Waganga wa Kienyeji wamgomea Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waganga wa Kienyeji wamgomea Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzalendoHalisi, Jan 26, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Yaani hawa waganga wataendelea na shughuli zao tuu..hawatambui kauli ya Pinda Kufuta Leseni zao na kuwataka waombe leseni upya!

  Je huu ndo utawala wa Sheria?

  Au Watz hatuigopi serikali?

  Sijui yaani nihamie kule China!!!!

  We acha tu!

  Source: BBC NEWS | Africa | Tanzania witchdoctors flout ban
   
 2. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Source ya mauaji ya albino siyo waganga wa kienyeji. Ni jamii kwa ujumla. Waganga wa kienyeji huwa wanasema tu wateja wao wanachotaka kusikia. Yaani amayetoa solution ya tatizo na muhisika (anayeenda kwa mganga) mwenyewe.

  Watu inabidi tufanye utafiti na siyo kujisemea tu kuhusu waganga wa kienyeji. In fact, mganga hamwambii mteja wake kitu kipya. Ila huwa anamwambia kilekile mteja wake anachokiamini tayari.

  Ukienda kwa mganga, kwa kawaida atakuuliza maswali mengi na kwa namna mbalimbali. Lakini katika maswali hayo, utakuwa umemwambia solution ya tatitzo wewe mwenyewe (au kitu unachokiamini kikifanyika utapona au utapata pesa) na yeye anachofanya ni kurudia tu ulichomwambia au unachokiamini na kufikiri kuwa ni yeye aliyekwambia. Jamani fanyeni utafiti, please!
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  serikari nayo haiko serious!!!! huyu wa tabata aliyepaka mtu mazinzi na kudai madondoka na ungo toka mbeya wamemfanya nini? waganga wa namna hii ni sumu
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ni nini tafsiri hasa ya Mganga wa Kienyeji? Mganga wa Tiba za Jadi? Mtu anaye prescribe namna ya kupata utajiri au kufanikiwa nae ni mganga?
   
 5. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,270
  Likes Received: 4,245
  Trophy Points: 280
  Hao wanasiasa ndio wanategemea hao waganga sasa wanaweza kuwazuia ?
   
 6. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Mganga wa kienyeji ni mtu mwenye utaalamu wa mitishamba na namna inavyotibu baadhi ya magonywa ya binadamu au mifugo. Katika hao waganga wa kienyeji kuna wale pia wanaotoa dawa za kinga kwa jili ya magonjwa fulani, mikasa katika maisha na wengine wanatoa ushauri namna ya kukabiliana na matukio fulani fulani katika maisha na pia kuna wanao'control' nguvu ya wachawi isizidi. Haya ni baadhi ya makundi ninayoyafahamu.

  Kundi hili ya mwisho linajaribu kutafsiri dalili fulani ambazo watu wa kawaida wanaweza kuona ni 'mysterious' au zile ambazo haziko wazi sana katika maisha ya watu na ku'attribute' kwa kazi ya hao wachawi.

  Mfano, ukipita kwenye miti mikubwa usiku utahisi (feel) hali ya joto. Hii ni hali ya kawaida kwa miti kama tulivyojifunza kwenye Bilogy lakini baadhi ya waganga wanaweza kutafsiri kuwa ni wachawi wanafanya mkutano huku wakiota moto. Pia kuna wale wanaoota usiku na kuamka na kuanza kutembea nje.

  Kama ikitokea wakazinduka wakiwa bado nje - tuseme kama umbali wa mita 300 hivi kutoka nyumbani na kwa kuwa mara nyingine huwa wanabeba shuka au nguo zao za kuvaa na wengine wanaenda wakiwa uchi - basi wanaweza watu hawa wakadhani wamechukuliwa kichawi au watu wakawaaminisha kuwa wao wenyewe ni wachawi. Watu kama hawa wakienda kwa mganga atawaambiwa kuna mtu anawachezea.

  Na mara nyingi mganga hatakwambia huyo mtu ila atajaribu kutafuta njia ya kukuuliza wewe umwambie ni nani unayemfikiria kuwa amefanya hivyo. Kisha atakupa dawa ili asirudie kukufanyia hivyo na anaweza kukupa masharti fulani ya kufanya kabla ya kulala.

  Hivyo, inaweza kutokea kuwa ndoto za kuota usiku na kutembea zinaweza kupungua au zikakoma kabisa na ikitokea vile huyo mganga anaoneka kuwa ni mtaalamu sana na kila anayedhani ana ndoto kama hizo ataambiwa aende kwa mganga fulani ambaye ana dawa ya kutibu au kuzuia wachawi wasisumbue.

  Babu yangu alikuwa mganga na nyumba yake ilikuwa imejaa dawa kila sehemu. Na alikuwa akitembelea baadhi ya vijiji alikuwa akiwataja wachawi kwa majina. Lakini kabla ya kufa alisema uganga wa aina hii (kuhusu kuwadhibiti wachawi) ni usanii mtupu!
   
Loading...