Wagombea urais wa vyama vya siasa vitakavyoshindwa kuingia bungeni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea urais wa vyama vya siasa vitakavyoshindwa kuingia bungeni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, Jul 24, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni vyema sasa sheria za uchaguzi zikarekebishwa ili angalau mshindi wa pili na watatu waliogombea uraisi kwa vyana vya siasa watakao shindwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu kuingia bungeni,hii itasaidia sana kwa wale wenye malalamiko au majeraha ya kisiasa kupata mahalipa kutolea madukuduku yao,na pia ili serikali ipate michago yao ambayo italisaidia taifa kupiga hatua.tumeshhudia wagombea wengi wenyeuwezo wakiachwa na michango yao ikipotea na pengine kuzaraulika kwa sababu tu hawana mahali sahihi pakusemea na michango ingelisaidia sana taifa kwani wangewawakilisha watanzania wengi waliowachagua kipindi cha uchaguzi mkuu na wananchi tungepata muda mzuri wa kuwatathimini na kùwapima.
   
 2. Electron

  Electron Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakawawakilishe nani huko bungeni?? Si utazuka utitiri wa vyama vyenye wagombea wasiojigusa hata kupinga kampeni wakijua wanakula bingo ya kuingia bungeni?? Hatuwataki hao watanunuliwa kirahisi....
   
 3. A

  Analytical Senior Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I see there is a point here. Tungeweza kuweka percentage limit, say asilimia 5% ya kura zote. Imagine watu 2, 000, 000 ya watanzania waliokuwa na imani na mtu fulani kwa sababu ya sera na mtazamo wake, wakakosa uwepo wa mtu huyu bungeni! Kwa hiyo leo tungekuwa tunafaidi uwepo say wa akina Dr Slaa, Lipumba na wengine Bungeni kuliko kuwa utitiri wa hopeless people in the name of 'Viti maalumu', ambao kazi wengine ni mipasho na kusema ndioooooooooooo.
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Ni hoja nzuri lakini kwanza tulisafishe bunge letu la sasa lenye wawakilishi miambili na kitu lakini mwisho wa siku tuna wala kodi 300 na!

  Tukiondoa viti maalumu na zile nafasi kumi za raisi kuteua wabunge bila shaka tutakuwa na bunge dogo lenye kujaziwa na watu watatu walioshindwa uraisi!

  Hapo naamini taifa litapata krimu ya kweli kuliko wagonjwa wanaolala na wanaobwabwaja kila mara bungeni huku wakitafuna vinono vya nchi hii kwa jasho la sisi makabwela wavuja jasho!
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kinachokosekana ni ile kitu inaitwa "fair play" kama kwenye mpira, mwenzako akiumia unatoa mpira nje. Kuna busara kubwa kwenye utamaduni huu wa soccer. Rais aliyeapishwa alipaswa kufanya "fair play" ya kumteua mwenzake kuwa mbunge. Kwa mfano, badala ya Kikwete kumteua Mbatia aliyekataliwa hata na watu wa kawe mpaka akawa wa tatu kwenye uchaguzi, angemteua Dr. Slaa aliyekubaliwa na watanzania zaidi ya milioni moja. Ila ili hilo liwezekane ni wajibu wa yule aliyeshindwa kukubali kushindwa.
   
 6. b

  bodachogo Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mchango kwa maendeleo ya taifa sio lazima mtu awe mbunge ni sawa sawa na kumchagua mbunge anayetumia fedha zake mwenyewe kuleta maendeleo,ukichunguza kwa umakini utakuta ni mfanyabiashara anayeliibia taifa 100 na kurudisha 10,jiulize mtu kama huyo alishindwa kutoa misaada yake ya maendeleo mpaka awe mbunge ? kulikomboa taifa sio lazima uingie kwenye siasa,kuingia kwenye siasa sio lazima uwe diwani,mbunge au rais,unaweza kuongoza kwa ku-monitor wawakilishi wa chama chenu kusimamia mnachokiamini kama chama ...Bunge hivi sasa limegeuka taasisi ya kutafuna fedha tu. Kama mtu anataka kuchangia anaweza kutumia wabunge wa chama chake ambao ndio wasimamizi wa sera anazoziamini. Kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali siungi mkono hoja.
   
 7. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ungefikiria kidogo badala ya kukurupuka usinge jibu ulivyo jibu
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wazo lako. Labda tuwe na mfumo kama wa Kenya unaoruhusu kugombea urais na ubunge. Akishindwa urais akashinda ubunge, aingie bungeni. Lakini akipigwa chini vyote abakie nje akajipange vyema.
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  wazo lako ni zuri sana ila kwa siasa hizi za majitaka hapa bongo sahau kabisa...kama suala la mgombea binafsi linapingwa ili kuilinda serikali ya magamba unafikiri hili litawezekana??
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mimi ninafikiri tungeiga utaratibu wa Kenya.

  Kwanza Kenya ili uwe RAIS kwanza lazima ushinde UBUNGE katika jimbo ulilogombea. Hivyo wagombea URAIS wote nchini Kenya Pia wanakuwa wagombea UBUNGE katika majimbo yao.

  Kama mgombea URAIS anakubalika katika jimbo, atachaguliwa kuwa MBUNGE. Ikitokea akashindwa URAIS basi atabakia na UBUNGE wake. Mfano Raila Odinga wakati anagombea URAIS wa Kenya, Pia aligombea UBUNGE wa Lang'ata. "Alishindwa" URAIS lakini akapata UBUNGE.

  Badala ya kupendekeza kwamba mtu akigombea URAIS akishindwa basi awe mbunge hiyo HAIFAI. Tulikuwa na wagombea URAIS kama (NO DISRESPECT) Fahmu Dovutwa, Shao, Anna Senkoro, Hashim Rungwe. Just imagine watu kama hawa wangeingia BUNGENI SIMPLY waligombea tu URAIS si ni janga jingine la VITU MAALUMU.

  WAGOMBEA URAIS wote wagombee pia UBUNGE iwe ni pre-requisite. Akikosa URAIS lakini kwao anakubalika atapata ubunge.

  Ninasikia kuna VETERANS wagombea URAIS lakini hawajawahi hata kupata UBUNGE. Tuwapime kama kwao wanakubalika.

  Kenya wallahi wako mbele sisi Watanzania hata nyayo zao tu hatuzifuati!
   
 11. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kasema watakao shaika nafasi ya pili na tatu, trend ya chaguzi zilizo pita zianonyesha wagombea wanoshaika nafasi hizi mbili wana vuka 5% ya kura. Mimi naunga mkono hoja
   
 12. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
   
 13. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
   
 14. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ndiooooooooooooo. Wananiboa wakisema ivo?>
   
 15. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Naunga na wewe, ila kuwe na kiwango cha kula anachotakiwa kupata, tuseme atakayepa kuanzia 5% ya kura zote aweze kuingia bungeni

   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,802
  Likes Received: 5,096
  Trophy Points: 280
  T.2015.CDM,

  ..mimi naona waachwe tu waendelee na shughuli zao kama sisi wapiga kura wao tunavyofanya.

  ..wanapoingia kwenye kinyanganyiro cha uraisi waelewe kwamba mshindi atakuwa ni mmoja tu.

  ..sasa hapa unajenga hoja kwa ajili ya waliokosa Uraisi, how about waliokosa ubunge,waliokosa udiwani etc etc?

  ..je, inamaana walioshindwa nafasi nyingine kama ubunge,udiwani,..nao tuwatafutie nafasi za "kifuta machozi??"
   
 17. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mimi nina mashaka ccm inaweza ikaweka mamluki ambao at the of the day watarudi kupunguza kasi ya hoja za mrengo wa kushoto. Nakubaliana na idadi ya watu waliompigia kura let say kuanzia 500,000 nakuendelea
   
Loading...