Wagombea hawaruhusiwi kuwa mashahidi katika kuhesabu kura? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea hawaruhusiwi kuwa mashahidi katika kuhesabu kura?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masauni, Oct 6, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama tunavyojua ni ukweli usiopingika kuwa CCM itatumia mbinu nyingi kutaka kuiba kura ili ionekane imeshinda. Nakumbuka mwaka 1995 wakati Balozi paul ndobo akigombea jimbo la musoma kupitia NCCR-Mageuzi. CCM walipoona kwamba Paul ndobo ameshinda walienda katika kituo cha kuhesabia kura na kutaka kubadilisha matokeo. Thank God Paul ndobo mwenyewe alikuwepo pale kituoni na baada ya mabishano makubwa paul ndobo aliwaambia CCM atakaye taka kubadilisha matokeo ya kura kinyume na yalivyo nitampiga risasi hapahapa!! na ccm walipoona mzee ndobo hatanii walikubaliana matokeo yawe kama yalivyo na hapo ndobo akatangazwa mshindi. Waungwana ebu naomba mnifahamishe sasa utaratibu huu wa wagombea kuwepo katika vituo ulishafutwa? Pia jambo jingine naomba tutoe ushauri kwa chadema jinsi gani watalinda kura zao!
   
 2. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Jimbo la Musoma liliwahi kuchukuliwa na upinzani??? Naomba tukumbushane plz....
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CUF inashindaje kule Pemba?
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes mwaka 1995. Balozi wetu mstaafu nchini Urusi Paul Ndobo
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hili na mimi linanipa wasiwasi. Nimemsikia Dr. Slaa akisema mwaka huu tutalinda kura zetu haitapotea hata moja. Lakini hajawa wazi ni mbinu zipi zitakazotumika. Ukichukuliwa ufinyu wa mtandao wa CHADEMA huko vijijini (hata baadhi ya maeneo mijini) na ukweli kwamba vyombo vya mabavu vya dola vimeishatangaza nia ya kuingilia kati kwa niaba ya CCM, kuna kigiza kinatanda.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  uteuzi makini wa mawakala ambao wametosheka ndiyo mwisho wa JK na ngome yake ya wezi na wabadhirifu wa CCM
   
Loading...