sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,032
Video ya utangulizi hii nasisitiza sana uiangalie mpaka mwisho, utapata picha kamili kabla hujasoma hii maada
Tangu nimezaliwa hapa nchini ma hadi sasa nikiwa na miaka 31 kuna mengi nimeyaona na kujifunza katika hii nchi, kitu kimoja wapo ni thamani kubwa mno anayopewa foreigner kuzidi mwananchi, na hao wageni ninaowazungumzia ni watu wa bara la ulaya (wengi wazungu), wakifuatiwa na watu wa bara la asia (sana sana waarabu)
Nitaanza kuchambua matukio kadha na kadha yaliyonisukuma kuandaa hii maada.
KUWA KIVUTIO KIKUBWA WAPITAPO MITAANI
Hapa nimeshudia matukio kadha na kadha, mzungu/mjapani anapopita mitaani watu wengi hunshangaa, na wengine huanza kumpa salamu hata kwa kiingereza kibovu (hey, how you doing, whats up,n.k) lugha ikikataa hata ishara hutumika, Ni kama anakuwa na positive attention kubwa mno
KUWA NA DHANA YA KUPENDA ZAIDI KUAJIRIWA NA MZUNGU UKIACHANA NA SERIKALI
Hapa wengi wanapokosa ajira serikalini huwa na dhana ya kwamba sehemu nzuri inyofatia ni kwa mzungu, ikumbukwe nae mzungu anafukuza kazi kama mtanzania, mzungu hataki mchezo kwenye kazi kama mtanzania, mzungu yupo kwajiiya faida kama mtanzania.
KUSHUGHULIKIWA KWA UHARAKA NA UMAKINI KWENYE OFISI BILA RUSHWA
Nakumbuka niliwahi kufanya kazi sehemu flani hivi, kuna vibali flani vilikuwa vikitoka kwa biashara flani, wengi walikuwa wanatoa na kitu kidogo ili mambo yaende fasta kidogo, Ila kuna siku alikuja jamaa flani wa sweeden kavaa kikaptura, alifanyiwa haraka tu bila hata kutoa cha ziada, alipotala kuondoka pia alipewa kitabu cha wageni kusaini, nikaona hapa kuna tatizo,Ofisi ya umma mtu mweusi hasa mbongo ukivaa ndala na kipensi hutaruhusiwa kuingia ndani,ila mzungu akivaa kipensi na ndala watamruhusu
HUPEWA THAMANI KWENYE MAHUSIANO YA URAFIKI NA MAPENZI
Tukianza kwenye mapenzi hapa, vijana wengi hupenda ku date na wazungu na hili halina mjadala, wana misemo yap kwamba wanasafosha nyota kwa mwarabu / mzungu. Ukija kwenye urafiki pia ni hivyo hivyo.
KUSAMEHEWA SANA PALE WANAPOKOSEA
Mnaweza kupanga foleni, akatokea mzungu/mwarabu/mjapani, n.j yeye akapita tu ila hakuna wwa kimkoromea tofauti na sisi tukifanya hivi,
Hali inakuwa tofauti sisi tukienda huko kwenye nchi zao hasa ambazo wamejazana wao kama ugiriki, romania, urusi, n.k