Wagombea ubunge wa CHADEMA wale kiapo cha kutohama chama ndani ya miaka 5 vinginevyo ni bora wachaguliwe CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,615
141,439
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mkuu Yohane, wengi wao dau nono likiwekwa mbele yao hugeuka kuwa mateka wa rushwa na usaliti. Kwa kuwa huaidiwa kulipiwa mafao yao yote, madeni pamoja na kuhakikishiwa kupewa vyeo.
 
Kiapo si milele. Unamkumbuka, James Ole Millya yule Mbuge wa Simanjiro? Huyu alikula kiapo tena cha kimila kabisa na kunywa damu mbichi chini ya mti. Alihama Chadema na kuendelea na maisha yake. Siasa ni siasa sio eti unadai Siasa ni Kilimo.
 
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
Mpaka unatoa ushauri huo,kwani watapata mbunge hata mmoja safari hii?
 
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
Mwambieni huyo anayewaghilibu na kuliingiza Taifa hasara ya kurudia uchaguzi.
 
Tume haihusiki. Wananchi hawataki kuisikia Chadema. Imechafuka kabisa ni matapeli wa kisiasa.

Ushenzi, uhayawani na ukatili wa wazi unaofanyika kwenye chaguzi zetu ili ccm watangazwe washindi, hakuna mtanzania asiyeujua. Tunafahamu kila kitu na wala hatuhadithiwi.
 
Uzuri kila kitu hufanyika kwa uwazi na kila chama huwa na mawakala na hutakiwa kulinda kura za chama chao. Pia mawakala huwa wanajaza fomu zote zinazotakiwa na matokeo hupandikwa kwenye kila kituo ngazi zote. Kwa hiyo propaganda zako ni uswahili usio na mbele wala nyuma.
 
Kitabu changu kitakatifu kimenikataza kuapa, watu wanavunja viapo vya ndoa itakuwa hicho cha siasa, wacha kila mmoja aape lwa nafsi yake.
 
CCM waache tabia hii ya kuwarubuni hawa watu, Rushwa ni adui wa Haki, sintatoa wala kupokea rushwa.
 
Uzuri kila kitu hufanyika kwa uwazi na kila chama huwa na mawakala na hutakiwa kulinda kura za chama chao. Pia mawakala huwa wanajaza fomu zote zinazotakiwa na matokeo hupandikwa kwenye kila kituo ngazi zote. Kwa hiyo propaganda zako ni uswahili usio na mbele wala nyuma.

Sina chembe ya shaka na nilichokisema. Huo uhuni, ukatali na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi, umefanyika mbele ya macho yangu na wapiga kura wengine. Tena umefanyika kwa uratibu wa vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu watu wengi kudharau box la kura, kwa kiwango cha hali ya juu toka nchi hii ipate uhuru.
 
Maneno ya mshindwaji.
 
CCM waache tabia hii ya kuwarubuni hawa watu, Rushwa ni adui wa Haki, sintatoa wala kupokea rushwa.
Mimi mpaka leo bado nashangaa watu wazima na sharubu zao kulia na kalalamika kuwa wanarubuniwa. Sijui wakati wanarubuniwa wenyewe wanakuwa wapi 🤷‍♂️
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom