Chibudee
JF-Expert Member
- Dec 28, 2016
- 1,775
- 2,397
Wanaume wawili nchini Uganda Joseph Kintu na Sulaiman Balinya wameifungulia kesi Taasisi moja inayohusika na masuala ya afya wakidai ilisambaza condom feki ambazo zilipasuka wakati wakifanya tendo la ndoa na kusababisha Joseph apate HIV, na Balinya Gonorrhea.
Kintu amesema alinunua Condom hizo Oct 01,2019 na moja ikapasuka akiwa katikati ya tendo, alipopimwa Nov 06, 2019 akakutwa na HIV "June na September nilipima nikawa mzima, nimemuambukiza Mke wangu na amepatwa na uchizi wa ghafla”
Balinya anadai alizitumia Oct 22, 2019 akahisi maumivu alipoenda kupima Oct 24, 2019 akakutwa na maambukizi ya Gonorrhea.
Wanadai kilichowafanya wafungue mashitaka ni baada ya kuona Waziri wa Afya akitoa report Bungeni November 11, 2019 kuwa Mamlaka ya Dawa Uganda (NDA) imegundua condom hizo zilisambazwa kimakosa zikiwa hazina kiwango.
Sent using Jamii Forums mobile app