Waganga wa jadi wamtishia Waziri Mkuu Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waganga wa jadi wamtishia Waziri Mkuu Pinda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Balantanda, Feb 3, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hadija Jumanne na Zacharia Osanga

  BARAZA la Waganga na Watafiti wa Tiba Asilia nchini, wamempa miezi miwili Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kufuta amri yake ya kufungia leseni zao na vinginevyo watampeleka mahakamani.


  Mwenyekiti wa baraza hilo, Shaka Mohamed Shemuiwa kuwa alisema wanataraji kumfikisha mahakamani, Waziri Mkuu endapo hatofuta kauli yake hiyo, iliyotokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) kwa muda wa miezi miwili.


  “Hatukubaliani na agizo la Waziri Mkuu la kufuta leseni za waganga wa jadi na kuwazuia kufanya shughuli zao, kwa sababu ya baadhi ya watu wanaojifanya waganga wanaohusika na mauaji ya albino na vikongwe,” alisema Shemuiwa na kuongeza:


  “Kwa asilimia kubwa, vitendo hivyo vya kikatili na kinyang’au vinasababishwa na maafisa wa halmashauri za wilaya na manispaa wanaohusika na kutoa leseni kwa waganga wa jadi na wamekuwa wakitoa leseni kwa watu wasio na utaalamu huo wa tiba asili,” alibainisha Shemuiwa.


  Shemuiwa alisema kwamba, sharti walilopewa la kutokutibu hadi dawa zitakapo thibitishwa na Kitengo cha Tiba Asili cha Hospitali Muhimbili chini ya uhakiki wa mkemia mkuu wa serikali kinalenga kuwakandamiza na kuwaumiza waganga wa jadi, kwani ni vigumu kutekelezeka.


  “Sharti hilo ni gumu na linalenga kuididimiza kazi yetu, hata hivyo sisi kama baraza tumeshazungumza na waziri wa afya juu ya agizo la waziri mkuu na amesema alisiki kwenye vyombo vya habari juu ya marufuku hiyo,” alinena mwenyekiti huyo.


  “Baraza la waganga watafiti wa Tiba Asili linaamini kama maafisa hao wangekuwa na utaratibu wa kushirikisha vyama vya waganga wa jadi katika kuwatambua waombaji wa leseni hizo, matapeli wasingeweza kujiingiza katika fani hiyo na kutuharibia,” alisema Katibu Mwenezi wa baraza hilo.


  “Tunalaani mauaji ya albino nchini na wote wanaohusika na vitendo hivyo wasakwe na kufikishwa mbele ya vyombo husika, ili sheria ichukuwe mkondo wake,” alisema mwenyekiti huyo.


  Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo, wanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini walisema akiuawa albino atauawa watawachukulia hatua za kisheria viongozi wa baraza hilo.


  Hatua hiyo inafuatia kauli uongozi wa baraza kutoa miezi mitatu kwa Waziri Mkuu, ya kumtaka abatilishe tamko lake la kusimamisha huduma za waganga wa jadi vinginevyo watampeleka mahakamani.


  Wanaharakati hao walisema wapo mbioni kuandaa siku ya maombolezo kitaifa kwa ajili ya kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha tangu janga la kuuawa kwao lilipoanza.


  Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wanaharakati hao walionyeshwa kushangazwa kwa na kitendo cha Kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atoe ufafanuzi kuhusu kauli yake aliyoitoa akiwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwamba, wanaoua albino nao wauawe, huku yeye mwenyewe akizunguka karibu dunia nzima kutangaza mauaji ya Wapemba 23 mwaka 2001.


  ‘‘Tunamuuliza Hamad Rashid kwamba, kama mauaji ya Wapemba 23 yalimzungusha dunia nzima kuyatangaza na kutoa tamko kali, kwa nini asione uchungu kwa mauaji ya ndugu zetu albino ambao wamefikia zaidi ya 43?’’ alihoji Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chini ya Jua moja nchini (UTSS), Josephat Turner.


  ‘‘Tunamhakikishia Waziri Mkuu kuwa machozi yake hayatapotea bure vilevile yametupa ujasiri mpya wa kuanzisha mkakati makini wa kupambana na tatizo hili,’’ alisema.


  Turner alisema walitarajia kuwa kiongozi huyo ambaye ameonyesha uchungu wa kweli angeungwa mkono na kutiwa moyo, lakini badala yake wanasiasa wameona ndiyo nafasi nzuri ya kumshambulia na kumshutumu.


  Aliongeza kuwa kauli kama hizo za baadhi ya wanasiasa zinaonesha hakuna nia ya kweli ya kumaliza ukatili huo, kwani hata Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurent Masha aliwahi kusema kuwa tatizo hilo ni dogo bali linakuzwa na waandishi wa habari.


  ‘‘Hatujui ili mauaji haya yawe makubwa anataka watu wangapi wauawe!’’ alishangaa.


  Pinda ilitangaza kufuta leseni zote za waganga wa jadi kuanzia Januari 23 mwaka huu likiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino na vikongwe nchini.


  Pinda atangaza amri hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Shinyanga, mwishoni mwa ziara yake ya mikoa ya mika ya Kanda ya Ziwa kuhamasisha mapambano ya serikali dhidi ya mauaji hayo.


  Waziri Mkuu alisema aliwasiliana na Mwanasheria Mkuu kuhusu uamuzi wa kuchukua hatua hiyo ya kufuta leseni hizo na kwamba alisema jambo hilo linawezekana.


  Katika mikutano na viongozi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Tabora na Shinyanga, wachangiaji wengi waliitaka serikali ifute leseni hizo. Hata baadhi ya waganga wa jadi waliochangia walikubalina na pendekezo hilo.


  Waganga wa jadi husajiliwa na kupewa leseni za kufanya kazi zao na Halmashari kwa utaratibu wa kiutawala. Ipo sheria ya mwaka 2002 kuhusu Tiba Asilia na Tiba Mbadala (Traditional and Alterntive Medicine Act), lakini kanuni za utekelezaji wake zilikuwa hazijatengenezwa.


  Waziri Mkuu alisema mganga wa jadi ambaye anaweza kuruhusiwa baadaye ni yule ambaye dawa zake za mitishamba au za asili zitakuwa zimethibitishwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Tiba Asili cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa kweli zinatibu na kwamba, mgonjwa atatakiwa awe na cheti kutoka hospitali kitakachothitisha maradhi yake na kuwa tiba yake hopitali imeshindikana.


  "Waganga hawa ni waongo wakubwa, siyo lazima kuwa nao. Wangekuwa waganga wa kweli magonjwa mengi yangepungua nchini, lakini magonjwa yapo na sasa wanapiga ramli na kuwa kichocheo cha mauaji.


  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Pinda asitake kuleta habari za mtego wa panya unaowakumba waliokusudiwaq na wasiokusudiwa.

  Kama ana sababu ya kutaka kufuta leseni aiseme, na kanuni zifuatwe, Waziri Mkuu si Sultan wa kusema jambo aliloota na kila mtu amsujudie.

  Wengine kipande hiki cha Mbwamaji mpaka Kilwa hospitali tunaisikia kwenye bomba tu, na hawa wazee wa mitishamba ndio angalau wanatupa matumaini, halafu yeye anataka kuwafungia hata hao nao?
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa si wanajidai kuwa ni wataalamu wa miti shamba, kwanini wasitumie mahaka yao mpaka waende kwenye hizi mahakama za kiserikali! wao ni maDr na MaProf. halafu wanashindwa kutumia huo utaalamu wao kumgeuza Pinda? au hawakutaka kuweka bayana?
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nono, Mkuu hapa umenichekesha sana na hakika una point kubwa sana!..
  Wao wajuzi na hapa ndio sehemu inayotakiwa hasa kuutumia ujuzi wao wanashindwa nini hadi kwenda mahakamani..
  Besides, hakuna mtu anayetaka kununua dawa feki, kama kweli wanatibu kwa nini wasikubali zifanyiwe majaribio au Uganga wenyewe ni wa kuondoa watu roho tu!..
   
 5. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni ajira na huduma kwa wananchi, huwezi kufuta lesenie bila kufanya uchunguzi.
  Sio wote wanaua maalbino!
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  M sorry but sometime Mkandara mkuu, there is no other alternative, so people are ready to take the risk ya kula miti shamba. About 80% of people in rural areas depend on this alternative medicine for treatment. Pia kumbuka dawa hizi za kithungu tunazoabudu zinatokana na miti shamba na hata synthetic drugs zimekuwa patented after miti shamba. Tatizo ni kuwa we want to throw out the baby with the bath water! Sasa kusema tu kwamba waganga ndo wanawaua maalbino is wrong. Hao wanaoua maalbino nina uhakika si wale wenye leseni halali! M ready to bet on that!
   
 7. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawana la kufanya nadhani ujanja wa bure sasa wamtishie ili iweje nadhani wamefanya jambo la busara sana kufungia hivyo vibali vyao ndio vizuri sana......
   
Loading...