Elections 2010 Wagombea Urais 2010; Tetesi na zaidi ya tetesi

talhuda.jpg

Kumbe. Now it makes sense. Unajua kabla ya kushangaa habari ni vizuri ukajua source. If this is the source then it's not surprising at all.
 
Kama sikosei mkulu Joka Kuu alituonya kutohamishia nguvu zetu nyingi kwenye mambo ya udini udini ambayo hayana tija kwa taifa. Ya kaisari tunapaswa kumpa Kaisari na ya mungu tumpe mungu. Ya serikali si ndiyo hayo ya Kaisari jamani au nimekosea?

Ni vyema tuka-dwell kwenye mambo ya msingi yanayotuunganisha kama nchi na siyo mambo ya dini kila inapokuwa siku mpya.Jamani hebu tujaribu kuliangalia hili kwa makini.
 
Siku zote ni lazima tupige vita udini ukabila na ubaguzi wa aina yeyote ile.kusema kanisa katoliki linawaandaa MH.PM NA MH.MEMBE kuwa marais ni hoja isiyoingia akilini.

karibu mawaziri wakuu wote waliotangulia hawakuwayi kuwania urais!


Kanuni na taratibu za kumpata rais wa nchi yetu zipo na zitafuatwe kwa umakini mkubwa sana.
 
Naamini walio wengi bado hatutazami changamoto zinazotukabili katika misingi ya udini. Kutoka leo mpaka 2015 yapo mambo mengi yatakayojitokeza na inawezekana kabisa yakabadilisha mitazamo yetu kuhusu uongozi katika nafasi mbalimbali. Nawaonea huruma wale wanaokesha kutengeneza mazingira ya kufanya wahusika wa siasa ni lazima wawe wahusika wa dini zao. Naamini itakuwa ngumu sana.Tunataka viongozi na sio watu wataotuchanganya na mambo yao ya kidini.
 
karibu mawaziri wakuu wote waliotangulia hawakuwayi kuwania urais!

Wapo:

Nyerere?
Sumaye?
Msuya?
Malecela?
Dr Salim?

Hata hivyo nakubaliana na wewe habari hii ya Pinda na Membe kuandaliwa na kanisa haina ukweli.
 
Kama sikosei mkulu Joka Kuu alituonya kutohamishia nguvu zetu nyingi kwenye mambo ya udini udini ambayo hayana tija kwa taifa. Ya kaisari tunapaswa kumpa Kaisari na ya mungu tumpe mungu. Ya serikali si ndiyo hayo ya Kaisari jamani au nimekosea?

Ni vyema tuka-dwell kwenye mambo ya msingi yanayotuunganisha kama nchi na siyo mambo ya dini kila inapokuwa siku mpya.Jamani hebu tujaribu kuliangalia hili kwa makini.

KAMA YA KAISAR TUNATAKIWA KUMPA KAISAR MBONA KUNA WARAKA WA WAKATOLIKI? KWANINI YASISHUGHULIKE NA ya Mwenyezi Mungu? tusidanganyanye.

Jasusi.

Source ya habari hii nimeipata Mjengwa Blog jaribu kupitia uone kama haipo? hadi sasa ukitizama Mjengwa blog utaiona.
 
jamani we have to be careful, lisemwalo lipo? na kama halipo basi ni umbea tuu! anyway nadhan kwa wanaotafakali they will prepare mtu mwenye hulka ya kuongoza na kusimamia maslai ya nchi!
 
Ni vyema tuka-dwell kwenye mambo ya msingi yanayotuunganisha kama nchi na siyo mambo ya dini kila inapokuwa siku mpya.Jamani hebu tujaribu kuliangalia hili kwa makini.[/QUOTE said:
Ni kweli. Lakini hata hivyo habari yenyewe ni ya kipuuzi. Kanisa moja haliwezi kuandaa watu wawili kuchukua Urais nafasi ambayo ni ya mtu mmoja. Magazeti kama Al-Huda yana tabia ya "ku-sensionalize" habari kwa ajili ya kuuza.
 
Wapo:

Nyerere?
Sumaye?
Msuya?
Malecela?
Dr Salim?

Hata hivyo nakubaliana na wewe habari hii ya Pinda na Membe kuandaliwa na kanisa haina ukweli.

Umemsahau Joseph Sinde Warioba nae aligombea Urais 1995.ni Mzee Kawawa tu ndiye aliyeshika wadhifa wa uwaziri mkuu na hakugombea.
kama wote waliowahi kuwa mawaziri wakuu waligombea kwanini Pinda asijiandae na kuandaliwa kwenye nafasi hiyo? au Pinda ni tofauti na hao sita waliojitokeza kugombea?
 
Ni kweli. Lakini hata hivyo habari yenyewe ni ya kipuuzi. Kanisa moja haliwezi kuandaa watu wawili kuchukua Urais nafasi ambayo ni ya mtu mmoja. Magazeti kama Al-Huda yana tabia ya "ku-sensionalize" habari kwa ajili ya kuuza.

wewe ni mgeni kwenye siasa. kanisa lazima liwe na mtu zaidi ya mmoja,ili akikwama mmoja mwingine anakwenda. hapo nyuma ya hao wawili kuna Mark Mwandosya kama huna habari hii ndio habari.

Lowassa na JK walikuwa timu moja 1995 na wote waligombea.akishinda mmoja mwingine anachukua waziri mkuu au sehemu Nyeti.

kama habari ya Gazeti hili ni udaku kwanini wasipeleke mahakamani kusafishwa?

Membe mwenyewe kahojiwa na vyombo vya habari hivi karibuni akasema kuwa anaandamwa kwa vile atagombea urais.
 
Pinda akipewa uraisi basi mafisadi watakiona cha moto ni papo kwa papo tu ,akuna kulaza damu ,ila sasa hivi kuna uswahiba ndio unampa ugumu wa kumaliza kazi kwa haraka ,hajui amuanze nani amuache nani maana anaweza akabakia peke yake ikawa mbinde.
 
Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha amekana kubebwa katika nafasi ya uwaziri kiongozi kama ilivyodaiwa hivi karibuni na vyombo vya habari.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya baraza la wawakilishi Maisara Mjini Unguja kufuatia kauli zilizotolewa na Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Ali Abeid Karume katika mahojiano maalaumu na gazeti mmoja linalochapishwa wiki mara moja nchini kuhusu nafasi ya urais wa zanzibar.
Juzi gazeti moja litolewalo kila wiki liliripoti kwamba Balozi wa Tanzania Nchini Italia Ali Abeid Karume alisema kwamba wadhifa wa aliopewa waziri kiongozi ni wa kubebwa tu.
“Kama mtu anasema mimi nimeokotezwa na kubebwa sasa ajiulize yeye amefika hapo kwa uwezo wa nani….hata yeye alibebwa na na kufanyiwa hivyo na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye alimchagua kuwa balozi katika kipindi cha miaka kumi ya urais wake na sasa ni Rais Jakaya Kikwete ambaye amemchaguwa kubwa balozi wa Tanzania nchini Italia au amesahau hilo” alihoji Nahodha ambaye anaonesha hakufurahishwa na kauli ya Balozi Karume.
Waziri Kiongozi alisema hana sababu ya kujitangaza na kupita kila sehemu kwa sababu anafahamika na uwezo anao ambapo katika kipindi chote hicho amefanikiwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kuitaangaza ilani ya chama cha mapinduzi.
Nahodha alisema ni kweli wapo baadhi ya watu wanaohitaji kujitangaza na kupita kila sehemu kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuomba Rais wa Zanzibar kutokana na kutokuwa maarufu au hawafahamiki vyema kwa wananchi.
Alisema yeye binafasi hana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa tayari ni maarufu na ameshakuwa katika nafasi nyingi alizozikamata mbali ya kuwa waziri kiongozi kwa muda wa miaka tisa sasa.
“Uwezo ninao…sina sababu ya kujitangaza katika kuwania nafasi hiyo ya urais wakati ukifika nitafanya hivyo kwa kufuata utaratibu unaokubalika katika chama chetu lakini hivyo ni nani asiyenijuwa mimi Micheweni kote Pemba pamoja na Unguja yake mbona najulikana sana” alisema Nahodha na kuwashangaa wanaomsema.
Nahodha alisema kumekuwa na watu wengi ambao wanatajwa kutaka kuwania urais wa Zanzibar mwaka 2010 akiwemo yeye lakini amesema bado ni mapema kusema azma yake hiyo na wananchi kama kweli wana hamu ya kumsikia iwapo yeye anataka kuwania wadhifa huo basi wasiburi wakati ufike kwani hivi sasa wakati haujafika.
Hata hivyo Nahodha hakutaka kuwaeleza waandishi wa habari nia yake ya kutaka kugombea urais wa Zanzibar wakati ukiwadia lakini alitumia utaratibu wake wa kila siku wa kuuliza swali yule aliyemuuliza.
“Kama wewe umeongoza nafasi ya waziri kiongozi kwa muda wa miaka tisa utafanyaje? katika uamuzi wako hebu nambieni hilo”aliuliza waandishi wa habari swali hilo .
Waziri Kiongozi ni miongoni mwa watu wanaotajwa kutaka kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar 2010 ingawa mara nyingi anapoulizwa husema kwamba anapojitizama aktika kioo huwa anajiona ni mdogo na hapaswi kuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika nchi kutokana na muono wake wanavyojiona mwenyewe.
Lakini kauli yake hiyo ambayo aliwahi kuitoa mara kadhaa kwa waandishi wa habari katika kipindi chake cha kwanza cha kuwa waziri kiongozi imeanza kubadilika kila siku zinavyokwenda na ambapo sasa huwa anazungumza lugha nyengine kabisa na hiyo.
Nahodha aliwahi kunukuliwa akisema iwapo watu watamuona anafaa basi sawa lakini yeye binafsi anajiona hana uwezo huo kwa kuwa kioo kinamwambia hivyo lakini sasa inaonekana dhahiri ana nia na dhamira ya kuwania nafasi hiyo ya uongozi katika kipindi kijacho ambacho Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume anamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba.
Watu wengine ambao huwa wanatajwa kuwania kinyanganyiro hicho na kupewa nafasi kubwa ya ushindi kwa kuwa ndio chaguo la wana CCM Zanzibar ni Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilali ambaye katika uchaguzi uliopita alipata kura nyingi za wajumbe wa halmshauri kuu ya CCM Zanzibar lakini kwa mujibu wa utaratibu wa CCM alitakiwa kujitoa katika kinyanganyiro hicho kwa kuwa utaratibu ni kumuachia Rais aliyepo madarakani kumaliza ngwe yake ya mwisho ya uongozi.
Balozi Ali Karume anatajwa kuwepo katika orodha hiyo ambaye tayari ametangaza azma yake hiyo ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kufuatilia kumalizika kwa kipindi cha miaka kumi kaka yake Rais Amani Abeid Karume ifikapo mwakani 2010 .
Balozi Karume ni miongoni mwa mabalozi ambao wanashikilia nafasi za ubalozi kwa muda mrefu sasa tangu kipindi cha Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa balozi nchini Ubelgiji ambapo yeye ndio kiongozi wa mabalozi wote nchini.
Orodha ya wanaotaka kuwania nafasi ya urais Zanzibar ni kubwa ambapo wapo baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na ya jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwemo Makamu wa Rais Dk. Ali mohammed Shein, Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud, Waziri wa Muungano Mohammed Seif Khatib, na Balozi Seif Idd na wengine wengi.
Wengine kwa upande wa Zanzibar ni Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman


SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Pitting the undiplomatic top diplomat against the clueless Chief Minister one wonders who is a bit better off, for they all stink of ignorance.

The diplomat reeks of sheer ignobility. despite his storied pedigree.

The Chief Minister contradicts himself by saying that he will not announce running until the time is right, then goes on to imply he is running but will not give further comments until the time is right, hello, what does that amount to if not a premature announcement? .

This sort of "entertainment" would have been hilarious if it weren't so seriously tragic.
 
Back
Top Bottom