Wagombea Ubunge CCM hawafai wamevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano, kuwachagua ni kuridhia uvunjifu huo

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Ndugu wana Siha habari zenu,Ndugu wana kinondoni habari zenu ,poleni na Majukumu.

Leo nataka kuonesha namna gani viongozi waliojiozulu Ubunge na kujiunga na CCM na baadaye kupitishwa tena na CCM kugombea walivyovunja katiba ya jamhuri 1977.pia na CCM imebariki katiba yetu kuvunjwa.

Ndugu wana kinondoni na Siha ,oneni namna hao viongozi waliojiuzulu Jimbo la siha Godwin Mollel na Maulid Mtulia Jimbo la kinondoni namna ambavyo hawaijui katiba,wala hawajui wajibu wao kama wabunge.Mbunge ni sehemu ya Bunge ,Majukumu yao ni tofauti na serikali (executive).

Mbunge hupitisha bajeti,hutunga sheria na kisimamia serikali (executive) ,serikali kupitia mawaziri ndio hutekeleza Sera na kutekeleza Bajeti kwa uwangalizi mkubwa wa bunge kikatiba,wabunge hawaleti umeme wala hawaleti maji,wala hawajengi barabara hawa(zaidi ya miradi midogo midogo ya wananchi kupitia Mfuko wajimbo (CDCF-constituency development catalyst Fund,ambapo Kila Mbunge hupewa ila ukifuatilia Ripoti za mkaguzi mkuu,CAG wapo hata baadhi ya wabunge wa CCM wanaofuja fedha hizo,hivyo hutegemea uwadilifu wa kiongozi(Integrity) sasa Muadilifu hana sifa ya usaliti na kuiimbia Majukumu.

Wabunge husimamia serikali tuu kuleta maendeleo katika jimbo lake na serikali au wizara inawajibu wa kumjibu Mbunge swali lolote au kujibu hoja yeyote ya Mbunge ,sio ombi ni lazima kisheria (tunaita ministerial responsibilities

Sasa ona hawa waliojiuzulu walivyokeuka katiba ya Jamhuri ,kwa kumuunga Mkono .Mh.Rais Magufuli aliyekatika Muhimili ungine(Executive)na kujiuzulu ubunge kutoka bungeni sababu ya Rais, ikiwa yeye kama Mbunge anatakiwa kumsimamia Rais na Baraza lake lote liwajibike kuleta maendeleo, ile wenyewe wamekeuka katiba na kuondoka.soma .Ibara ya(63)(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

(Badala ya kuishauri na kusimamia serikali wenyewe wakaona kuwajibika ni kujiuzulu kumuunga mkono Mh.Rais badala ya kumshauri Rais azidi Fanya vizuri wakakimbia,CCM wamewasimamisha tena waliokimbia kuishauri na kuisimamia serikali)

(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge
laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu
mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano
ambayo yako katika wajibu wake;

(Wamekimbia kumuuliza waziri swali lolote la maslahi ya UMMA,Leo wanataka Ubunge wakafanye nini tena wakati walikimbia )

(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;

(Bajeti ndio maendeleo ya wananchi ,Bajeti ndio uchumi wa wananchi walipata nafasi wamekimbia ,eti wanamuunga Mkono Rais wanafuata nini tena ?)

(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda
mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa
katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya
kusimamia utekelezaji wa mpango huo;

(Wamekimbia sababu hawana IQ ndogo (uwezo wa akili yao kujadili mambo ni mdogo, wamekimbia Leo wanarudi tena kweli jamani?).

(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji
kuwapo sheria;

(Wamekimbia kutunga sheria hawawezi ,eti walienda kumuunga mkono Rais ,sasa waache GAME kwa wanaoweza,wenyewe watulie)

(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri
ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

(Walikimbia kuridhia mikataba sababu hawana huo ,uwezo wa kutoa hoja).

Hivyo kwa kutotekeleza haya kama wawakilishi wa wananchi Bungeni ,wamekeuka katiba ya Jamhuri ambayo waliapa kuilinda walipochaguliwa.

Mw.Nyerere alisemaje kwa kiongozi anayevunja katiba?

Baada ya 1985,alipostaafu kuwa Raisi,akiongea na waandishi wa habari kwake Msasani,alisema.

Katiba haiwezi kupuuzwa. Akishachaguliwa mtu ataapishwa kuilinda Katiba ili tuweze kumshtaki aliyeikiuka. Mtu yeyote ambaye hawezi kuilinda wala kuisimamia Katiba baada ya kuchaguliwa, hatufai anasema katika moja ya hotuba hizo.

Nyingine alisema,

Hatuwezi kupuuza Katiba..Katiba ndiyo sheria mama, mtu ambaye hawezi kuitetea Katiba,na kuilinda akishaapa hNyerere - Mwalimu Nyerere

Ndugu,Raia nampiga kura wa SIHA na Kinondoni unajukumu la kuilinda na kuitetea katiba,umia kuchagua mtu aliyevunja katiba,umia na epuka kuchagua kiongozi asiyejua wajibu wake.

Soma ibara ya ,26.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
na sheria za nchi.

Naomba niwaombe wakazi wa SIHA na KINONDONI, uchungu wa Adhabu kwao ya kuvunja katiba ,na kutojua wajibu wao ni kuwaadhibu kwa kuwanyima kura wao na CCM yao.,kuwa Mzalendo Linda katiba Yako, Kura yako Jimbo la Siha mpe Elvis Christopher Jimbo la kinondoni Mpe Ndug. Salum Mwalim

Naomba kama hupendi wavunja katiba Zambaza andiko hili Kila sehemu,kwa Kila Mwana Siha na Mwanakinondoni asifanye Makosa.

Hashtag yetu sote.

sema #NO mtulia ON BALLOT PAPER#

sema #NO molleli ON BALLOT PAPER#

Abdul Nondo.
0659366125.
0762082783.
Abdulnondo10@gmail.com
 
Ni ajabu kuwa hili hata Polepole na Mzee wake wameshindwa kuliona maana uteuzi wa hao watu kugombea sio wa chama bali ni wa kwao wenyewe
Sio kwamba hajui wamefanya hivyo ili kuwavutia wabunge wengine wa upinzani.
 
Mimi nilipoona jina "Nondo" nikafarijika kwa kudhani kuwa mleta hoja angetushushia nondo za uhakika, only to be disappointed!

I think this country has way too many bush lawyers! You obviously don't know why Tanzanian elected officials often choose to resign and switch political parties when they find themselves holding political beliefs that strongly clash with those of their current political parties! The reason is simple; the country's laws are flawed.

You know or should know that, in Tanzania, one cannot be a member of parliament, for example, without first being a member of a political party. As such, a member of parliament who loses his or her political party membership, automatically loses his or her parliamentary seat. There are numerous examples of people who lost their parliamentary seats because their political parties stripped them of their political party membership.

Mtulia, Mollel and the like couldn't fundamentally disagree with their political parties without risking expulsion. In the circumstances, resignation and political party switching should be the most logical option available to politicians who fundamentally disagree with their political parties. Certainly, if such politicians choose to hold on to their seats, they'll just be humiliated and expelled by their political parties!

Kusubiri kufukuzwa ni uwendawazimu!
 
Go back to school Dude

You don't know nothing about politics

Swissme
 
Ungefahamu kuwa bunge lina sehemu mbili na mojawapo no Rais wa JMT usingeandika haya yote.

Anyway umejitahidi kama mkulima wa jembe la mkono. Jitihada na nguvu nyingine sana, kitu anachozalisha sasa, duuuh.
 
Go back to school Dude

You don't know nothing about politics

Swissme

Umeipata wapi hiyo 'go back to school dude'?

Aisee unaipenda kweli. Umeipata kwenye tamthilia eenh.!??

Bravo, hiyo nzuri. Endelea kuipigapiga ndani ya miezi minne mitano hivi ukiendelea kuangalia tamthilia utapata msemo mwingine.
 
Ndugu wana Siha habari zenu,Ndugu wana kinondoni habari zenu ,poleni na Majukumu.

Leo nataka kuonesha namna gani viongozi waliojiozulu Ubunge na kujiunga na CCM na baadaye kupitishwa tena na CCM kugombea walivyovunja katiba ya jamhuri 1977.pia na CCM imebariki katiba yetu kuvunjwa.

Ndugu wana kinondoni na Siha ,oneni namna hao viongozi waliojiuzulu Jimbo la siha Godwin Mollel na Maulid Mtulia Jimbo la kinondoni namna ambavyo hawaijui katiba,wala hawajui wajibu wao kama wabunge.Mbunge ni sehemu ya Bunge ,Majukumu yao ni tofauti na serikali (executive).

Mbunge hupitisha bajeti,hutunga sheria na kisimamia serikali (executive) ,serikali kupitia mawaziri ndio hutekeleza Sera na kutekeleza Bajeti kwa uwangalizi mkubwa wa bunge kikatiba,wabunge hawaleti umeme wala hawaleti maji,wala hawajengi barabara hawa(zaidi ya miradi midogo midogo ya wananchi kupitia Mfuko wajimbo (CDCF-constituency development catalyst Fund,ambapo Kila Mbunge hupewa ila ukifuatilia Ripoti za mkaguzi mkuu,CAG wapo hata baadhi ya wabunge wa CCM wanaofuja fedha hizo,hivyo hutegemea uwadilifu wa kiongozi(Integrity) sasa Muadilifu hana sifa ya usaliti na kuiimbia Majukumu.

Wabunge husimamia serikali tuu kuleta maendeleo katika jimbo lake na serikali au wizara inawajibu wa kumjibu Mbunge swali lolote au kujibu hoja yeyote ya Mbunge ,sio ombi ni lazima kisheria (tunaita ministerial responsibilities

Sasa ona hawa waliojiuzulu walivyokeuka katiba ya Jamhuri ,kwa kumuunga Mkono .Mh.Rais Magufuli aliyekatika Muhimili ungine(Executive)na kujiuzulu ubunge kutoka bungeni sababu ya Rais, ikiwa yeye kama Mbunge anatakiwa kumsimamia Rais na Baraza lake lote liwajibike kuleta maendeleo, ile wenyewe wamekeuka katiba na kuondoka.soma .Ibara ya(63)(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

(Badala ya kuishauri na kusimamia serikali wenyewe wakaona kuwajibika ni kujiuzulu kumuunga mkono Mh.Rais badala ya kumshauri Rais azidi Fanya vizuri wakakimbia,CCM wamewasimamisha tena waliokimbia kuishauri na kuisimamia serikali)

(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge
laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu
mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano
ambayo yako katika wajibu wake;

(Wamekimbia kumuuliza waziri swali lolote la maslahi ya UMMA,Leo wanataka Ubunge wakafanye nini tena wakati walikimbia )

(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;

(Bajeti ndio maendeleo ya wananchi ,Bajeti ndio uchumi wa wananchi walipata nafasi wamekimbia ,eti wanamuunga Mkono Rais wanafuata nini tena ?)

(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda
mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa
katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya
kusimamia utekelezaji wa mpango huo;

(Wamekimbia sababu hawana IQ ndogo (uwezo wa akili yao kujadili mambo ni mdogo, wamekimbia Leo wanarudi tena kweli jamani?).

(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji
kuwapo sheria;

(Wamekimbia kutunga sheria hawawezi ,eti walienda kumuunga mkono Rais ,sasa waache GAME kwa wanaoweza,wenyewe watulie)

(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri
ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

(Walikimbia kuridhia mikataba sababu hawana huo ,uwezo wa kutoa hoja).

Hivyo kwa kutotekeleza haya kama wawakilishi wa wananchi Bungeni ,wamekeuka katiba ya Jamhuri ambayo waliapa kuilinda walipochaguliwa.

Mw.Nyerere alisemaje kwa kiongozi anayevunja katiba?

Baada ya 1985,alipostaafu kuwa Raisi,akiongea na waandishi wa habari kwake Msasani,alisema.

Katiba haiwezi kupuuzwa. Akishachaguliwa mtu ataapishwa kuilinda Katiba ili tuweze kumshtaki aliyeikiuka. Mtu yeyote ambaye hawezi kuilinda wala kuisimamia Katiba baada ya kuchaguliwa, hatufai anasema katika moja ya hotuba hizo.

Nyingine alisema,

Hatuwezi kupuuza Katiba..Katiba ndiyo sheria mama, mtu ambaye hawezi kuitetea Katiba,na kuilinda akishaapa hNyerere - Mwalimu Nyerere

Ndugu,Raia nampiga kura wa SIHA na Kinondoni unajukumu la kuilinda na kuitetea katiba,umia kuchagua mtu aliyevunja katiba,umia na epuka kuchagua kiongozi asiyejua wajibu wake.

Soma ibara ya ,26.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
na sheria za nchi.

Naomba niwaombe wakazi wa SIHA na KINONDONI, uchungu wa Adhabu kwao ya kuvunja katiba ,na kutojua wajibu wao ni kuwaadhibu kwa kuwanyima kura wao na CCM yao.,kuwa Mzalendo Linda katiba Yako, Kura yako Jimbo la Siha mpe Elvis Christopher Jimbo la kinondoni Mpe Ndug. Salum Mwalim

Naomba kama hupendi wavunja katiba Zambaza andiko hili Kila sehemu,kwa Kila Mwana Siha na Mwanakinondoni asifanye Makosa.

Hashtag yetu sote.

sema #NO mtulia ON BALLOT PAPER#

sema #NO molleli ON BALLOT PAPER#

Abdul Nondo.
0659366125.
0762082783.
Abdulnondo10@gmail.com

Aisee ndugu Abdul nondo umechambua vizuri sana

Tatizo lililopo hapo Tanzania ni ujinga , umasikini sasa hivi yameongezeka upumbavu na uoga haya uliyoyaandika nina uhakika 60% ya wabunge wa ccm hawayajui haya kama hao weneyewe hawayajui kweli mwananchi wa kawaida atayajua kweli hapo Tanzania????

Wakishawekewe taarabu za TOT na mipasho amsha amsha , push ups jukwaani hizo kwao ndio Sera

Asilimia kubwa ya wananchi ni washabiki wa kisiasa na sio kwenye kujua na kudai haki zao na kutekeleza wajibu wao
 
Umeipata wapi hiyo 'go back to school dude'?

Aisee unaipenda kweli. Umeipata kwenye tamthilia eenh.!??

Bravo, hiyo nzuri. Endelea kuipigapiga ndani ya miezi minne mitano hivi ukiendelea kuangalia tamthilia utapata msemo mwingine.

Sawa mama pole pole.

Swissme
 
Back
Top Bottom