Wagombea urais CCM wafunguka kauli ya Rais Kikwete

G 4real

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
454
212
Dar es Salaam. Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa nafasi hiyo ni kadhia na kazi ngumu, baadhi ya wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo wamesema wanafahamu changamoto hizo na kwamba kauli hiyo inazidi kuwapa nguvu na hamasa ya kuendelea na mchakato huo.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete akiwa Marekani, wakati akihutubia kwenye taasisi ya Wood Wilson International Center for Scholars alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10 unaomalizika Oktoba, mwaka huu na kusema:

"Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa sana pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia."

Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja wakati makada wa CCM wakipigana vikumbo kuwania urais.

Miongoni mwa wanasiasa waliotangaza na waliotajwa katika kinyang'anyiro hicho cha kurithi kiti kitakachoachwa wazi na Rais Kikwete ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Pia wamo, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Msimamo wa January

Akizungumza jana kuhusiana na kauli hiyo ya January alisema kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais.

"Nilitangaza nia hiyo huku nikiwa nafahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo... kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyonisukuma kuchukua uamuzi huo," alisema.

Alisema moja ya changamoto ambazo ameshakumbana nazo alisema: "Kwanza mimi nina bahati sana. Wakati nikiwa msaidizi wa Rais kipindi anagombea nafasi hiyo, nilipata fursa ya kutembea naye nchi nzima na kuona mambo mengi."

Mbunge huyo wa Bumbuli, alisema haikuwa kazi rahisi kufanya kampeni za kuhamasisha Watanzania wampigie kura Rais Kikwete... "wakati ule tulikuwa tunatembea katika maeneo mbalimbali nchini. Ukiwa umesimama jukwaani unaona sura za watu zilivyojawa na shauku… pale nilijifunza na kuona ukubwa wa changamoto za uongozi.

Nimebahatika pia kuona changamoto mbalimbali ambazo uongozi wa sasa umekumbana nazo kwa kipindi nilichowatumikia hadi sasa. Hiyo ni nafasi nzuri ya mimi kujifunza na kufahamu ni namna gani ninaweza kukabiliana nazo.

"Kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi na kiongozi huyo naamini kwamba zipo nyakati ambazo Watanzania tungepitia shida nyingi, lakini kutokana na busara na hekima yake nchi imeendeshwa vyema," alisema na kuongeza: "Ndiyo maana nasisitiza kuwa nchi yetu inahitaji kiongozi mwenye hekima na busara."

Naibu Waziri huyo ambaye alitangaza nia ya kuwania urais Julai mwaka jana, huku akisema kuwa huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola alisema nafasi hiyo ina sura mbili kwamba urasi ni kama taasisi na upande mwingine ni mtu mwenyewe.

"Nawaonea huruma wale wanaodhani kuwania nafasi hiyo ni sherehe. Nafasi hii inahitaji mtu mwenye afya nzuri, hekima na busara ya hali ya juu kwani atakuwa anafanya uamuzi kwa nchi. Watu wanadhani urais ni ushabiki… hakuna kitu kama hicho."

Mtazamo wa Sumaye

Sumaye ambaye aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema wakati ukifika atatangaza rasmi nia yake, alisema: "Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu anachokitaka. Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi."

Dk Kigwangalla

Akizungumzia kauli hiyo, Dk Kigwangalla alisema: "Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia anataka kutoa utumishi wake kwa nchi yake kama mimi."

Chanzo: Mwananchi
 
Hao walionukuliwa kwenye habari yako siujui kama wao wenyewe ndani ya dhamira zao wanaamini kuwa wanasifa za kugombea uraisi
 
Dar es Salaam. Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa nafasi hiyo ni kadhia na kazi ngumu, baadhi ya wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo wamesema wanafahamu changamoto hizo na kwamba kauli hiyo inazidi kuwapa nguvu na
“Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa sana pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”

hamasa ya kuendelea na mchakato huo.



Msimamo wa January

Akizungumza jana kuhusiana na kauli hiyo ya January alisema kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais.

“Nilitangaza nia hiyo huku nikiwa nafahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo... kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyonisukuma kuchukua uamuzi huo,” alisema.

Alisema moja ya changamoto ambazo ameshakumbana nazo alisema: “Kwanza mimi nina bahati sana. Wakati nikiwa msaidizi wa Rais kipindi anagombea nafasi hiyo, nilipata fursa ya kutembea naye nchi nzima na kuona mambo mengi.”

Mbunge huyo wa Bumbuli, alisema haikuwa kazi rahisi kufanya kampeni za kuhamasisha Watanzania wampigie kura Rais Kikwete... “wakati ule tulikuwa tunatembea katika maeneo mbalimbali nchini. Ukiwa umesimama jukwaani unaona sura za watu zilivyojawa na shauku… pale nilijifunza na kuona ukubwa wa changamoto za uongozi.

Nimebahatika pia kuona changamoto mbalimbali ambazo uongozi wa sasa umekumbana nazo kwa kipindi nilichowatumikia hadi sasa. Hiyo ni nafasi nzuri ya mimi kujifunza na kufahamu ni namna gani ninaweza kukabiliana nazo.



“Kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi na kiongozi huyo naamini kwamba zipo nyakati ambazo Watanzania tungepitia shida nyingi, lakini kutokana na busara na hekima yake nchi imeendeshwa vyema,” alisema na kuongeza: “Ndiyo maana nasisitiza kuwa nchi yetu inahitaji kiongozi mwenye hekima na busara.”

Naibu Waziri huyo ambaye alitangaza nia ya kuwania urais Julai mwaka jana, huku akisema kuwa huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola alisema nafasi hiyo ina sura mbili kwamba urasi ni kama taasisi na upande mwingine ni mtu mwenyewe.

“Nawaonea huruma wale wanaodhani kuwania nafasi hiyo ni sherehe. Nafasi hii inahitaji mtu mwenye afya nzuri, hekima na busara ya hali ya juu kwani atakuwa anafanya uamuzi kwa nchi. Watu wanadhani urais ni ushabiki… hakuna kitu kama hicho.”

Mtazamo wa Sumaye

Sumaye ambaye aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema wakati ukifika atatangaza rasmi nia yake, alisema: “Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu anachokitaka. Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.”

Dk Kigwangalla

Akizungumzia kauli hiyo, Dk Kigwangalla alisema: “Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia anataka kutoa utumishi wake kwa nchi yake kama mimi.”

images
images
images
images
 
Urais Tanzania ni mrahisi sana kama mtoto kuhesabu moja mbili tatu; NGOJA TUONE RAIS AIKINGIA MADARAKANI wote hawa watanyweaaaaa maji kopo la choooni
 
Who is January? Soon she will be February. Huyu jamaa makamba yani hata kusaidia Watanzania ktk mitandao yeye anazidi kuwagandamiza.mlugo Dvs 5


Swissme
 
Ccm ni sawa na mfumo wa umeme wenye kasoro ktk nyumba.hata ukiweka taa mpya lazima iungue.ccm haina jipya.
 
Magazeti yetu yana shida, kumbe Wassira bado ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais?
 
Who is January? Soon she will be February. Huyu jamaa makamba yani hata kusaidia Watanzania ktk mitandao yeye anazidi kuwagandamiza.mlugo Dvs 5


Swissme

Hahahaaa,ule muswada ukipitishwa utawamaliza wengi sana.
 
majuzi mh.rais kikwete alikua marekani katika kituo cha kimataifa cha woodwilson akifanya mahojiano. mh.rais jk alisema kuwa hakuna kazi yenye kadhia na ngumu kama kuwa rais,na yeye anashukuru kufikia salama kwenye muhula wake wa mwisho hapo october, lakini kauli hii ya rais kikwete imepokelewa kwa mitazamo tofauti na makada wanaowania nafasi ya kupata tiketi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM,makada hawa wamesema kauli ya mh.rais kuwa nafasi hiyo ni ngumu haiwakatishi tamaa na badala yake ndio inawaongezea nguvu ya kupambana hili kupata nafasi hiyo adimu. kuna makada wengi waliotangaza nia ya kuwania urais ndani ya chama na baadhi yao ni. waheshimiwa JANUARY MAKAMBA,DR.KIGWANGALA,NGELEJA,EDWARD LOWASA.
 
Nilidhani kuna hoja ya maana, kumbe ni mambo ya ccm!. Hayo wanayajua wao wala hatuna haja nayo na hayatuhusu. Sisi tunaendelea mbele kujenga nchi na UKAWA!.

UKaWA ndio mna kazi kubwa ya kulikwamua taifa kutoka mahala ccm imelikwamisha. Mnahitaji kuwa na timu imara yenye watu sahihi ili mtakapoanza kazi October, pasiwe na sehemu inaregalega.

Vingievyo, Watanzania wote wako pamoja sana na UKAWA.
 
Yawezekan urais ukiwa na nia kuisadia nchi ukiwa ssiem, ccm haifai inamajimajinamizi hayataki ufanye mema ya nchi.
 
majuzi mh.rais kikwete alikua marekani katika kituo cha kimataifa cha woodwilson akifanya mahojiano. mh.rais jk alisema kuwa hakuna kazi yenye kadhia na ngumu kama kuwa rais,na yeye anashukuru kufikia salama kwenye muhula wake wa mwisho hapo october, lakini kauli hii ya rais kikwete imepokelewa kwa mitazamo tofauti na makada wanaowania nafasi ya kupata tiketi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM,makada hawa wamesema kauli ya mh.rais kuwa nafasi hiyo ni ngumu haiwakatishi tamaa na badala yake ndio inawaongezea nguvu ya kupambana hili kupata nafasi hiyo adimu. kuna makada wengi waliotangaza nia ya kuwania urais ndani ya chama na baadhi yao ni. waheshimiwa JANUARY MAKAMBA,DR.KIGWANGALA,NGELEJA,EDWARD LOWASA.

We jamaa si unashindaga celebrity forum kujadili mambo ya diamond na wema sepetu?
 
Hivi kweli kabisa tunataka kujadiliana juu ya mgombea wa CCM? Mbuzi wanaweza kujadiliana ni mgombea gani toka familia ya chui atakuwa na maslahi kwao?
 
Back
Top Bottom