WAFUGAJI wa mazao ya baharini wametakiwa kujikita katika kilimo cha majongoo ya pwani ambacho mahitaji yake ni makubwa katika soko la nje la kimataifa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
kombo ed.JPG

Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Abdalla Hussein Kombo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Abdalla Hussein Kombo, wakati akiwasilisha makadirio, mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021-2022 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.

Alisema wizara tayari imeanza kuwashajihisha wafugaji wa mazao ya pwani ikiwamo majongoo na jumla ya wafugaji 180 wametambuliwa katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba.
Alisema hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa vizimba vinne vya mashamba ya mfano vyenye mita za mraba 1,800 kila kimoja kilijengwa katika bahari ya vijiji vya Mkokotoni, Kama, Shungi, Makunduchi na Chwaka.

Alisema ziara ya kuangalia maeneo yaliotengwa kwa ajili ya ufugaji wa vifaranga vya majongoo umefanyika katika kijiji cha Bungi na Kingungwi na maeneo ya ufugaji wa vifaranga umeanza.

Alisema kituo cha vifaranga kiliopo Beit-el-Ras kinaendelea na kazi za uzalishaji vifaranga hivyo kwa ajili ya wakulima walioamua kujikita katika kilimo hicho.
“Utafiti uliofanywa na wizara umebaini kwamba ufugaji wa mazao ya majongoo ya pwani hivi sasa una tija kubwa na kipato chake ni kizuri kitakachomkomboa mkulima kwa hivyo tumeanza kuwashajihisha walengwa hao,” alisema.

Alisema serikali ya Zanzibar ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa kiwanda cha kusarifu mazao ya baharini ya mwani na kuongeza thamani ya uzalishaji wake.
Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa Chamanangwe, Pemba ambacho kitakuwa mkombozi kwa wakulima wa kilimo hicho ambao asilimia 80 ni wanawake.

Aidha, alisema katika utekelezaji wa mpango kuelekea uchumi wa bluu serikali inakusudia kujenga kiwanda cha kusarifu dagaa huko Mkokotoni pamoja na minofu ya samaki huko Malindi Unguja.

NIPASHE
 
Back
Top Bottom