Wagombea Ubunge wagawa fedha kama njugu kanda ya ziwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea Ubunge wagawa fedha kama njugu kanda ya ziwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Apr 27, 2010.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nimesoma kwenye gazeti la kanda ya ziwa ingawa halimo kwenye mtandao
  Na Mathias Byabato.
  Ikiwa ni siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kusaini sheria inayolenga kudhibiti fedha chafu katika uchaguzi,sasa fedha zimeanza kugawiwa kama njungu miongoni mwa wananchi katika baadhi ya majimbo Mkoani Kagera.

  Kwa takribani wiki tatu sasa gazeti hili limekuwa katika uchunguzi wa suala hilo na limejiridhisha kuwa fedha zinagawiwa kwa wananchi hasa katika majimbo ya Bukoba Vijijini na Nkenge.

  Ugawaji wa fedha hizo unafanywa na wapambe wa baadhi ya wale wanaotarajia kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo tajwa na imefikia hatua watu wanajipanga mistari kupata mgao wa fedha za bure.

  Katika kata ya Kakunyu huko Nkenge wananchi waliongea na gazeti hili wamedai kutojua fedha hizo zinapotoka lakini wanaongeza kuwa wamekuwa wakipata mgao wa kati ya sh 500 na 2000 kila mwananchi na kuelezwa kuwa wataelezwa baadaye mtoaji wa fedha hizo.

  “Tunaletewa fedha za bure hapa tena za noti mpya mpya za sh 500,1000 au 2000 lakini kwa kuwa hatuelezwi zinapotoka na malengo yake sisi tunakula tu” Alisema mzee Novatus Kalila wa Kakunyu.

  Wananchi wa kata ya Kashenye huko Kanyigo walisema kuwa hivi sasa wamekuwa wakipokea wageni wanaotumwa na watu wanaotarajia kugombea ubunge kwa lengo la kuwagawia fedha.

  Wanakuja kwenye misiba,harusi na wakati mwingine kwenye mikutano ya vyama vya ujima hasa vya wanawake ambapo wanatoa fedha taslimu wakidai kuwa wametumwa na wagombea hao kama msaada kwao huku wakiongeza kuwa muda ukifika wasiwasahau.

  Katika wilaya ya Bukoba Vijijini,taarifa zinasema kuwa baadhi ya madiwani(majina tunayo) walikurupushwa hivi karibuni wakiwa katika harakati za kusambaza fedha kwa wananchi katika kata ya Nyakibimbili ambapo iliezwa kuwa walikamatwa baadaye na kutoa maelezo wa maafisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).

  Imeelezwa kuwa usambazaji wa fedha katika jimbo hilo unafanywa na wapambe wa wagombea ubunge katika jimbo hilo na kwamba wananchi wa jimbo hilo wanapata kati ya tsh 2000 na 5000 kila mtu.

  “Huu ni muda wa neema,hapa kuna mgao wa fedha karibu kila juma tunakuwa kwa (anataja kituo cha mgao) ambapo tunakusanyika kila mtu anapata chake ingawa tunaelezwa wazi kuwa zimetoka kwa (anataja) ili tumsaidie kumpitisha awe mgombea ubunge kupitia CCM.”Alisema Mkazi wa kata ya Nyakibimbili(tunahifadhi jina lake).

  Aidha taarifa tulizozipata wakati tukienda mitamboni zimeeleza kuwa kigogo mmoja wa CCM alikamatwa kuhusiana na ugawaji wa fedha,kanga,chumvi na sabuni kwa wananchi ingawa viongozi wa CCM wamekataa kuongelea suala hilo.

  Akiongea na gazeti hili ofisini kwake kuhusiana na hali hiyo Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Xavery Mhyella alisema kuwa Ofisi yake haina taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya wanasiasa au wapambe wanaogawa fedha katika majimbo hayo inagawa kuna ufuatiliaji unaofanywa na chombo hicho kuhusiana na masuala ya rushwa ikiwa ni kazi zake za kila siku.

  “Sisi tunaelimisha,kuzuia na inapobidi tunakamata lakini tupo katika ufuatiliaji katika majimbo ya uchaguzi kuona nani anatoa nini kwa malengo gani na ikidhibitika ni katika mazingira ya rushwa tutawakamata tu” Alisema.

  Aliongeza kuwa Sheria ya gharama za uchaguzi na sheria mama ya TAKUKURU zinawafanya waendelee na majukumu yao kama kawaida ya kufuatilia wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

  “Sheria inaturuhusu kuingia katika mchakato wa vyama kuona kama kuna dalili za rushwa ikiwemo kugawa zawadi,misaada au ligi za michezo na iwapo watatumia misaada hiyo kujinadi basi tutawakamata kwa kutoa rushwa” Alisema

  Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera Bw Sabby Rwazo alisema chama kimekwisha pokea malalamiko ya ugawaji wa zawadi na fedha katika majimbo hayo.

  “Ni kweli katika kamati zetu za chama tumekwishapokea malalamiko tena kwa barua kutoka kwa baaadhi ya wagombea wakilalamikia hali hiyo ikiwemo vitendo vya kuchafuana kwani mtu anaweza kuchafuliwa na wakati wa uteuzi chama kikampendekeza huyo huyo aliyechafuliwa” Alisema Rwazo wakati akihojiwa na gazeti hili kwa njia ya simu.

  Rwazo alifafanua kuwa ni marufuku mtu anayetarajia au aliyekwisha kutanagza nia ya kugombea udiwani au ubunge kupita kwa wapiga kura kujinadi kwani muda bado na kwamba hali hiyo inaweza kumfanya apoteze sifa za kupendekezwa kuwa mgombea kupitia chama hicho.
  “Kanuni haziruhusu mgombea kupita kwenye misiba au harusi kujinadi au kutoa zawadi zinazolenga kushawishi kuchaguliwa lakini hatukatazi watu kwenda kwenye misiba, watu waende lakini wasipige kampeini”Alisema.

  Ameongeza kuwa chama hicho kimejipanga kushinda majimbo yote ya uchaguzi na viti vyote katika mkoa wa Kagera kwani hivi sasa aslimia 95 ya viti vyote vya udiwani ni kutoka CCM wakati upande wa ubunge ni aslimia 100 kwa maana ya kuwa katika mkoa huo hakuna mbunge wa kutoka upinzani.

  Chanzo gazeti Malengo Yetu toleo la leo jumanne
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Rushwa ni Dondandugu! Haliponi hilo mpaka liende na mtu kaburini.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  sijui kama iko siku rushwa itaisha nchi hii ..
   
Loading...