Waganga wa Kienyeji toka Tz waula Kenya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,375
2,000
WAGANGA wa kienyeji kutoka Tanzania wamevuka mpaka na kuingia kaunti ya Migori nchini Kenya ili kujinufaisha na mgomo unaoendelea wa wahudumu wa afya.

Na katika kaunti ya Narok, wakazi waliokata tamaa wanatafuta tiba kwa waganga hao wa mitishamba. ‘Matabibu’ hao wamefungua ‘kliniki’ za muda Migori, Kehancha na katika mpaka wa Isebania na kudai wanatibu maradhi yote.

Wengi wao wametokea wilaya ya Tarime baada ya kusikia kwamba hospitali zote za umma nchini zimefungwa kufuatia

mgomo huo ulio katika wiki yake ya pili: “Tumekuja kuwasaidia ndugu na dada zetu wa Kenya. Bei yetu sio ya juu kama ile ya hospitali za kibinafsi,” alisema Bw Rashid Mohammed, anayedai amekuwa daktari wa mitishamba kwa miaka 20.

Ameweka kliniki katika mtaa wa Nyasare katika mji wa Migori ambako anasema huwahudumia wagonjwa takriban 20 kila siku. Ada ya kumwona ni Sh100 nayo gharama ya dawa ni kati ya Sh500 na Sh10,000 kulingana na aina ya ugonjwa.

Baadhi ya matabibu hao wanatumia ‘majini’ kubaini ugonjwa na taabu zinazowakumba watu: “Mtoto wangu alikuwa na malaria kali pamoja na kuhara damu lakini baada ya kunywa kinywaji kama uji hivi, sasa anahisi vyema zaidi,” alisema Bi Elizabeth Anyango, mama wa watoto sita.

Aliomba wahudumu wanaogoma kurudi kazini ama wengine wachukue nafasi zao kwani watu wengi hawawezi kumudu gharama ya hospitali za kibinafsi wala madaktari wa mitishamba: “Mgonjwa asiye na senti atakufa tu kwani hata hawa Watanzania hawatibu watu bure’’, alisema.

Katika kaunti ya Narok, mahojiano ya gazeti la Taifa Leo yalipata kuwa wagonjwa wengi wanaoishi kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wanavuka mpaka na kuingia mataifa jirani ya Afrika Kusini kusaka matibabu katika hospitali za Uaso, Loliondo na Ngorongoro: “Tumeamua kusaka tiba mbadala kama mababu zetu walivyofanya vizazi na vizazi kabla dawa za kisasa kuwadia. Hatuwezi kungoja tu watu wetu wakifariki ilhali tuko na madaktari wa kienyeji, dawa za mitishamba na hospitali nchini Tanzania,” alisema John Mpoe, mkazi wa eneo la Olderkesi kwenye mpaka wa mataifa hayo mawili.

Source: Mgomo wa Madaktari Kenya: Waganga kutoka Tanzania waona fursa ya kuchangamkia - wavuti.com
 
ijoz

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
731
1,000
Kuna mtu mmoja aliwahi niambia kuwa,ukitaka kuteka akili ya mtu,mkamate kwenye afya,chakula na pesa. Hili naliamini kwenye hii habari,matangazo mengi ya waganga wa kuagua na uanzishaji wa makanisa.
 
Jonatus

JF-Expert Member
Dec 16, 2013
1,401
1,500
duh kweli afya sio kitu cha kuchezea utafanya juu chini mgonjwa apate huduma
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
WAGANGA wa kienyeji kutoka Tanzania wamevuka mpaka na kuingia kaunti ya Migori nchini Kenya ili kujinufaisha na mgomo unaoendelea wa wahudumu wa afya.

Na katika kaunti ya Narok, wakazi waliokata tamaa wanatafuta tiba kwa waganga hao wa mitishamba. ‘Matabibu’ hao wamefungua ‘kliniki’ za muda Migori, Kehancha na katika mpaka wa Isebania na kudai wanatibu maradhi yote.

Wengi wao wametokea wilaya ya Tarime baada ya kusikia kwamba hospitali zote za umma nchini zimefungwa kufuatia

mgomo huo ulio katika wiki yake ya pili: “Tumekuja kuwasaidia ndugu na dada zetu wa Kenya. Bei yetu sio ya juu kama ile ya hospitali za kibinafsi,” alisema Bw Rashid Mohammed, anayedai amekuwa daktari wa mitishamba kwa miaka 20.

Ameweka kliniki katika mtaa wa Nyasare katika mji wa Migori ambako anasema huwahudumia wagonjwa takriban 20 kila siku. Ada ya kumwona ni Sh100 nayo gharama ya dawa ni kati ya Sh500 na Sh10,000 kulingana na aina ya ugonjwa.

Baadhi ya matabibu hao wanatumia ‘majini’ kubaini ugonjwa na taabu zinazowakumba watu: “Mtoto wangu alikuwa na malaria kali pamoja na kuhara damu lakini baada ya kunywa kinywaji kama uji hivi, sasa anahisi vyema zaidi,” alisema Bi Elizabeth Anyango, mama wa watoto sita.

Aliomba wahudumu wanaogoma kurudi kazini ama wengine wachukue nafasi zao kwani watu wengi hawawezi kumudu gharama ya hospitali za kibinafsi wala madaktari wa mitishamba: “Mgonjwa asiye na senti atakufa tu kwani hata hawa Watanzania hawatibu watu bure’’, alisema.

Katika kaunti ya Narok, mahojiano ya gazeti la Taifa Leo yalipata kuwa wagonjwa wengi wanaoishi kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wanavuka mpaka na kuingia mataifa jirani ya Afrika Kusini kusaka matibabu katika hospitali za Uaso, Loliondo na Ngorongoro: “Tumeamua kusaka tiba mbadala kama mababu zetu walivyofanya vizazi na vizazi kabla dawa za kisasa kuwadia. Hatuwezi kungoja tu watu wetu wakifariki ilhali tuko na madaktari wa kienyeji, dawa za mitishamba na hospitali nchini Tanzania,” alisema John Mpoe, mkazi wa eneo la Olderkesi kwenye mpaka wa mataifa hayo mawili.

Source: Mgomo wa Madaktari Kenya: Waganga kutoka Tanzania waona fursa ya kuchangamkia - wavuti.com

Mie hapo kwenye red bado sijaelewa...nahisi viroba bado vipo kichwani.Nisaidieni ufafanuzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom