Wageni wana haki ya kuamini Kilimanjaro haipo Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wageni wana haki ya kuamini Kilimanjaro haipo Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, May 19, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wageni wana haki ya kuamini Kilimanjaro haipo Tanzania Send to a friend Tuesday, 10 May 2011 09:58


  [​IMG] Mlima Kilimanjaro

  Mhariri,
  DHANA ya kwamba Tanzania tumekuwa hatufaidi maliasili zetu kama vile utalii, madini , pamoja na mlima Kilimanjaro, na badala yake fursa hii inatumiwa na nchi za wenzetu, dhana hii inazidi kupata mashiko kutokana na kile nitachokiita kushindwa kujitambua.
  Nasema hivyo nikimaanisha kwamba bado watalii wengi wanazidi kuaminishwa kwamba, nirahisi kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kenya kuliko Tanzania.
  Lakini bado serikali kwa kupitia mamlaka za mawasiliano na utalii hawajaona umuhimu wa kudhibiti habari au taarifa potofu zinazoingia mara tu unapoingia Wilaya jirani na Mlima Kilimanjaro.
  Mfano mzuri ukiingia Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro utakaribishwa na ujumbe mfupi (sms) toka Kenya katika baadhi ya mitandao ukiambiwa "umeingia Kenya" au "karibu Kenya” na kupata maelekezo ya huduma kwa nchi hiyo.
  Zaidi ya hapo utalakiwa na vyombo vya habari vyenye matangazo makini na yakudhihirisha utaifa wao kutoka Kenya, Vyombo hivyo ni kama vile KBC idhaa ya taifa, Mwanedu FM, Citized radio, Milele FM na nyinginezo lukuki.

  Wakati huo kwa Tanzania ni redio mbili tu zinazosikika vizuri, ambazo ni Killi FM na Sauti ya Injili ambazo zote ni za palepale mkoani Kilimanjaro.Hivyo basi kwanini watalii wasione mlima upo Kenya, au ni vema kupitia Kenya kuliko Tanzania?.

  Wakati umefika Serikali kuangalia maeneo yenye faida kubwa inayopotea pasipo sababu na isiwe Kilimanjaro tu, ila maeneo yote yenye thamani kubwa katika uchumi wa Taifa.
  Mecky b.Richard, 0787 882190

  kwa hisani ya gazeti la Mwananchi


   
 2. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hilo nalo neno. Ila serikali yetu mmmmmmmmmmmmm
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ishu sio serikali tu....NA SISI TUMEFANYA JITIHADA ZIPI????? AU KILA KITU SERIKALI?
   
Loading...