Uchaguzi 2020 Wagombea Urais 2020 Kupitia Upinzani: Tundu Antipas Lissu, Lazaro Nyalandu Na Zitto Kabwe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,877
2,000
Baada ya Edward Lowassa kurudi CCM, na kwa jinsi siasa zilivyo kwa sasa, wanasiasa wanaoonekana kutaka kuviwakilisha vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2020 katika nafasi ya Urais ni
1.Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu
2.Aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na
3.Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuber Kabwe.
Tudu Lissu na Zitto Kabawe tayari kwa nyakati tofauti wameshatangaza kupeperusha bendera za vyama vyao endapo vitawaamini. Lazaro Nyalandu baada ya Lowassa kuhamia CCM , amenukuliwa akisema hana mpango wa kurudi CCM na yuko tayari kuongoza kile alichokiita mapambano ya kuleta mabadiliko.

Tundu Lissu amepata 'coverage' nje ya nchi jambo ambalo kimsingi Mataifa ya nje yanamhitaji sana mtu aina ya Lissu kutoka Mataifa Machanga kwa ajili ya Maslahi yao binafsi. Lissu ameonekana kuwa pamoja na Mataifa ya nje katika mambo ambayo yanagusa maslahi yao kama vile kuwashambulia viongozi wa juu wa nchi yake, viongozi ambao ni alama ya Utaifa kama ambavyo Taifa lolote lile duniani huwatambua Viongozi wao kama alama ya Taifa husika, kutetea Mikataba ya Kinyonyaji ya Madini (ACACIA), Mapenzi ya jinsia moja na mengineyo mengi. Katika harakati zake za kutaka kujiuza ughaibuni , Lissu ameonekana akiomba msaada wa kifedha za kumuwezesha kuishi huko. Kimsingi Lissu ameshakuwa 'Çompromised' na Mataifa haya, anaweza kufanya chochote kibaya kwa nchi ilimradi tu kulipa fadhila na kuwafurahisha Wanaompa pesa. Hafai kuwa Rais wa nchi hii.

Lazro Nyalandu, yeye sina haja ya kumuelezea Zaidi. Kushindwa kwake kuiongoza Wizara nyeti kabisa kwa Uchumi wa nchi hii, Wizara ya Maliasili na Utalii ni dosari kubwa sana. Akiwa katika Wizara hii Wageni ndiyo walikuwa kama wamiliki wa Rasilimali hii adimu ya Tanzania . Nyalandu akiwa Waziri alitumia muda mwingi kujirusha nje na Walimbwende atawezaje kuyajua matatizo ya Wanzania? atawezaje kuwa na uchungu na Rasilimali za nchi hii? Kibaya zaidi kwa Nyalandu ni Uraia wake pacha, mtu wa aina hii hawezi kuwa mzalendo hata kidogo na matendo yake yanaonesha hivyo, akimaua kuiuza Tanzania, ni kiasi cha kuukana Uraia wa Tanzania na hapo atakuwa amemaliza kazi.

Zitto anaonekana kuwa nafuu kati ya hawa watatu, mwanzoni alionekana kuwa mwanasiasa wa ndani zaidi akiamini katika mapambano ya ndani kwa ndani Hata hivyo siku za hivi karibuni naye ametaka kumuiga Tundu Lissu na kudhania kuwa matatizo ya Watanzania yataisha kwa kushitakia kila kitu kwa Mataifa ya nje. Hata hivyo Zitto anaonekana kuwa na chembechembe za Uzalendo ingawaje pia ni mtu wa fursa kwa maslahi binafsi. Pale anapoonekana kufaidika na jambo Fulani huweka pembeni hisia zake za uzalendo hata kama halina mslahi kwa Taifa na kuziibua pale anapoonekana hana maslahi binafsi hata kama jambo analolipinga lina maslahi kwa Taifa. Tabia yake ya kuamini kuwa yeye ndiye anaweza kuwa juu nayo ni kikwazo.

Kwa Ujumla Upinzani una Mtihani mkubwa wa kumpata mgombea atakayeweza angalau kufikia Nusu ya Lowassa katika kupambana na Mgombea wa CCM ambaye ni Rais wa sasa , Dkt. John Pombe Magufuli mtetezi wa Wanyonge.
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,086
2,000
Write your reply...kila mtu anavaa,kinachotakiwa ni kushinda tu
 
CHADEMAASILI

Senior Member
Jan 19, 2018
123
225
Baada ya kuona video Lissu akiombaomba, nilimtoa kabisa kwenye kichwa changu. ni aina ya akina Mobutu Tsetseko, Zabanga
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,413
2,000
Lissu na Nyalandu ni hovyo kabisa, Zitto kidooogo anafaa
Mtu pekee Upinzani anayekubalika pande zote za muungano mwenye pesa za uchaguzii na anayekubalika na watu wa chini na wafanyabiashara kwa sasa ni mmoja tu Seif Sharif Hamad.The rest are crap including Zitto Kabwe
 
CHADEMAASILI

Senior Member
Jan 19, 2018
123
225
Mtu pekee Upinzani anayekubalika pande zote za muungano mwenye pesa za uchaguzii na anayekubalika na watu wa chini na wafanyabiashara kwa sasa ni mmoja tu Seif Sharif Hamad.The rest are crap including Zitto Kabwe
Bila shaka maana hawa akina Lissu sasa wamekuwa kama Tanzania ndiyo ugenini na Ulaya ndiyo nyumbani kwao, nadhani hata Wazungu wanatushangaa sana.
 
lubamba

JF-Expert Member
Jan 13, 2015
936
1,000
Baada ya Edward Lowassa kurudi CCM, na kwa jinsi siasa zilivyo kwa sasa, wanasiasa wanaoonekana kutaka kuviwakilisha vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2020 katika nafasi ya Urais ni
1.Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu
2.Aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na
3.Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuber Kabwe.
Tudu Lissu na Zitto Kabawe tayari kwa nyakati tofauti wameshatangaza kupeperusha bendera za vyama vyao endapo vitawaamini. Lazaro Nyalandu baada ya Lowassa kuhamia CCM , amenukuliwa akisema hana mpango wa kurudi CCM na yuko tayari kuongoza kile alichokiita mapambano ya kuleta mabadiliko.

Tundu Lissu amepata 'coverage' nje ya nchi jambo ambalo kimsingi Mataifa ya nje yanamhitaji sana mtu aina ya Lissu kutoka Mataifa Machanga kwa ajili ya Maslahi yao binafsi. Lissu ameonekana kuwa pamoja na Mataifa ya nje katika mambo ambayo yanagusa maslahi yao kama vile kuwashambulia viongozi wa juu wa nchi yake, viongozi ambao ni alama ya Utaifa kama ambavyo Taifa lolote lile duniani huwatambua Viongozi wao kama alama ya Taifa husika, kutetea Mikataba ya Kinyonyaji ya Madini (ACACIA), Mapenzi ya jinsia moja na mengineyo mengi. Katika harakati zake za kutaka kujiuza ughaibuni , Lissu ameonekana akiomba msaada wa kifedha za kumuwezesha kuishi huko. Kimsingi Lissu ameshakuwa 'Çompromised' na Mataifa haya, anaweza kufanya chochote kibaya kwa nchi ilimradi tu kulipa fadhila na kuwafurahisha Wanaompa pesa. Hafai kuwa Rais wa nchi hii.

Lazro Nyalandu, yeye sina haja ya kumuelezea Zaidi. Kushindwa kwake kuiongoza Wizara nyeti kabisa kwa Uchumi wa nchi hii, Wizara ya Maliasili na Utalii ni dosari kubwa sana. Akiwa katika Wizara hii Wageni ndiyo walikuwa kama wamiliki wa Rasilimali hii adimu ya Tanzania . Nyalandu akiwa Waziri alitumia muda mwingi kujirusha nje na Walimbwende atawezaje kuyajua matatizo ya Wanzania? atawezaje kuwa na uchungu na Rasilimali za nchi hii? Kibaya zaidi kwa Nyalandu ni Uraia wake pacha, mtu wa aina hii hawezi kuwa mzalendo hata kidogo na matendo yake yanaonesha hivyo, akimaua kuiuza Tanzania, ni kiasi cha kuukana Uraia wa Tanzania na hapo atakuwa amemaliza kazi.

Zitto anaonekana kuwa nafuu kati ya hawa watatu, mwanzoni alionekana kuwa mwanasiasa wa ndani zaidi akiamini katika mapambano ya ndani kwa ndani Hata hivyo siku za hivi karibuni naye ametaka kumuiga Tundu Lissu na kudhania kuwa matatizo ya Watanzania yataisha kwa kushitakia kila kitu kwa Mataifa ya nje. Hata hivyo Zitto anaonekana kuwa na chembechembe za Uzalendo ingawaje pia ni mtu wa fursa kwa maslahi binafsi. Pale anapoonekana kufaidika na jambo Fulani huweka pembeni hisia zake za uzalendo hata kama halina mslahi kwa Taifa na kuziibua pale anapoonekana hana maslahi binafsi hata kama jambo analolipinga lina maslahi kwa Taifa. Tabia yake ya kuamini kuwa yeye ndiye anaweza kuwa juu nayo ni kikwazo.

Kwa Ujumla Upinzani una Mtihani mkubwa wa kumpata mgombea atakayeweza angalau kufikia Nusu ya Lowassa katika kupambana na Mgombea wa CCM ambaye ni Rais wa sasa , Dkt. John Pombe Magufuli mtetezi wa Wanyonge.
Umemaliza?
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,814

Wana CCM swala la upinzani na UKAWA linawahusu nini ?!. Si mfurahi kwa sababu mnaletewa wagombea wasio washindani. Mbona mnawaka hovyo ?!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwenye machoyote

New Member
Mar 2, 2019
3
20
Ni kweli kabisa unao uwezo wa kujenga hoja vizuri lakini huzuni yangu juu yako ni kwamba umeshindwa kabisa kubalance makala yako na imeonesha moja kwa moja wewe Ni mdau au shabiki au kada wa chama furani.

Anyway ninakushauri ujipe muda wa kuchambua upya mambo Kama haya kabla hujaandika chochote maana uwezo huo wa kuunda hoja ni mzuri but already corrupted by personal interest.
Jiulize Tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom