Wafuasi wa Magufuli muelewe, siasa zenu hazina nafasi tena nchi hii, ila wapinzani nao wana wajibu

Kwahiyo Magu aliiga mabaya ya Nyerere kwakuwa sio mambo mapya? Magu alistahili kutawala enzi za ujima, lakini hakustahili kuwa kiongozi enzi hizi za wastaarabu.
Kama katiba na system inaruhusu, atakuja tuu Magu mwingine.
 
Mbowe aliishiwa Hela za kulipa mawakili, akaitisha mchango mitandaoni akapata chini ya milioni tano, alijiaminisha Chadema Ina watu watamchangia, hawakuchanga, alivyoona wanachadema wamemtelekeza, akaamua kuomba radhi kwa SSH.

Akaona hana haja ya kujiumiza kukaa gerezani kwa ajili ya Wana Chadema wenye roho ya ubinafsi
Ndo yale yale alosema mtoa mada watu wa Magufuli mlikua mkipika data na mlizoea uongo...

Alipata chini ya milioni tano?

Nyie ni mashetani ona hii data then uje tena.
Screenshot_20220305-232137_Samsung%20Internet.jpg
 
Pamoja na matatizo mengi Tanzania ilyokuwa nayo kabla ya mwaka 2016 lakini ilikuwa katika njia nzuri na ilikuwa inapiga hatua, Then akaingia Magufuli ambaye wengi, ikiwemo mimi nilidhani atatatua matatizo mengi ya nchi yetu kwa kipindi kile

Lakini Magufuli alikuja na siasa mpya ambazo ziliongeza matatizo ambayo hayakuwepo, siasa za kugombana na majirani na kufungiana mipaka, kugombana na jamii ya kimataifa, siasa za kupika takwimu, siasa za kuua sekta binafsi na kufilisi wafanyabishara, siasa za kufungia vyombo vya habari na kuvitisha visiandike habari fulani, siasa za kuhonga na kulazimisha wapinzani wakuunge mkono, siasa za kuteka na kuua watu wanaokukosoa kubambikiza kesi n.k

Uongozi wa Samia hautakuwa perfect, utakuwa na mabaya yake lakini angalau ameonyesha nia ya kuachana na siasa hizi zilizoturudisha nyuma sana, Samia alionyesha nia hii tangia hotuba yake ya kwanza lakini akapelekwa chaka na elements za Magufuli zilizokuwa zimesalia Serikalini na kwenye chama

Wapinzani nao wana wajibu wa kufanya compromise zao, wana madai mengi ya msingi lakini hayawezi kutekelezwa yote kwa wakati mmoja

Kuna yale ya msingi kama watu waliofungwa au wenye kesi za kubambikizwa hawa wafutiwe tu mara moja

Pia waachane na watu wa siasa za kali za matusi, wanaojifanya wana uchungu sana na nchi, waliona jinsi akina Kigogo na Mange walivyowageuka, watu wa siasa hizi sio wa kuwaamini na wanawaharibia taswira ya upinzani, kama kuna wanachama wao wenye tabia hizi wawafundishe pia

Upinzani kazi yake ni kutafuta mapungufu ya serikali na ku offer alternative, sio kazi yao kusifia, kwa hiyo serikali isitegemee wala isilazimishe kusifiwa na wapinzani
Uzi umetulia
 
Back
Top Bottom