Wafuasi wa CHADEMA wana maslahi gani na chaguzi nje ya Tanzania?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Ndugu zangu,

Kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania kuisha tumeshuhudia jinsi wafuasi wa CHADEMA wanavyopambana katika harakati za kisiasa mitandani katika kila nchi duniani kipindi cha uchaguzi.

Baada ya saa moja kwa waganda kumaliza kupiga kura tumeshuhudia wafuasi wa CHADEMA nchini wakisambaza matokeo ya uchaguzi kutoka sehemu mbalimbali nchini Uganda.

Si Uganda tu, wafuasi wa CHADEMA walishiriki harakati za uchaguzi katika nchi ya Kenya, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Amerika, Afrika kusini, Urusi, Uingereza nk.

Nini haswa dhumuni la wanaharakati hawa kushiriki chaguzi hizo huku wakionesha hisia na ushabiki mkubwa kama vile kuna manufaa ya moja kwa moja wanayapata.

Nakaribisha mjadala usioumiza
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,251
2,000
Kiongozi wa kusambaza matokeo ya Uganda ni Hilda Newton
Matokeo ya uchaguzi ni kama matokeo ya mechi ya soka. Sioni ubaya wa watu kusambaza au kupata habari za matokeo ya mchuano wowote ule. Labda ungeweka hadharani, ni kitu gani kinachokusumbua kama habari ikiwekwa hadharani?
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,435
2,000
"Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja". Huu ulikuwa msimamo wa TANU na ni wa mapendo makubwa sana.

Tunaishi kwenye dunia moja. Kinachotokea popote kinatuhusu. Na Waganda ni ndugu zetu wa karibu. Nimefurahi kuona wanavyohesabu kura kwa uwazi. Laiti tungekuwa hivyo.

Don't be parochial. Have a global view of things.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,122

Tume ya Uganda kidogo ina nafuu kuliko hili tawi la CCM(NEC)
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,122
2,000
Matokeo ya uchaguzi ni kama matokeo ya mechi ya soka. Sioni ubaya wa watu kusambaza au kupata habari za matokeo ya mchuano wowote ule. Labda ungeweka hadharani, ni kitu gani kinachokusumbua kama habari ikiwekwa hadharani?
Watu wanashabikia ligi kuu ya Uingereza na hasemi mbona!
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,129
2,000
Umejuaje kama ni wafuasi wa Chadema?
Huna kazi nyingine za kufanya?

CHADEMA HUYU HAPA Erythrocyte
CHADEMA AKIMPONDA MUSEVENI JUKWAA LA WAGANDA

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Unamslahi gani na uchaguzi wa Uganda?
Matokeo ya uchaguzi ni kama matokeo ya mechi ya soka. Sioni ubaya wa watu kusambaza au kupata habari za matokeo ya mchuano wowote ule. Labda ungeweka hadharani, ni kitu gani kinachokusumbua kama habari ikiwekwa hadharani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom