Wagombea ubunge wa CHADEMA wale kiapo cha kutohama chama ndani ya miaka 5 vinginevyo ni bora wachaguliwe CCM

Ninajua ni kwa kiwango gani ukweli huu unauma. Kungekuwa na ushindani tungeongelea mshindi na mshindwa, ila sio kwa upuuzi unaoendelea kwenye chaguzi zetu chini ya awamu ya tano.
Ngoja nicheke tu. Maana hao wananchi huko vijijini wanaofurahia umeme wa REA ambao haukatiki wakikusikia wanakupopoa mawe.
 
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
Muache kuwanunua
 
Ngoja nicheke tu. Maana hao wananchi huko vijijini wanaofurahia umeme wa REA ambao haukatiki wakikusikia wanakupopoa mawe.

Umeme ni haki yao, na wala sio hisani. Ila sioni mahusiano ya uhayawani, ukatali na ushenzi wa wazi kwenye chaguzi zetu, na uwepo wa umeme.
 
Hayo ya ukatili wa na ushenzi kwenye umeme huwa sio kweli. Umeme sio hisani lakini utashi wa kisiasa wa JPM na Ccm ndio umesababisha hayo yafanyike hivyo ni lazima apate kura 100%.
 
Mpango wa REA uko kabla Magufuli hajawa rais. Huna ujualo zaidi ya kupiga propaganda mfu hapa jukwaani. Narudia tena umeme popote hapa nchini sio hisani ya mtu yeyote, bali ni kodi za wananchi. Kura zinatolewa kwa utashi wa wapiga kura, na sio kwa vitisho na shuruti.
 
Tindo serikali ya Ccm imekuwepo toka tunapata uhuru. REA imekuwepo kabla JPM hajawa rais,lakini awamu hii ya tano vijiji vingi vimewekewa umeme. Kwa hiyo wametekeleza kwa asilimia kubwa kwa muda mfupi.Mpaka sasa ni 75% ya vijiji vya Tanzania. Tunachopima ni kasi ya utekelezaji.
 
REA ilianza lini? Kumbuka kila ukinunua umeme 3% inaenda kwenye mfuko wa REA. Kadiri wateja wanavyoongezeka mfuko unakusanya zaidi. Hivyo ni wazi kabisa kasi ya usambazaji itakuwa kubwa pia. Na hili kiongozi au chama chochote kitakachokuwa madarakani, kitawajibika kutekeleza mradi huo. Halafu hiyo % sasa hivi inatumika kama propaganda kwenye kila kitu. Kila mradi wa serikali sasa hivi, utasikia umetekelezwa kwa 70%+. Hivyo hizo % waeleze wenye upeo mdogo na propaganda za kikomunisti.
 
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
Huwezi kuwa na Imani na mbowe lakini huna Imani na wenzao

Chadema this year imeharibika Sana
 
REA ilianza lini? Kumbuka kila ukinunua umeme 3% inaenda kwenye mfuko wa REA. Kadiri wateja wanavyoongezeka mfuko unakusanya zaidi. Hivyo ni wazi kabisa kasi ya usambazaji itakuwa kubwa pia. Na hili kiongozi au chama chochote kitakachokuwa madarakani, kitawajibika kutekeleza mradi huo. Halafu hiyo % sasa hivi inatumika kama propaganda kwenye kila kitu. Kila mradi wa serikali sasa hivi, utasikia umetekelezwa kwa 70%+. Hivyo hizo % waeleze wenye upeo mdogo na propaganda za kikomunisti.
Tindo kama hakuna utashi wa kisiasa na kiongozi muadilifu hayo makato yote ya REA ingekuwa story kama huko nyuma. Mambo yamebadilika chini ya utawala wa JPM ndio maana unaona kwa muda mfupi mambo makubwa yamefanyika.
 
Ndio maana tunadai katiba mpya, itakayowezesha kuwajibisha watu wote watakaotumia fedha za umma kinyume na utaratibu. Hii kutegemea utashi wa mtu, kunatoa kichaka cha kuficha viongozi wezi, na kuishia kulindana.
 
Hata hii katiba ya sasa na sheria za nchi haziruhusu ufisadi na wizi wa mali za umma. Kwa hiyo katiba sio solution. Lazima muwe na viongozi kama JPM ambao hawajali matumbo yao.
 
Tatizo la ufisadi ndani ya nchi hii linachangiwa na rais kuwa na kinga ya kutoshitakiwa. Jaribu kuangalia mafisadi wote walipata backup ya rais wa nchi aliyekuwa madarakani, na inakuwa vigumu kuwachukulia hatua, maana lazima rais atashitakiwa pia. Hii kuona sasa hivi rais anazidi kusaka kinga ya kutoshtakiwa na viongozi wengine kadhaa, ni dalili kuwa sio waadilifu, ndio maana wanasaka kinga ili wapate nafasi ya kufanya wizi na uovu. JPM sio muadilifu, mtu muadilifu hawezi kuwa adui wa uwazi, na uhuru wa vyombo vya habari.
 
Kwani si wanatakiwa kushitakiwa wakiwa wanafanya kazi zao ila kupitia kwa Ag?
Bunge pia linaweza kumuondoa rais madarakani kama akifanya makosa na baadae kushitakiwa.
 
Ndio maana tunadai katiba mpya, itakayowezesha kuwajibisha watu wote watakaotumia fedha za umma kinyume na utaratibu. Hii kutegemea utashi wa mtu, kunatoa kichaka cha kuficha viongozi wezi, na kuishia kulindana.
Tuanze na chama.vyote vya siasa
 
Kwani si wanatakiwa kushitakiwa wakiwa wanafanya kazi zao ila kupitia kwa Ag?
Bunge pia linaweza kumuondoa rais madarakani kama akifanya makosa na baadae kushitakiwa.

Hakuna uwezekano wa hilo kutokea. Hizo mbinu zinatumika ili kuzuia kushitakiwa. AG anateuliwa na rais, tena hata uchaguzi wenyewe huwa ni wa hisani, hapo unategemea nini?
 
Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.

Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.

Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.

Maendeleo hayana vyama!
sio democracy hiyo ni utopora 🚩🚩🚩🚩
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom