Wafugaji Rwanda wavamia ardhi TZ waua Watanzania sita Ngara, Serikali yetu iko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafugaji Rwanda wavamia ardhi TZ waua Watanzania sita Ngara, Serikali yetu iko wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jun 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Kamati ya Ulinzi na Usalama yasaka watuhumiwa

  Na Theonestina Juma, Bukoba

  WATANZANIA sita ambao ni wakulima wa Kijiji cha Murbanga Kata ya Mursagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wamevamiwa shambani na kuua kikatili na
  wafugaji wanaosaidikiwa kuwa ni raia wa Rwanda.

  Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati wakulima hao wa Tanzania wakiwa wamepiga kambi katika eneo la pori lililoko katika kijiji hicho, kwa ajili ya kuandaa mashamba kwa kusubiri mvua za vuli na kulinda mazao yao yasishambuliwe na wanyama.

  Habari za uhakika zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Bw. Vitus Mlolere zinasema kuwa waliouwa ni wanaume.

  Habari hizo zinadai kuwa katika tukio hilo, wafugaji hao ambao ni raia wa Rwanda (idadi haijafahamika) walipowakukuta watu hao katika mashamba yao ambako wamejenga vibanda vya muda kwa ajili ya kupumzikia, waliwakamata na kuwafunga kamba mikono kwa nyuma na kuanza kuwashushia kipigo kwa kutumia fimbo na marugu hadi kufa.

  Wakulima hao walikuwa wanane, wawili kati yao walikimbia na kunusurika katika mauaji hayo.Miongoni mwa walionusurika mmoja alikimbia hadi kwa wananchi wanaoishi jirani na kutoa taarifa.

  Kwa sasa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara kwa kushirikiana na polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa imepiga kambi katika pori hilo kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka Wanyarwanda hao wanaosakidiwa kufanya mauaji hayo.

  Kati ya waliouawa, watatu wametambulika kuwa ni Bw. Karabanye Daniel (70), Benedict Bashogongo (65) na Selestine Mawela (47).

  Wakulima wa Kata ya Mursagamba kila mara wamekuwa wakizozana na wafugaji wa Kinyarwanda kwa kuacha mifugo yao kushambulia mzao yao kila kukicha.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Mlolere alisema kuwa atatoa taarifa za mauaji hayo leo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nchi yetu sasa hivi hakuna kiongozi wakufuatilia mauaji haya, inasikitisha sana serikali ya Tanzania yenyewe ni yawauaji sasa unadhani watahangaika kufuatilia raia waliouawa na wageni? nchi haina kiongozi in waigizaji na wauaji

  Waziri wa Mambo ya Ndani Mzanzibari; inaonekana hata hajui Mipaka ya Nci; Wanchaguana kiurafiki na sio kwa mantiki ya kazi
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jeshi letu linafuatilia kwa ukaribu mauaji ya viongozi wa ccm. Mfano yule m/kiti wa halmashauri kule nyanda za kusini, ndani ya siku 10 wauaji 11 wamekamatwa na silaha iliyotumika na nguo walizokuwa wamevaa. Wananchi wa kawaida hawatambuliki.
   
 4. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Serikali yako ya Tanzania bado imelala na itaamka tu Chadema watakapotaka kufanya maandamano.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Uliona wapi "muuaji" akamtafuta "muuaji" mwenzake? Labda kama hao waliouliwa ni "wauaji wenzao". Au labda akawatafute waje washirikiane!
  Tumeshuhudia Polisi wakiua watu Arusha, Tarime, tumeshuhudia watu wakipigwa mabomu na Polisi huko Udom, Tosamaganga, Serengeti. Leo tunaambiwa wamepiga kambi kuwasaka wauaji!? Hiki ni kichekesho cha mwaka! Ngoja nilale bada....
   
Loading...