Wafungwa kuwa na simu za kiganjani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafungwa kuwa na simu za kiganjani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eeka Mangi, Dec 3, 2008.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pamoja na na utetezi wake wa jinsi Mramba na Yona walivyoletwa mahakamani jumatatu bila removal order, Mkuu wa magereza nchini Ndugu Nanyaro (kama sijakosea jina leke) alikiri kuwa ni kweli wafungwa katika gereza moja hapa nchini waliongea kwa njia ya simu na chombo kimoja cha habari na kutoa taarifa mbalimbali zinazowahusu. Katika mahojiano hayo na radio ya Taifa jana usiku, nanyaro anakiri kuwa hajui ni nani aliyewapa simu watu hao. Je katika hali hii, si ni kweli kuwa usalama katika kitengo cha Magereza nchini ni kitu ambacho hakipo. Tutaamini vipi kuwa hawajui wakati hawa jamaa wako mikononi mwao. Tena hakuongea mfungwa mmoja, ni kama 3 au 4 hivi. Kwa nini Nanyaro na team yake wasiwajibishwe kwa uzembe huu?
  Nawasilisha
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Eeka ukianza kuangalia suala zima la jinsi Yona na Mramba walivyotendewa keko utaona kuwa kuna watu wengi tu wanaopaswa kuwajibishwa. Lakini nina uhakika wa asilimia nyingi tu kuwa hakuna atakayewajibishwa, hata huyu aliyekiri hadharani kwamba kulikuwa na simu hatawajibishwa.
   
 3. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Above all VIP siku zote atakuwa VIP, ktk maisha yangu nilitokea mtu mmoja mkubwa ninayemfahamu alikamatwa na kupelekwa hapo keko, na bahati nzuri au mbaya alikuwa analala chumba kimoja na Bwana Zombe. ki ukweli ktk chumba chao tofauti iliyokuwepo ni vile tu kuwa wamefungiwa ndani bila kutoka nje, lakini karibu huduma muhimu zote wanazo ndio maana hata tulipokuwa tunaenda kuwaona watu tulikuwa tunaingia hadi vytumbani kwao na kupiga stori japo simu walijitahidi zisitumike lakini watu tuliingia nazo binafsi mmoja wapo na wafungwa hao wanatumia kama kawaida tu, wanapata huduma zote kama wapo uraini.

  kama kweli magerza wanataka kuthibiti vitu wanavyosema hawaitaki, basi waheshimu sheria zao kwamba wafungwa waonwe sehemu zilizotengwa kwa ajili ya kuonwa na sio VIP waruhusiwe kuonwa hadi wanakolala, na vile vile waweke vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukagua watu wanaokwenda kuwaona ndugu zao na sio kukagua kwa macho tu unachungulia kisha unamruhusu mtu apite.
   
 4. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2008
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  V.I.P ni Very Important Prisoner katika hili. Swala ni how important are Mramba and Yona rated... ! Rated as a threat to the country economic security au important for thier power abuse...? Kuna professional ethics hazikufatiliwa ndio kuambiwa wametumia vibaya madaraka yao.

  Hawa V.I.P wana mali ambazo hawawezi kuzi account for: Yona bila aibu kaleta hati zenye kuwa na mali inayozidi Shs 3bil... wakati vijijini hakuna shule. Mjanja mchagga kadhaminiwa waliofaidika na exemption zake NAFIKIRI NDIO MATOKEO YA SIMU ZA MKONONI HUKO KEKO
   
  Last edited by a moderator: Dec 3, 2008
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ipo Haja ya kuwachunguza hao waliowadhamini VIP hao....ukiweka dots zote utakutana na mambo ya AJABU MNO....
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sawa lakini hawa hawakuwa VIP, ni watu wanaongojea kunyongwa na wengine wanasubiri rufaa zao. Ni watu wa kawaida mno! ingekuwa ni akina Mramba na akina Zombe nisingeshangaa sana! Ila hawa ni watu wakwetu tu hawa.
   
 7. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
   
 8. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu Bongolander, kwani Yona na Mramba wamefanyiwa nini Keko zaidi ya kulala siku hizo????
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Naona kama ville unachanganya kati ya 'mahabusu' na 'wafungwa'. Mahabusu ni watuhumiwa tu na hivyo hawapotezi haki zao kama vile wafungwa. Na ndio maana mahabusu anaweza kuachiwa huru kama atatimiza masharti ya dhamana. Taratitu za kuana wafungwa ni tofauti kabisa na taratibu za kuona mahabusu.

  Hata hivyo hili la wafungwa (waliohukumiwa kunyongwa) kuwa na simu gerezani nadhani Bwana Nanyaro inabidi atueleze vizuri. Nahisi pia linaweza kumweka pabaya bwana Adalla Majura (wa BBC) if he was not carefully in covering his back!
   
 10. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
   
 11. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo hili la wafungwa (waliohukumiwa kunyongwa) kuwa na simu gerezani nadhani Bwana Nanyaro inabidi atueleze vizuri. Nahisi pia linaweza kumweka pabaya bwana Adalla Majura (wa BBC) if he was not carefully in covering his back![/QUOTE]

  Abdallah Majura anakosa gani hapa? yeye kapigiwa simu kapokea na kufanya kazi yake ya uandishi wa habari - katoa taarifa. Wenye kosa ni maaskari na bwana jela kwa kuachia mianya kwa wafungwa kuwa na simu nk
   
 12. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Abdallah Majura anakosa gani hapa? yeye kapigiwa simu kapokea na kufanya kazi yake ya uandishi wa habari - katoa taarifa. Wenye kosa ni maaskari na bwana jela kwa kuachia mianya kwa wafungwa kuwa na simu nk[/QUOTE]

  Ingawa mimi sio mwanasheria lakini nafahamu ni makosa kumsadia mtu kuvunja sheria. Sina hakika kama ni kweli wafungwa ndio walimpigia simu au yeye pia alihusika katika kumfanikisha mpango huo. Kwa interview ya mfungwa wa kwanza anaweza kujitetea, lakini hata baada ya kugundua kwamba anaaongea na mfungwa isivyo halali bado aliendelea kuwainterview wafungwa kadhaa baada ya hapo (Hi ni kama vile mtu anaeua kwa kisu - kama alichoma mara moja anweza kujitetea kwamba hakukusudia, lakini kama alimchoma marehemu mara kadhaa huwa ni vigumu kutoa utetezi kama huo). That's why I am saying he may be incriminated if he was not carefully in covering his ass!"
   
 13. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ingawa mimi sio mwanasheria lakini nafahamu ni makosa kumsadia mtu kuvunja sheria. Sina hakika kama ni kweli wafungwa ndio walimpigia simu au yeye pia alihusika katika kumfanikisha mpango huo. Kwa interview ya mfungwa wa kwanza anaweza kujitetea, lakini hata baada ya kugundua kwamba anaaongea na mfungwa isivyo halali bado aliendelea kuwainterview wafungwa kadhaa baada ya hapo (Hi ni kama vile mtu anaeua kwa kisu - kama alichoma mara moja anweza kujitetea kwamba hakukusudia, lakini kama alimchoma marehemu mara kadhaa huwa ni vigumu kutoa utetezi kama huo). That's why I am saying he may be incriminated if he was not carefully in covering his ass!"[/QUOTE]

  Nakubaliana na hili la kumsaidia mtu kuvunja sheria, lakini hapa laziam tuelewe kuwa mwandishi hapo alitaka kutuma ujumbe kuwa hata hawa ambao wako kifungoni bado wanaweza kuwa na easy access watu walioko uraiani. Issue walipataje simu kama sio maafisa magereza walizipeleka?
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nyie wanaJF hapa hawa watu wa magereza wasitake kutudanganya. Maana magereza zetu zimejaa ubaguzi sana na hili si geni hata huyu mkuu wa magereza analijua kabisa. Watu waliowahi kuwa viongozi hapa wanakuwa treated kama bado ni viongozi wa nchi wakati ni waharifu. Mbona hajauliza waliwezaje kuwatoa Keko na kuwapeleka mahakamani bia removal order. Leo anataka kutuambia ujinga gani huu?
  Na ubaguzi huo unaweza kuuona katika issue hii ya wakina Mramba. Angalia hata waziri wa mambo ya ndani anavunja sheria kwa kwenda kuwaona wahalifu hawa na hakuna aliyelalamika. Wao wanaona kwamba kwa kuwa ni waziri tena wa mambo ya ndani anaweza kwenda tu kumtembelea criminal kama wakina Yona kwa kuwa wote walikuwa wakiiba pamoja? Kwani tunaweza kuambiwa Masha alikwenda Keko kama nani? Kama Masha au kama waziri wa mambo ya ndani? Je alikuwa anakwenda kuwapelekea magodoro au mashuka au nets? Alikuwa anakwenda kuwabembeleza wasimkasirikie yeye au JK?
  Sasa huu ujinga anaowaambia watanzania kwamba atawachukulia hatua waliohusika plus vyombo vya habari si ni ujinga tu. Ameumbuka huyu.
  Wacha nao wapate angalau kafursa kama wakina Mramba.
   
 15. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,181
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Bongo nani ana muda wa kufanya uchuguzi? Na pia nani atamchunguza nani?
  Hakuna wa kumfunga paka kengele maana hata wengi wa hao wachunguzi mali walizonazo zina maswali kibao!
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tanzani ni zaidi ya uijuavyo usanii kila kona huu ni wizi mtupu....
   
 17. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa Nanyaro anasema kuwa rufaa ya Mramba na Yona haikumalizika siku ile ya tarehe 28/11/08 hivyo ilibidi waletwe Mahakama Kuu kumalizia rufaa yao siku ya Jumatatu tarehe 1/12/08. Akaongezea kuwa kwa kuwa akina Mramba walimaliza shughuli zao pale Mahakama kuu basi ilibidi wapelekwe pale Kisutu watafutiwe mahali salama wakae wakisubiri watuhumiwa wengine wamalize kesi zao pale Kisutu ndo warudishwe Keko na hawakwenda kisutu kwa ajili ya dhamana. Hii ni kwa mujibu wa bwana Nanyaro. lakini kwa ufahamu wangu mimi, mtuhumiwa amalizapo shughuli zake na Hakimu/Jaji, na akatakiwa kurudi mahabusu, basi hurudishwa mahabusu ndogo pale mahakamani kusubiri gari (karandinga, siku hizi kuna marco polo) la kuwarudisha keko, ukonga segerea etc Hayo yote alitaka kujitetea tu. Issue atuambie watu walipataje simu huko gerezani na niwafungwa sio mahabusu. Ama wanawapeleka mjini kufanya shopping halafu wanawarudisha tena huko gerezani?
   
 18. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Siku hizi ni tofauti sana na enzi za Mwalimu kwani wafanyakazi woooote wa serikali ni WEZI WATUPU, ndio maana utaratibu haufuatwi na hakuna cha maana kinachofanytika zaidi ya kurudi nyuma tulikotoka.

  WIZI MTUPU.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..huu "ubaguzi" sidhani kama umeanza baada ya Mramba na Yona kupelekwa Keko.

  ..kuna jamaa waliiba BOT wakati wa utawala wa Mwalimu. walipokuwa jela hawakuchanganywa na wafungwa wa uhalifu mdogo-mdogo.

  ..hata wale jamaa waliofungwa kwa kesi ya uhaini inasemekana walitengwa ktk eneo maalum.

  NB:

  ..tatizo letu wa-Tanzania huu "usawa" miongoni mwa wafungwa/wahabusu tunaupigania wakati huu wa kesi ya Mramba na Yona tu. suala hili likiisha kila mtu kimyaaa!! mapambano ya namna hii hayapaswi kuangalia sura na wasifu wa watuhumiwa.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Dec 3, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Ebana Joka vipi babu? Sasa mkuu vipi "ze dataz" za Salim?
   
Loading...