Waganda wateka ajira za ualimu kwenye mashule binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waganda wateka ajira za ualimu kwenye mashule binafsi

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Alexism, Sep 18, 2011.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Wakati wa harakati za kuingia kwenye EAC hasa Common Market tayari waganda wameteka soko la ualimu mkoani Kagera hasa wiliya za Karagwe,Bukoba mjini na vijijini hasa kwenye private English medium na secondary school.Kitu gani kimechangia kuwa hivi
  1.Imani ya watu wengi kuwa waganda wana akili kuliko Watanganyika na Wazanzibari
  2.Waganda wanajua Kiingereza kuliko Watanganyika na Wazanzibari
  3.Waganda wanafanya kazi kwa umaki kuliko wazawa
  4.Mshahara wao siyo mikubwa kwani pesa yetu inathamani kuliko ya Uganda
  Mfano wa shule hizo ni KEMEBOS,BUHEMBE ENGLISH MEDIUM,AMANI PR. AND SEC. SCHOOL,RWEIKIZA ENG.MEDIUM (MB-BK VJ)KAJUMURO GIRLS(MB-MULEBA-ANA TIBA)TWEYAMBE nk.
  Je kuna sababu za msingi kuwatumia hao watu wakati wabongo wapo?
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  wabongo kweli wapo mkuu tatizo kuiwasilisha ngeli ipasvyo ni iiishu
   
 3. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 80
  Waganda ni wanyenyekevu sana, unaweza hata kumpiga vibao na akaendelea kuwepo kazini tofauti na wabongo. Pia mishahara wanalipwa ni kidogo na wanaridhika.
   
 4. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 80
  <br />
  <br />
  Ngeli ya Waganda ya hovyo sana..wanaitamka kigandaganda tu..mfano..goodu morningi madamu..mie nna katoto kangu kanasomea Huwiler English Medium kanafundishwa na Waganda kanatamka maneno kiajabu ajabu.
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Sa kama wabongo hawachangamkii fursa zilizopo,wameweka usharobaro mbele,c 2wasaidiaje tena?wacha waganda wapge mzigo bana
   
 6. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mtu wangu cc waTZ tunakuwa waoga 2 kiingereza sio ishu sana kuongea hasa cc wabongo 2naweza, TATIZO KUJIAMINI!!
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Kuna watu wanasema watanzania hawajui kiingereza,well and good sikatai hilo,but I think we need to ask ourself what is the source of this situation? Kama hao watanzani ambao hawajui kiingereza wamesoma shule zinazomilikiwa na serikali kwa niaba ya umma nani wakulaumiwa? Serikali ya CCM haitakwepa lawama hizi hata siku moja...ni kweli tunatakiwa kuwa na juhudi binafsi,lakini kama hakuna conducive environments to support our efforts I dont think if we would be able to move one step ahead....Tazama hizi English Medium school,watoto wanapewa mazingira mazuri ambayo yanawasaidia kuelewa kiingereza,walimu wapo,vitabu vipo,madawati yapo,madarasa masafi nk...shule za umma ni maumivu makubwa sana kwa wananchi jamani....na kumbuka huyu mtoto anayesoma kwenye mazingira magumu(kwenye shule za serikali) ndio anaandaliwa kuwa mwalimu wa baadae unategemea nini? Basically;hawa watoto wanaosoma shule za wakubwa hawawezi kuja kuwa walimu maana katika nchi hii ualimu ni fileld of failures............mtu aliyefeli ndio anaambiwa jaribu ualimu(JAPO SI WOTE)...Kwa ujumla wake wananchi tunapenda sana kufanikiwa tatizo ni serikali yetu,haitoi mazingira mazuri ya sisi kufanikiwa...............
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kabilianeni na ushindani...msiukimbie... nyakati za kulishwa ka watoto wa njiwa zimekwisha..
   
 9. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Hapa nadhani kabla ya kujiuliza kwa nini Waganda na hata Wakenya wanakubalika kufundisha hapa kwetu badala ya Watanzania.

  Mfumo wetu wa elimu ukoje je viwango vya elimu yetu vikoje leo asubuhi nimesikia kuna baadhi ya wanafunzi wamechaguliwa kujiunga na sekondari za umma lakini hawajui hata kuandika!.

  Nadhani kutoa walimu nchi jirani ni zaidi yakuzungumza kingereza vizuri hata ukiangalia kwenye mtandao nchi za Kenya Tanzania Rwanda Burundi Somalia Sudan DRC nk zinachangia vizuri pato la Uganda kwa wanafunzi wanaosoma huko kuanzia shule za msingi sekondari na vyuo vya elimu ya juu.

  Tumeshawai kujiuliza kwa nini Mtanzania akienda kufanya kazi nchi jirani kitu cha kwanza anafanya uhamisho wa watoto wake kwenda kusoma anakoelekea lakini wao wanapokuja Tanzania hawaji na watoto wao kusoma huku au inakuwaje watoto wanaoishi mipakani mwa Kenya Uganda Zambia Malawi nk wanaamua kwenda kuhudhuria masomo katika nchi za jirani na kurudi jioni Tanzania lakini wao hawaji kusoma kwetu.

  Nikirudi kwenye suala la walimu kutoja nje kuajiliwa Tanzania je ni walimu wangapi toka hapa wanafundisha katika nchi jirani hata kama sio kufundisha kiingereza walau kiswahili.

  Mimi sidhani kuwa hoja nikutojua kiingereza hapa kinafundishwa toka shule ya msingi ukiongeza na miaka ya sekondari utakuta ni takriban miaka kumi unajifunza kiingereza kama hiyo lugha inafundishwa vizuri utakuwa umeshaijua Nakumbuka vijana wetu wanaopelekwa Ulaya Mashariki wanapewa miaka miwili kujifunza lugha na baadae ndio uanza masomo ya shahada au stashahada na wanafanya vizuri je hapa tunashindwa nini?.

  Rafiki yangu toka Uganda alinidokeza kuwa wao walipotaifisha shule za madhehebu ya dini serikali iliyaachia uendeshaji wa kila siku madhehebu husika lakini wakawa wafuata mwongozo na mitaala ya serikali ikiwa ni pamoja nakupokea wanafunzi kufuatana naufaulu na si vinginevyo.

  Huyo jamaa anasema shule hizo zilizotaifishwa pamoja na vyuo vya ualimu bado zinaendelea kutoa elimu bora na ni kati ya shule zinazoongoza kwa kutoa matokeo mazuri kitaifa.

  Tanzania hatujachelewa endapo serikali itaidhamini elimu na kuipa kipaumbele sio kuleta mikakati ya zimamoto tunaweza. Kuna kipindi walikuwa wanawapeleka vijana waliomaliza kidato cha sita kozi ya miezi miwili halafu wanapangwa kufundisha sekondari. Mataifa yote yanayoendelea kwa kasi yanawekeza kwelikweli kwenye elimu.Kazi kwetu ELIMU KWANZA so goes the slogan.
   
 10. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ngeli si issue kihivyo. Nadhani sisi WaTZ njaa bado haijatuuma inavyotakiwa.
   
 11. O

  Optimistic Soul JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nakubaliana nawe mkuu, wabongo tunachagua sana kazi, bado njaa hazijatuuma, naona hata supermarkets siku hizi waganda na wakenya kibao, njaa ikiuma vizuri hata spanish utapiga ivoivo kimagumashi ili utoke sio tu kingereza.
   
 12. amu

  amu JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  who is eating you?DaaENGLISH ya ug majanga sana
   
 13. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2013
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani hebu tuwe makini ktk hoja. Hivi Tanzania ni walimu wangapi walio tayari kufanya kazi ktk shule binafsi. Tanzania hatuna tatizo la ajira ya ualimu tofauti na nchi nyingine. Pia mishahara ya ualimu ktk nchi hizo nyingine ni mibaya ukilinganisha na Tanzania. Kwa mfano ukiuona mshahara wa mwalimu wa Rwanda hutaamini! Sidhani kama ni sahihi kusema wameteka soko la ualimu wakati wazawa hawapo tayari!
   
 14. Posho City

  Posho City JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2013
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 639
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Shule kama Tusiime wapo kibao na kwa ujumla matamshi yao majanga.
  Sema hawa jamaa hasa waganda ni cheap sana na yes men ili waendelee kuchuma pesa maana Uganda mishahara ya ualimu majanga.
  Hata mikataba ya kazi hawana.
   
Loading...