu ulikuwa wa kihistoria kwani ulikigawa chama katika makundi, makundi ambayo yapo hadi leo.

  Vyombo vya dola, hasa Intelligence vilitumika kutishia wagombea wengine wajitoe ili kumpitisha Jk ambaye bila ya kufanyika hivyo asingefua dafu – kwani wengi walikuwa sahihi katika kutabiri kwamba urais wa Jk ungekuwa kituko tu – na kweli umekuwa kituko!. Fedha chafu zilitumika – fedha ambazo kumbe ziliibwa kutoka BoT.

  Swali: Kabisa kabisa CCM haiwezi kiufanya siasa zake kwa njia za kistaarabu?
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Stupid question! You know they can't, most of them -- even dream of coming near to Parliament grounds!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawawezi hao!! Daima mzoe vya kunyonga vya kuchinja haviwezi!!!
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Jun 22, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi nilidhani unakuja na option? in short ni ndoto
   
 5. c

  cesc Senior Member

  #5
  Jun 22, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hakuna swali...uliza...hilo ni jibu ...hawawezi hata yesu akirudi....
   
 6. E

  Erica Furaha Member

  #6
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawawezi ,wameshazoea wakitaka madaraka mpaka wahonge na kutumia nguvu za giza
   
 7. J

  Jane Jastine New Member

  #7
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 22, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,860
  Trophy Points: 280
  Hakuna la ajabu,huo ndio utamaduni wao.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama jibu ni NO hawawezi kabisa ustaarabu kwa nini wanawaimbia hao wengine (vyama vya upinzani) kwamba ni vurugu tupu. Nakubali kuna vurugu pia katika upinzani -- lakini hawa CCM walitakiwa kuonyesha njia za kufanya demokrasia kwa njia za kistaarabu kwani wao ndiyo walifungua mlango wa plural democracy.

  Wasiwasi wangu ni kwamba mfano (Mungu apitishie mbali) tukiingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na matendo hayo, nani ataweza kuwa credible enough luituliza? Au ndiyo itakuwa kama DRC au Somalia? hakuna watu ndani ya uonmgozi wa CCM wenye cool minds na kukemea hivi vitendo, au wote ndo mafiosi tu? sikamsikia hata JK mwenyewe kukemea vitendo vichafu katika chama chake. Inatisha kwelikweli!!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye red: My brother wako tele ndani ya CCm wenye cool minds na uwezo wa kukemea, lakini hawa wanatishwa sana wanapojitokeza au kujulikana -- hadi wananywea! Watanzania wana hulka ya woga kudai haki zao, sijui kwa nini -- ukilinganisha wale wa zama za mababu zetu walipigana na wakoloni.

  Wakijitokeza tu wanapakaziwa kila aina ya tuhuma na kuitwa kila aina ya majina. Na utashangaa brains behind wanaofanya vitisho hivyo ni kikundi cha watu wachache tu -- hawazidi kumi. Hawa wamewashika at ransom Watz mamilioni -- ambao hawafurukuti! Wengi katika kikundi hiki siyo hata wazalendo -- asili yao.
   
 11. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  CCM fujo tu lask week wamepiga watu ovyo kule Moshi
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  No, hawazidi 5!
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anayepaswa kuweka sawa mambo si mwingine yeyote bali kiongozi wa ngazi ya juu iwe ni wa Chama ama Serikali. Mwenyekiti wa CCM akiwa ni legelege basi mafiosa ndani ya chama hicho wataweza hata kumkalia kichwani. Serikalini hivyo hivyo akiwa Rais hovyohovyo kila aliyechini yake atafanya atakalo na wale ambao wana nia njema ya kutaka kulisaidia taifa watashindwa kufanya kazi zao vizuri kutokana na maamuzi ya hovyohovyo ya kiongozi wao wa juu.

  Nashangaa kwa nini hatuna ujasiri wa kumnyooshea kidole Kikwete kwa matatizo yaliyoko ndani ya CCM na Serikali yake kwa ujumla. Wakati wote tunazunguka tuuu na kudai wawepo watu wa kukemea. Kiongozi wa juu hapaswi kukemewa yeye ndiye anapaswa kukemea walio chini yake pale wanapokwenda kinyume.

  Bado naamini kwa mbali kwamba Kikwete kama ana akili nzuri, katika muhula huu wa pili atakaopewa atajitahidi kwa ari zaidi, na nguvu zaidi na wala si kwa kasi kujirekebisha na kuchukua hatua zinazostahili ili kulirejeshea taifa letu heshima yake. Tanzania haina tena ile heshima kubwa iliyokuwanayo Afrika na duniani enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere. Tanzania imebaki kuongozwa kisanii na kitapelitapeli tu.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Boramaisha:
  Wwe unajua, nami ninajua, na karibu kila mtu mwenye akili timamu nakuweza kutambua mambo anajua kwa nini Jk hawezi kuwakemea wanaoidhalilisha CCM. Bila wao uprezida angeusikia kwa mbali tu, na kwa kuwa bado anayo tamaa ya kipindi cha pili (ingekuwa mimi ningesema basi, inatosha!) hawezi kamwe kuwanyooshea kidole -- hata wafanye nini.

  Na safari hii (katika kipindi chake cha pili) ndiyo hasa nchi itafilisika kwa kuchotwa kwa sababau ndo mwisho wa mtandao aliyobebeshwa begani -- kukaa madarakani.
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Zak:
  Naomba nisikubaliane na wewe kwa hilo la JK kubebeshwa mtandao begani. JK na rafikizake namely, Lowassa na Rostam ndio engineers na waasisi wa mtandao. Ni kweli mtandao ndio uliomfikisha madarakani, lakini kama angekuwa kiongozi makini na shupavu alikuwa na nafasi nzuri ya kuweza kuuvunja mtandao ule mara tu alipoingia madarakani. Udhaifu wake ndio uliomfanya ashindwe kuuvunja pale alipopaswa kufanya hivyo ndio maana ameendelea kuteseka kubeba 'msalaba' huo na asipoangalia msalaba huo utamuangamiza baada ya kipindi chake cha pili kwisha. Narudia, kama ana akili nzuri atumie nafasi atakayopewa kurekebisha mambo katika kipindi cha pili atakachopewa.

  Tunao mfano mzuri wa kiongozi ambaye amefanikiwa kujiengua kutoka kwenye mtandao. Mzee Samuel Sitta alipoona ameishapata alichokitaka - Uspika. Akaanza kazi yake kwa mbwembwe zote za kutaka bunge lake liwe Bunge la "Viwango" na kwa kiasi kikubwa ameweza kufanikiwa. Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania Bunge kuweza kumuengua Waziri Mkuu kutoka kwenye wadhifa wake, Bunge la viwango liliweza kufanya muujiza huo and thanks to Mr. Speaker. Mzee Sitta alikuwa "mwenzao" wakampitisha kwa mbwembwe kuwa Spika lakini alipofika pale akaiweka kazi yake "kwanza"; mtandao ule ukawa historia nzuri kwake iliyomfikisha mahali alipotaka. Kwa nini JK ashindwe? Isitoshe alianza vizuri kwa kututangazia kwamba urais wake hauna ubia, ilikuwaje akayala maneno yake mwenyewe - udhaifu!
   
 16. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hicho chama cha upinzani kinachoibiwa kura ni kipi? Maana CUF iko chakari Tanzania Bara, CHADEMA inasimamisha wagombea wazuri kwa viti visivyozidi 50... sasa hivyo vingine ni chama gani kinatakiwa kushinda...
   
 17. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Kuhusu;
  Wagombea wa CCM waweza kushinda bila ya uharamia na mchezo mchafu?

  Hawawezi kwa vile hiyo ndiyo dini yao mpya waliyoianzisha nayo imeenea pote kwa viongozi na waumini wao. For example, mtangaza nia can not not achieve his/her mission unless ametoa 'dash' kwa waumini yaani watangaziwa nia wake
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mbinu chafu sisi M ni utamaduni.

  Sikiliza kisa hiki cha kweli cha karibuni.

  Katika jimbo moja la uchaguzi kuna tawi moja wametangazia wanachama wao kuwa wala wasipate shida katika kuchagua mbunge kwa kuwa yule aliyepo tayari halmashauri ya wilaya imeshampitisha kama mgombea pekee na hakuna mwenye ruhusa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea. Wakati huo huo katokea mtu pembeni ambaye ameanza kutangaza nia ya kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo hilo. Naye pia ni mwanachama wa sisi M. ambaye amelalamika kuwa kwa nini chama kinatangaza mgombea pekee wakati kuna wanachama wanahitaji kugombea?

  Habari zilipopatikana kuwa huyu mgombea mtarajiwa anatangaza nia tayari wameshaanza kuunda zengwe kwamba si mwanachama wa chama cha sisi M. Na kama haitoshi wametoa maelekezo kwa viogozi wa tawi lake wasimuorodheshe kwenye daftari la tawi ili ionekane kwamba yeye si mwanachama na hivyo wamkoseshe haki ya kuchagua au kuchaguliwa katika kura za maoni.
  Hizi mbinu za ki sisiemu ziko hata ndani ya chama chenyewe.

  Mungu tuepushe na ghiriba za chama hiki.
   
Loading...