Wafungwa Waislamu Uingereza Watenganishwa na Wasio Waislamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafungwa Waislamu Uingereza Watenganishwa na Wasio Waislamu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Jela ya Winson Green iliyopo katika mji wa Birmingham. Sunday, June 21, 2009 7:58 AM
  Wafungwa wa kiislamu katika jela moja nchini Uingereza wamepewa vyumba wakae na waislamu wenzao au wamepewa vyumba vyao pekee yao baada ya malalamiko yao ya kutofurahishwa kukaa chumba kimoja na wafungwa wasiokuwa waislamu kukubaliwa. Wafungwa hao walisema kwamba hawajisikii vizuri kusali na kula mbele ya wafungwa ambao si waislamu katika jela ya Winson Green iliyopo katika mji wa Birmingham.

  Hii ni mara ya kwanza nchini Uingereza wafungwa kutenganishwa kutokana na dini zao.

  Taarifa ya jela hiyo ilisema kwamba wafungwa wa kiislamu katika jela hiyo watawekwa chumba kimoja na waislamu wenzao au watapewa vyumba vya pekee yao kama nafasi itakuwepo.

  Jela hiyo ina wafungwa 1,400 wakiwemo wale waliofungwa kwa makosa ya mauaji na wale waliofungwa kwa makosa ya ujambazi.

  "Hadi sasa wafungwa 15 wa kiislamu aidha wamewekwa chumba kimoja na mwislamu mwenzao au wamepewa chumba chao pekee yao" kilisema chanzo cha jela hiyo.

  Awali inasemekana wafungwa hao walitaka watengewe sehemu yao maalumu katika jela hiyo lakini ombi lao lilikataliwa.

  Waislamu wapatao 200 katika jela hiyo walilalamikia kupikiwa nyama zisizochinjwa kiislamu ambazo zilikuwa zikiandaliwa katika jela hiyo na kuifanya jela hiyo ianze kununua nyama zilizochinjwa kiislamu kutoka nje.

  Afisa mmoja wa jela hiyo alidai kwamba hali hiyo imesababisha hali ya kuonekana kama vile wafungwa wa kiislamu wanapendelewa kwa kupewa huduma maalumu.

  Hata hivyo msemaji wa jela hiyo alijibu madai hayo kwa kusema kwamba maombi ya wafungwa kushea vyumba vya jela yanaangaliwa kwa kutumia vigezo vya kuwa dini moja au kutumia chakula cha aina moja, pia kabla ya uamuzi kutolewa uchunguzi wa madhara yanayoweza kutokea hujadiliwa.

  Katika wafungwa 80,000 waliopo katika jela za Uingereza na Wales asilimia 10 ya wafungwa hao ni waislamu.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2298178&&Cat=2
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wangekuwa washika dini kweli wasingekuwapo jela in the first place..
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijakuelewa kwanini umeweka hii thread, sioni jambo la ajabu hapa. Wafungwa wamekuwa treated vizuri kulingana na madai yao. Tuseme umeileta hii habari kwa sababu ya uzuri wake au ubaya wake? Eleweka pls!
   
Loading...