Wageni wanaoitembelea awamu ya tano na ahadi zao

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,065
18,358
Habari wanajamvi,
Tangu awamu ya tano ya mheshimiwa JPM imeingia madarakani kuna wageni wengi kutoka mataifa mbali mbali wamekuwa wakija nchini mwetu na kumwaga ahadi kede kede, nyingine za kuombwa na nyingine ni wao wenyewe kujitolea .

Kumezuka malumbano kuna wananchi wengine wanasema hao wageni wanaokuja na kutoa ahadi hizo hawana tija kwa taifa na ahadi zinazotolewa kwa jicho la kawaida zinaonekana utekelezaji wake ni mgumu hivyo kwa lugha ya hapa nyumbani tuziite ahadi hewa.
Sasa uzi huu uwe maalumu tukumbashane nani alikuja na aliahidi nini huku tukisubiri utekelezaji wa ahadi hizo.
Naomba ieleweke si kwa nia mbaya ila ni kuweka kumbu kumbu sawa ili wale wanaosema hizo ahadi hazitekelezeki pindi mambo yatakapokuwa mazuri siku zijazo wao wawe wa kwanza kwenda airport kuwapokea wageni watakao kuwa wanakuja kwani watakuwa na mifano inayoshikika(halisi) kabisa

Na upande mwingine mwingine ikiwa hazitatekelezwa kama wenzetu wanavyosema siku zijazo tujifunze kuomba vitu vinye uwezekano wa kutekelezeka.
Mimi nianze na mfalme wa Morocco huyu licha ya mikataba mbalimbali(TUMEMUOMBA) kwasababu raisi anafanya kwa niaba yetu sote;
1.Atujengee msikiti mkubwa daresalaam
2.Atujengee uwanja wa mpira mkubwa kuliko ule wa taifa huko Dodoma

Naomba na wenzangu ongezeeni nyingine mnazokumbuka ,Lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa!

Karibuni
 
~~>>>Ordinary person lazima atembelewe na watu ordinary..........
 
Waziri mkuu wa ethiopia ameahidi kutuuzia umeme kwa gharama nafuu
 
Wakati Ethiopia ni nchi ya pili Dunia kwa kuwa na wananchi wengi wasio na huduma ya umeme!!
 
Na Bado ahadi za wachina.. Wazir mkuu wa india.. Kiongoz wa mabohara.!!!
 
~~>>>Ila hii ya Ethiopia kutumia Bandari ya Dar kisha watumie ndege kusafirisha mizigo ni kali zaidi

Hao wafanyabiashara waache Bandari ya Djbout waje Dar
Jamani watanzania sasa tunachukuoiwa kama hatuna akili. Kenya, Somalia kote huko wana bandari. Sasa Djbout ndio wapo puani kabisa alafu waje bongo. Kwa kuwa tuna nn cha zaidi.
 
Bandari ya djibuoit iko mita chache kutoka ethiopia leo wavuke mombasa,kismayu kuja bandari ya bongo kweli?
 
Jamani watanzania sasa tunachukuoiwa kama hatuna akili. Kenya, Somalia kote huko wana bandari. Sasa Djbout ndio wapo puani kabisa alafu waje bongo. Kwa kuwa tuna nn cha zaidi.


~~~~>>>>Raisi anasema kontena za Ethiopia zitapelekwa kwa kutumia Ethiopia Airways...........



Haaaaa!!!!Haaaaa!!
 
Back
Top Bottom