MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Salaam wanaJF! napenda kuchukua nafasi hii kuwashirikisha juu ya utapeli unaofanywa na wanaojiita waganga wa kienyeji(siyo wataalam wa tiba za asili na mitishamba). wengi wanaliwa pesa zao bure lakini hamna tiba. waganga wanajidai kuwa na nguvu za ziada za kutatua karibu kila aina ya tatizo. mtu mmoja kawaendea baadhi ya waganga na kubaini utapeli wao. alijifanya kapotelewa na mke anataka kujua aliko. mganga kamwambia yuko Makambako na atamsaidia kumpata. kumbe jamaa hana mke. alipomwambia amtafutie aliko akatoa pesa ila mganga baada ya cku hayupo. wengine badala ya kuwapeleka hospitali ndugu zao wanashinda kwa hawa 'masangoma' hadi wagonjwa wanakufa.hata hizo hirizi na vitu vya namna hiyo havina nguvu yoyote. ni kutaka kututia hofu na kula hela zetu. tuwe makini.