Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Glenn

JF-Expert Member
May 23, 2015
65,757
156,818
Mpendwa mwana JF, unaweza kushangaa kusikia kuwa mbwa ni biashara nzuri kupita hata kufuga ng'ombe kibiashara na ukashangaa.

Uzi huu utakuwa ni maalum katika kupeana uzoefu katika biashara hii ya kufuga mbwa kwa lengo la kujipatia kipato na ulinzi pia.

Tutajifunza aina bora na inayohimili mazingira yetu hasa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Hivyo mdau ikiwa wewe ni mfugaji wa wanyama hawa kibiashara, nakukaribisha sana utupatie uzoefu juu ya aina mbali mbali mfano;

a) German shephard
b) Belgian shephard
c) Bull dog
d) Rottweiler
e) Ridge back nk

mambo muhimu ya kupeana uzoefu;
1) banda/ nyumba bora ya kufugia
2) chanjo
3) Masoko nk

1-threequartersitting.jpg
German-Shepherd-on-White-00.jpg
rotties.jpg




Ni nakukaribisha utupe uzoefu wako na kwa wale wanaotamani kujifunza mnakaribishwa kwa maswali na wadau watakujibu


Maelezo ya German Shepherd hapa

Maelezo ya Belgian Shepherd hapa
 
German shephard;
Kama anavyoonekana hapo juu kwenye picha;
Huyu kwangu ni mbwa bora kabisa kwa ulinzi na Kibiashara;
Mbwa huyu ana nguvu nyingi,
Anafundishika kirahisi na
mwenye mvuto machoni.

Katika majeshi ya nchi nyingi
anatumika kama mmoja wa askari cc Waziri Lugola..hahaha.
Sababu kubwa ni moja yambwa wenye akili na kufundishika.

mbali na majeshi ya nchi mbalimbali kumtumia, pia watu binafsi humtumia kwa ulinzi.
Mbwa huyu anasoko sana endapo utakuwa na mbegu nzuri kwani uzao mmoja waweza kupata vitoto 5 na kuendelea.
Kitoto cha miezi 2 huuzwa kuanzia 700,000 hadi 1,200,000 hapa bongo na Kenya zaidi

SIFA YA MBEGU BORA
1. Masikio yaliyosimama
2. miguu ya mbele ni mirefu
kuzidi ya nyuma...
3. kifua kikubwa
4. miguu ya nyuma kupinda
5. mdomo mrefu
6. rangi ya kaki/kahawia na nyeusi mgongoni
 
Leo tumwangalia huyu Belgian shephard aina ya Malinois, tamka kwa kiswahili "Malinwaa"

Huyu ni Mbwa Kibelgiji aliyefugwa enzi na enzi, Wabelgili waliwafundisha kuchunga kondoo kiasi kwamba waliweza kwenda machungani na kondoo na kuhakikisha wanawarudisha nyumbani salama baada ya saa za malisho.

SIFA
a) ni mbwa mwenye nguvu sana
b) anahimili mazingira magumu
c) Ana akili na anafundishika kirahisi
d) Ni mbwa aliyejaa utayari hasa aliyefundishwa.

***E) Huyu ndiye mbwa anayefaa kwa ulinzi 100%

Kwa hapa Tanzania wanapatikana kwa uchache sana na bei yao iko juu kiasi flani.
Mbwa mdogo wa miezi 2 bei inaanzia 900k


QUOTE="Rama liymo, post: 28656338, member: 461316"]Napenda Sana miubwa hasa hii yenye misikio yakusimam[/QUOTE]karibu mkuu
 
kitoto cha german shephard bora kabisa

Screenshot_20181005-223300.jpeg
 

Attachments

  • Screenshot_20181005-223300.jpeg
    Screenshot_20181005-223300.jpeg
    74.4 KB · Views: 343
  • Screenshot_20181005-223300.jpeg
    Screenshot_20181005-223300.jpeg
    74.4 KB · Views: 376
Hao mbwa walipigwa marufu nchi nyingi ninavyosikiaga, ni hatari sana.

Kuhusu kufuga koko ni hasara sana kwani huwezi hata kuuza akizaa.

Mimi nilianza kwa kufuga koko nikahamia German na belgian shephard sijawahi kujuta.
Napenda kufuga Pitbull ila nasikia ni hatari sana unaweza ukapata kesi ya mauaji ngoja niendelee kufuga hawa wala "NYA".
 
Nimefuga mbwa sana tokea nikiwa mdogo until mambo ya shule yaliponibana nilashindwa na mpaka sasa bado sijarudi ila niko na plan angalau kuanzia mwakani nifunge German Shepherd, Dobbermann na Serbian Husky.
 
Back
Top Bottom