Wafungwa wa kisiasa DRC kuachiwa huru

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,388
2,000
media
Rais wa DRC Félix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ameahidi kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa ndani ya siku kumi zijazo.

Akielezea mipango ya serikali yake kwa siku 100 zijazo, rais Tshisekedi amesema atahakikisha pia wanasiasa waliokimbia nchi hiyo kwa sababu za kisiasa, wanarejea nyumbani.

Kauli hii inatoa matumaini kwa mwanasiasa Moise Katumbi aliyezuiwa kurejea nchini humo mwaka 2018, na amekuwa akiishi nchini Ubelgiji.

Wiki hii msemaji wa Katumbi, alisema mwanasiasa huyo ameanza mchakato wa kuanza kupata pasi yake ya kusafiriia ili arejee nyumbani.

Ameeleza kuwa, anafanya hivyo ili kufanikisha mchakato wa demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Mbali na hayo, rais Tshisekedi amesema serikali yake itahakikisha kuwa haki na ukweli zinawekwa katika nafasi ya kwanza.

Aidha, amesisitiza kuwa watu watakaopewa kazi ya kutafuta haki, watakuwa ni watu waandilifu ambao pia watakuwa na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom