Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo asilimia 99 ya wabunge watakuwa wakitoka CCM basi, na pia kwa kuwa zipo sura mpya kabisa ambazo zimeingia bungeni kwa mara ya kwanza na nyingine kuendelea kukalia nafasi zao basi, huu uzi ni mahsusi kwa ajili ya kuwatambua wale ambao dalili zinaonyesha kuwa watakuwa sehemu ya baraza la mawaziri!

Wafuatao ni top 10 ya wale ambao hawajawahi kuwa wabunge lakini kwa vyovyote wengi wao watakuwa sehemu ya baraza jipya la Mawaziri, wapo watakaokuwa mawaziri kamili na wengine manaibu!

1. Charles Kimei
2. Prof. Adolf Mkenda
3. Prof. Kitila Mkumbo
4. Askofu Josephat Gwajima
5. Jerry Slaa
6. Mrisho Gambo
7. Fredy Lowassa
8. Shaashisha Mafuwe
9. Patrobas Katambi
10. Kirumbe Ng'enda

Lakini pia wapo wengine watakaoteuliwa kuwa wabunge na Mh, hivyo wana nafasi kubwa pia ya kuwa ndani ya baraza hilo!

Kwa hizo sura mpya, na maeneo ambayo pia waligombea ni wazi kabisa ni mkakati mahsusi wa kuwaingiza sehemu nyingine nyeti zaidi!

N.B: Ieleweke kuwa Mh, naye hatabiriki pengine anaweza akabadilisha upepo humo angani na akaendelea na lile baraza lake la awali!
Kanda ya ziwa, tengemea Niko mawaziri wanakotokea. Ukabila Kwanza baada ya wizi wa kura
 
Bongo bwana ni nchi nzuri sana,yenye furaha na amani tele,wepesi wa kusameheana na kusahau yaliyopita.

wana CCM na wanaChadema leohii wanashirikiana kubashiri balaza jipya la mawaziri 2025.
pongezi kwa wote,hivi ndivyoinatakiwa.

uchaguzi huu tulioshinda ni sisi watanzania kama taifa,sio CCM wala Chadema ni watanzania ndio tumeibuka washindi kwenye huu uchaguzi.
Walioshinda ni CCM tu. Huko kusema ni Watz wote ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Kenya wameulahisisha uchumi wao kwa kufungulia fursa za wananchi wao kufanya biashara kimataifa wakiwa nchini mwao online
Hii imekuwa rahisi baada ya system ya kenya kuruhusu mihamala ya kifedha kufanyika kupitia paypal na njia zingine ambazo hapa bongo zimepigwa pini na wakubwa ili kulinda hisa zao mpesa,tigopesa etc
Paypal itapanua wigo wa ajira kwa vijana ndiyo wabongo wengi wanazitafuta laini za sadaricom kenya
Mkuu natamani sana kupata elimu kuhusu hili kama hutajali.
 
1. Charles Kinei - Atapewa uwaziri Fedha/Mipango.
2. Mrisho Gambo - Atapewa wizara ya mambo ya ndani.
3. Hussein Bashe - Atapanda na kuwa waziri kamili Kilimo/Mifugo.
4. Ndalichako - Anarudikua Elimu.
5. Ummy - Atabakia wizara ya Afya.
6. Kalemani - Anabaki nishati.
7. Dotto Biteko - Anabaki madini.
8. Mwanry (X-RC Tabora) namuona akateuliwa kwenye nafasi ya ubunge na atapewa wizara.
9. Paul Makonda - Ni mmoja kati ya vijana watakao teuliwa na kisha kupewa unaibu waziri (mambo ya ndani).
10.........
11...........
12..............
Nitaendelea badae
Kwa hiyo waziri mkuu hakuna?
 
Maboto kutoka Bunda akikosa uwaziri nitajua uchawi upo.. Yule amewashinda wasomi pekee nchi hii wa BOT.
 
Back
Top Bottom