• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Elections 2010 Wagombea Urais Upinzani kugombea Ubunge, nini tafsiri yake?

Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,282
Points
1,225
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,282 1,225
Naona MAPAMBAZUKO katika siasa za upinzani!.............wagombea wqengi wa URAISI kupitia vyama pinzani tanzania wameamua kugombea ubunge>

MREMA,ameelezea KUITIKA WITO uliomtaka agombee kwenye jimbo lake la zamani,vunjo kilimanjaro.

MBOWE,amekuwa akitajwa mara kadhaa kugombea ubunge jimbo la hai

MBATIA,anataka kwenda kugombea KAWE,

PROF LIPUMBA,anasema nafasi ipo wazi KWA YOYOTE MWENYE SIFA!

MTIZAMO WANGU!
naona kama wapinzani wanataka KUMSURPRISE J.K kwa kumpa LADHA TOFAUTI KATIKA UPINZANI!kwa sisi wana kandanda tunasema WANATAKA KUBADILISHA FORMATION!

Wanajamii naamini mnaona mbali sana!........naomba maoni yenu MNAONA PICHA GANI YA MWAKA 2010?
 
Recta

Recta

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2006
Messages
854
Points
195
Recta

Recta

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2006
854 195
Pamoja na kwamba walitakiwa wawe na mwamko huo mapema zaidi (chaguzi tatu zilizotangulia), ila uamuzi wao bado ni sahihi kabisa.

Nadhani ni vyema wapinzani wakaweka nguvu nyingi sana katika Ubunge kuliko katika u-Rais. Pamoja na kuweka nguvu hizo kwenye Ubunge, wasisahau pia kushirikiana katika kiti cha u-Rais ili waweze kutoa changamoto kwenye uchaguzi mkuu.

Mhimili wa Bunge ni muhimili muhimu. Ila kama inavyojulikana (kikatiba), Bunge halina nguvu sana kama ilivyo kwa Serikali kuu. Hivyo nashauri Mbowe, Mrema, Mbatia na Lipumba na Cheyo kugombea Ubunge popote wanapodhani watakubalika, na pia watafute mtu mmoja wa upinzani mwenye haiba na uwezo wa kushindana na CCM katika kugombea u-Rais. Wakifanya hivyo, si tu kwamba watakuwa wameonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao kwa kushiriki katika yale wanayoamini yanatakiwa kufanyika katika nchi yao, bali pia wataongeza uwezekano wa wananchi kuchagua bila kuchanganyikiwa, na kutumia uchaguzi vizuri zaidi. Nasema hivyo kwasababu, si rahisi kwa wenyeviti hao kushinda CCM endapo wote au baadhi yao wataamua kugombea urais.
 
J

Jujuman

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
248
Points
0
J

Jujuman

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
248 0

Mkuu Recta Salam,
Nakubliana nawe sana hata Sefu S hamadi angegombea ubunge sidhani kama katiba inazuia hilo. Ili wakosapo Uraisi watakua na jukwaa jingine kwa kupitia bunge kuendeleza sera za upinzani bungeni badala ya kutegemea mikutano ya wao na wananchi mitaani. Nadhani Waingereza wanatumia mfumo huo viongozi wa upinzani ni wabunge na hua ndio wa kwanza kuibana serekali kwa hoja Bungeni kabla ya wabunge wengine kuchangia.
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,419
Points
1,500
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,419 1,500
Pamoja na kwamba walitakiwa wawe na mwamko huo mapema zaidi (chaguzi tatu zilizotangulia), ila uamuzi wao bado ni sahihi kabisa.

Nadhani ni vyema wapinzani wakaweka nguvu nyingi sana katika Ubunge kuliko katika u-Rais. Pamoja na kuweka nguvu hizo kwenye Ubunge, wasisahau pia kushirikiana katika kiti cha u-Rais ili waweze kutoa changamoto kwenye uchaguzi mkuu.

Mhimili wa Bunge ni muhimili muhimu. Ila kama inavyojulikana (kikatiba), Bunge halina nguvu sana kama ilivyo kwa Serikali kuu. Hivyo nashauri Mbowe, Mrema, Mbatia na Lipumba na Cheyo kugombea Ubunge popote wanapodhani watakubalika, na pia watafute mtu mmoja wa upinzani mwenye haiba na uwezo wa kushindana na CCM katika kugombea u-Rais. Wakifanya hivyo, si tu kwamba watakuwa wameonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao kwa kushiriki katika yale wanayoamini yanatakiwa kufanyika katika nchi yao, bali pia wataongeza uwezekano wa wananchi kuchagua bila kuchanganyikiwa, na kutumia uchaguzi vizuri zaidi. Nasema hivyo kwasababu, si rahisi kwa wenyeviti hao kushinda CCM endapo wote au baadhi yao wataamua kugombea urais.
Nakubaliana sana na maoni yako, ila nadhani sisi ndio tuliwakuwa na maoni tofauti juu ya weneviti wa vyama. Sidhani kama katina zao zinasema kuwa wenyeviti ndio lazima wawe wagombea urais wa vyama vyao. Ingekuwa hivo basi kusingekuwa ni mikutano ya kuchagua wagombea urais katika vyama mbalimbali.

Suala la pili, bado naamini kuwa vyama vinanafasi ya kujijenga na kujitangaza ili sera zake zifahamike kwa wananchi. Sio sahihi kupitishia sera ya mfano UDP kwa CUF halafu ukadhani kuwa umeijenga UDP, unless UDP na CUF wameungana na kuwa chama kimoja. Mimi naunga mkono hasa kuunganisha vyama na kuwa na chama chenye nguvu na sio kusimamisha mgombea mmoja aungwe mkono na vyama vingine! Hii itauwa demokrasia kwa sababu tayari CUF au TLP wameshawekeza zaidi kuliko NLD, na sio sahihi tu kusema kuwa 1995 mgombea wa NLD alipata kura nyingi kwenye jimbo hili kwa maana hiyo ndiye anayekubalika. Hivyo bado naona ili vyama vijijenge ni lazima viendelee kusimama kama vyama au viungane.
 
H

Heri

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2007
Messages
244
Points
195
H

Heri

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2007
244 195
Vyama vya Upinzani hauna support kubwa kwenye grassroot level haswa kwenye rural areas. Kuhishinda CCM inakuwa vigumu. Wakiweza kwa kuanzaia kushinda viti vyingi vya Ubunge na wataweza kukikabiliana na Chama cha CCM vizuri bungeni na hapo hapo kujijenga na kuenroll wagombea wazuri (hata kutoka CCM) na wanachama wengi.
On a less serious note, inalipa kugombea ubunge ukizingatia malipo ya wabunge i.e mishahara, posho etc na ukianagalia umri wa hao wagombea urais.
 
J

Jafar

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2006
Messages
1,137
Points
0
J

Jafar

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2006
1,137 0
Kama wanaamka sasa ni vizuri. Mwl Nyerere (RIP) aliwaambia mwaka 1994 (alipokuwa anaongea na viongozi wa NCCR-Mageuzi, wakati huo Mrema na akina Mabere) kwamba nendeni mkagombee ubunge ili kuwe na upinzani bungeni kwanza kabla ya kufikiria uraisi, maana kwenye uraisi mtaingia kugombea kama under-dogs. Wakatoka hapo wakawaeleza watu wa magazeti kuwa Nyerere ametuita mbwa. Leo 15 years later wanarudi kinyumenyume. Mimi nawaunga mkono japo wamechelewa. Wazungu wanasema "the best time to plant a tree was 20 years ago, but the second best time is now". Kila la heri.
 
zacha

zacha

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2009
Messages
972
Points
1,000
zacha

zacha

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2009
972 1,000
mnh! Hii imesimama meku! kwa navyojua mimi hapa tz hatuna upinzani zaidi ya kuwa na wawakilishi tu ambao wanakula kodi zetu kila kukicha. Hivyo hivi vyama mi naviona kama NGo's ambazo watu wanatumia kujipatia pesa nyingi tu kuendesha maisha yao na kutufanyia fujo sisi tabaka la chini.... Siji piga kura mimi ng'o!
 
Forum statistics

Threads 1,405,417
Members 531,983
Posts 34,485,509
Top