Waganga wa jadi marufuku kutangaza kuongeza nguvu za kiume

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
196,133
2,000
Wednesday, 01 December 2010 | Na Hamad Amour (TSJ) na Kalonga Kasati

SERIKALI imewataka waganga wa jadi kuondoa mabango ya matangazo katika maeneo mbalimbali nchini, yanayohusu kuongeza nguvu za kiume na mvuto wa kimapenzi.

Tamko hilo, lilitolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Chiku Galawa katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro na kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijni Dar es Salaam jana.

Galawa alisema waganga hao, wanapaswa kuondoa mabango hayo kwa kuwa yanachochea watu kufanya mapenzi na wakati mwengine kufanya ngono ambazo si salama na kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Alisema waganga wanaotaka kuweka mabango hayo, wanapaswa kulipia kodi na kupata kibali kutoka serikalini.

Galawa alisema tafiti zinaonyesha Mkoa wa Dar es salaam, umeshika nafasi ya pili kwa maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 9.3 na wanawake wameathirika kwa zaidi ya asilimia 10.2 ukilinganisha na wanaume ambao wameathirika kwa asilimia 7.3, zaidi ya wanaoishi vijijini.

"Kuanzia leo, ninatoa tamko la kuondolewa kwa mabango ya matangazo ya waganga wa kienyeji kwani yamekuwa chanzo kikubwa cha kuchochea maambukizi ya ukimwi,"alisema Galawa.

Alisema kuongeka kwa kumbi za starehe imetajwa kuwa chanzo cha kuongeza kwa kasi ya maambukizi ya UKIMWI.

Katika hatua nyingine, alisema huduma kwa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU), zitaendelea kutolewa kama kawaida na kwa ufanisi zaidi, kama vile kutoa dawa za kurefusha maisha kwa wathirika.

Wakati huohuo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Hawa Kawawa aliwataka watu wajitokeze kwa wingi kupima afya zao.

"Kwa sasa tuna jumla ya vituo 122, vikiwemo 68 vya serikali na 54 vya watu binafsi. Mashirika na asasi zisizo za kiserikali ambavyo vinatoa huduma za kupima VVU,"alisema Kawawa.

Aliitaka jamii kubadili tabia na kuwa waaminifu ili kuepuka kuambukizwa VVU. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Huduma za ukimwi na haki za binadamu kwa wote.'
 

seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
0
Serikali ipunguze umaskini kwa Watanzania, maana kasi yote hii ya matangazo ni kutafuta fedha za kumudu maisha, watu wanaishi kwa ujanja wa kila aina....viagra haitoshi?
 

Bongemzito

Senior Member
Nov 5, 2010
162
0
Hapo pointi ni kulipa kodi kwa serikali sio kupiga marufuku kwa kuwa wanaongeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.....wale wakilipa kodi wataruhusiwa waendeleza business zao kwani biashara hiyo sio haramu bado kwa iyo kuilipia kodi ni ruksa..
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,562
2,000
Mimi ninayo Dawa ya kuongeza Nguvu za kiume hata kama mtu amekuwa hafai hiyo dawa yangu inaweza kumsaidia ina nguvu sana hiyo dawa anayetaka ani ( PM) tafadhali.
 

MAKAH

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,589
0
hahaaaaa!!! majuzi mbeya mganga mmoja anayetamba kwa matangazo katika fms alipata kipigo cha mbwa toka kwa vijana fulani. kumbe vijana hao walinunua dawa ya kuongeza chaji kuwa marudufu toka kwa mganga huyo. walipo kwenda uwanjani haikuwa lolote wala chochote. ndipo walipomrudia mganga wao na kumpa kisago wakimlaani kuwa ni tapeli. CHUNGA MAMBO HAYA. kwa nin usitumie INJOY ya shellys ya hapa nyumbani na ambayo ina viwango.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom