28 July 2022
Ukerewe, Mwanza
MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA KTK KESI No. 171 OF 2021, YAWAACHIA HURU WANACHAMA WA CHADEMA
Waliokuwa wagombea udiwani kupitia chama cha CHADEMA washinda rufaa yao na kuachiwa huru. Mzizi wa Hii kesi ilitokea wakati wa kurudisha fomu za udiwani, walipigwa risasi mwilini na walibabikiwa kesi.
Makamanda hao ni Mateso Mgeta na Alfred Mabagala ambao mbali ya kushinda kesi hiyo walikuwa tayari wametumikia miaka 2 katika ya mitano kabla ya kushinda rufaa yao.
Makamanda hao wa CHADEMA sasa wataenda kukaguliwa afya zao kwani walipata majeraha na vipigo vilivyopelekea kutembelea magongo na walipokuwa jela, mazingira yale yalikuwa magumu kuweza kupata huduma kamilifu za kutibu majeraha yao.
CHADEMA kanda ya Victoria na taifa inaomba wana CHADEMA na waTanzania kwa ujumla kuwaangalia hawa makamanda ili waweze kupata huduma za kiafya baada ya kutoka gerezani na sasa wapo huru.
Jaji wa mahakama kuu kanda ya Mwanza katika uamuzi wake ulio andikwa katika jumla ya kurasa 17 Alfred Mabagala @ Mugeta & Another vs Republic (Criminal Appeal 171 of 2021) [2022] TZHC 10789 (25 July 2022); | Tanzlii na kusomwa mbele ya Mahakama Kuu, alikubaliana na hoja za upande wa utetezi kupiga hukumu ya mahakama ya wilaya ya Ukerewe.
Source : CHADEMA Media TV