Wafukua Maiti na Kuzitupa Ili Wauze Tena Makaburi Yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafukua Maiti na Kuzitupa Ili Wauze Tena Makaburi Yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mashimo hayo yaliyofunikwa kwa mujibu wa Polisi ni miongoni mwa sehemu ambazo wafanyakazi wa makaburi hayo waliokamatwa walikuwa wakizitupa maiti kutoka kwenye makaburi waliyoyafukua Friday, July 10, 2009 4:56 AM Watu watano wanashikiliwa na polisi nchini Marekani kwa kufukua jumla ya makaburi 100 na kuzitupa maiti zilizomo na kisha kuwauzia watu wengine makaburi hayo. Wafanyakazi watano wa makaburi ya historia ya Burr Oak Cemetery yaliyopo Alsip, Chicago nchini Marekani wametupwa rumande baada ya polisi kugundua kwamba wafanyakazi hao walifukua makaburi mengi sana na kuzitupa maiti zilizokuwemo na kisha kuyauza tena makaburi hayo kwa watu wengine, alisema mkuu wa polisi wa eneo hilo, Tom Dart. Wapelelezi waligundua lundo la mifupa ya binadamu ambayo inahisiwa inatokana na maiti zaidi ya 100 zikiwa zimetelekezwa juu ya ardhi kwenye kwenye kichaka karibu na uzio wa makaburi hayo. Watu hao waliokamatwa inasemekana walikuwa wakifukua makaburi na kuyauza tena kwa takribani miaka minne kabla hawajakamatwa juzi. Inasemekana kwamba wafanyakazi hao walijiingizia kiasi cha dola laki tatu kutokana na biashara hiyo ya kuuza makaburi katika miaka hiyo minne. Habari za makaburi kufukuliwa na kuuzwa tena zilisambaa sana siku ya jumatano usiku na kuwafanya wanafamilia ambao walizika ndugu zao kwenye makaburi hayo kuwahi makaburini kuangalia kama makaburi yao yamefukuliwa. Makaburi hayo ni miongoni mwa makaburi maarufu ya kihistoria ya mwanzo kuanzishwa kwaajili ya wamarekani weusi. Katika makaburi hayo wamezikwa watu wengi maarufu wa Marekani kama vile Emmett Till, gwiji wa muziki wa blues Dinah Washington na bingwa wa ndondi za uzito wa juu wa zamani Ezzard Charles. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2463022&&Cat=2
   
Loading...