Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Akina Mama wa jamii ya wafugaji wa Barbaig wa maeneo mbalimbali nchini wamesema wamechoshwa na vitendo vya kubakwa hadi kufa, kuibiwa mifugo, kuchomewa mabanda na waume zao kuuawa na kuambiwa warudi walipotoka huku wakiwa hajaelekezwa mahali pa kwenda.
Wameyasema hayo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, na viongozi wengine wa serikali waliokuwa wamefika kutafuta suluhu ili maiti zilizokuwa zimeachwa kuzikwa sababu ya tofauti ya polisi na wabarbaig hao
"Tukiamka salama tunashukuru Mungu, watoto wetu wa kike wakienda kuchunga wanabakwa hadi wanakufa, vijana ambao ndio wanatulinda wanateswa, kupigwa na kuuawa, sisi twende wapi? walihoji akina mama waliokaribishwa
katika Mkutano huo Polisi wametuhumiwa kuwa wamekuwa wakiiba unga wa mahindi kwenye mabanda ya wafugaji, kuiba maziwa,simu na vitu vyenye thamani wanapovamia na kuchoma nyumba za wafugaji
Katika Mkutano huo baada ya kuridhiana Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameambiwa na wafugaji hao atoe ripoti aliyoificha, na imekubaliwa kuwa askari wanaoenda kwenye operesheni wawe wanajulikana isiwe kwa kuviziana mwanya ambao askari wanautumia kufanya uhalifu kama ilivyotokea na ksuababisha mauaji.
Aidha wabarbaig hao wameomba kila kiongozi wa serkali anapoenda kuwaondoa wafugaji awe anawatajia eneo mbadala sio kufanya ukatili
Mkutano ulidumu kwa saa nne, huku Mwigulu akishindwa kuweka wazi kama askari hao watatuhumiwa au la, ila kwa sasa amesema jeshi la polisi linawashikilia askari hao kusubiri maelekezo ya mwanasheria mkuu tangu Februari 28
Aidha kuhusu Askari aliyeua tangu Mwaka jana, Mwigulu ameitupia lawama ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa ndio haijaleta jalada ili askari PC ERIC afunguliwe mashtaka tangu auwe Agosti 16 Mwaka Jana.