Waganga wa kienyeji na uchaguzi mwaka huu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waganga wa kienyeji na uchaguzi mwaka huu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mpeni sifa Yesu, Jun 12, 2010.

 1. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Miaka yote tz tunajua wakati kama huu waganga wa kienyeji ndio wanatajirika kwa pesa toka wa wanasiasa....hivi ni lini tutafuta kabisa huu upupu unatuchafulia sifa taifa letu?....jamani mimi hata nikitembea nchi gani sasahivi, ni immigration na office muhimu tu ndio zitajua kama natoka tz,...ni aibu kuonekana kuwa unatoka tz watu wanaona kama wewe ni mwuaji...uingereza watu hawana hamu na tz kutokana na matangazo mengi ya albino wanaouawa...

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mimi nikiwa Mganga wa kienyeji ningekutafuta wewe Mpeni sifa Yesu ili uwe muhanga wa kushinda huu Uchaguzi unaokuja kusema kweli hao Waganga wanaofanya Vitendo vya kuawatowa Muhanga ndugu zetu Maalbino kusema kweli hao Waganga wengi wao ni Waongo watupu watu hutowa muhanga wa mbuzi ,Ng'ombe,Jogoo, kondoo na Wanyama wengine sijawahi kusikia watu hutowa muhanga wa Albino eti ndio awe Tajiri au awe ndio mshindi kwenye kugombea Ubunge au mambo yanayohusu vyama vingi huo ni utapeli wa hao Waganga na wengi wa hao Waganga wa Kienyeji haswa kwa wakati huu ni Waongo wakubwa na Matapeli wakubwa wanawauwa maalbino wasiokuwa na hatia Mungu atawaunguza kwa Moto wake Mkali sana Ee Mwenyeezi Mungu walinde Maalbino wasiokuwa na hatia ameen.
   
 3. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #3
  Jun 13, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mambo yamebadilika saana, ndio sababu binadam wanatolewa kafara badala ya wanyama!
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye blue, sijakuelewa kabisa mkuu, ulikuwa unamaanisha nini? by the way, uganga wote hata kama wa kutoa kafara kuku, mbuzi etc unakubalika kwako kutokana na paragraph hii uliyoandika?...tutafanyaje kuwanusuru ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi..na ni lini tutafuta hawa waganga wa kienyeji?

  nasema hivi kwasababu you never know who is next...mwanzoni hawa jamaa hawakuanza na albino..walianza kuua watu wenye vipara, wakaja wakaanza kuchuna watu ngozi, wakaja kuanza kukata wanawake matiti, wakaja kuanza kupiga watu nondo ili ile damu ya kwenye nondo waende kutumia kwenye vyuma kwenye mabucha ya nyama,..wakaja kutoa watu sehemu za siri na kuondoka nazo...wakaja kuwa wanakata mkono wenye M, na sasa hivi wapo kwenye kuua albino..you never know who is next...pengine wataanza kukata watu wenye nywele ndefu, watu wenye pua ndefu, watu wafupi, watu warefu, watu wenye identity yeyote ile wanayotaka wao na sisi wananchi hatujui nani atafuata baada ya list hizi walizoanza na wanabadilibadili kila wakati...kitu ambacho kinafanya vita hii iwe ya kwetu sote wala si ya kundi moja...wanaoathirika ni wote jamani..

  kiini kikubwa hapa ni WAGANGA WA KIENYEJI ambao selikali inawafahamu, inawapa vibali na inawaogopa....safari za bagamoyo tanga na sumbawanga haziiishi....now, hivi kwenye uchaguzi huu hawa jamaa watakuwa na sauti ya kuwakemea waganga wa kienyeji? kama hawatakuwa na uwezo huo, basi inference ni moja kwa moja kuwa wanawategemea kuwafanyia uganga kwenye uchaguzi hivyo wanaogopa kutukana mamba kabla ya kuvuka mto...hii dhana ya uchawi itaisha lini? na kwanini tz tumefikia hata international community inatuogopa huku majuuu?
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  hapa patakuwa padogo, kwasababu kuna watu wengine hao waganga wa kienyeji..hasa wale waliojaa magomeni kina dr.tamba, sijui dr. nani kibao, wanaopunga pepo na kufukiza majini, imani za watu wengine zinaruhusu...sasa ukisema uganga ufutiwe leseni, watu wengine ndo ibada yao na hawawezi kukubali..ndo kama unavyomwona mziziMkavu alivyo, akili yake imeelekea huko..utasemaje utamtoa mwenzio kafara kama ungekuwa mganga? na kwanini unashabikia wachawi?
   
 6. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ninachojua hakuna imani yoyote kwa namna yoyote ile iwavyo inayokubali uganga. Hizi ni njia tu watu wanazozitumia kushibisha matumbo yao kwa kivuli cha imani fulani. Muumini wa kweli siku zote uganga kwake ni sumu. Tatizo linalokuja hapa waganga wengi wanapata support kutoka kwa viongozi wakubwa na pia waganga hawa mtandao wao ni mkubwa mno. Rejeeni utafiti wa Vicky Ntetema ili kuthibitisha mtandao huu!
  Ni jukumu la kila mmoja kupiga vita ushirikina huu.
   
 7. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna aina mbili kuu za watu; kuna wajinga (wasiotaka kujishughulisha na fikra) na waelewa. Na kwa bahati mbaya sana katika waelewa, wastaarabu ni wachache na wajanja ndio wengi zaidi. Hivyo, siku zote, ukweli unabakia kuwa WAJINGA NDIO WALIWAO - na wajanja. Mtu usipoweza au usipotaka kufikiri na kuchambua mambo mwenyewe basi tarajia kukutana na wajanja wa kila aina watakaokufanyia kazi hiyo jinsi waijuavyo wao!
   
Loading...