Wagombea ubunge CCM Kakonko wapeta u DED

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
Mwaka 2015 katika jimbo la Buyungu - Kakonko walijitokeza makada sita (6) kugombea nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu. Makada hao waliojitokeza ni kama ifuatavyo:
1. Mhe. Eng. Christopher Chiza (Aliyekuwa mbunge - kura 10,249);
2. Bw. Msakila M. Kabende (Afisa Takwimu Mkoa Kagera - kura 3,689);
3. Eng. Modest Apolinary (Mtaalamu wa Madini - Arusha - kura 848);
4. Bw. Carlos Gwamagobe (Afisa Maendeleo ya Jamii Kakonko - kura 426);
5. Bw. Ernest G. Basaya (Mkurugenzi mstaafu - kura 107); na
6. Bw. Liberi Ndabita (Dereva wa gari ndogo - taxi driver - kura 89)

Katika uteuzi uliofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa wagombea wawili kati ya sita (6) - yaani namba 3 na 4 ndio wamepata kuteuliwa kuwa Wakurugenzi Watendaji katika mkoa Geita. Namba 1 hajateuliwa kwa kuwa shauri la kupinga matokeo ya ubunge liko mahakamani na huenda likahitimishwa 8/7/2016; mshindi wa pili vile vile hakubahatika kuwa ktk safu ya kundi la Magufuli - halikadhalika kwa mshindi namba 5 na sita.

TUKIO GUMU HUMKOMAZA BINADAMU
MUNGU AWATANGULIE WATEULE WA RAIS - AMINA
 
Yes nadhani uteuzi uliangalia sana watu waliojaribu kutafuta fursa ya ubunge kupitia CCM. Kwa hiyo it is official kwa sasa ili upate nafasi ya juu ya utendaji serikalini lazima uwe mwanasiasa. Siasa imechukua nafasi ya utendaji, ngoja tusubiri tuone kama hao makada watatuletea Tanzania ya viwanda?
 
DED wa Ludewa ndg. Ndatwa aliwahi kuomba kuchaguliwa ubunge na Mh Pombe jimboni Chato, kura hazikutosha.... jamaa huyu kwa fadhila ni zaidi ya mzee wa Msoga!
 
Back
Top Bottom