Wafuasi wa CHADEMA wafikishwa mahakamani - Arusha

Naomba Nanyaro uje utupe updates. Kama walifanikiwa kuwapatia dhamana au la!
Nadhani Ngongo leo atakuwa ameumbuka sana maana jana alikataa kabisa kwamba hakukuwa na mgomo wa vifodi. Habari za leo zitakuwa zimemuumbua maana ziwethibitisha ukweli.

Moja kati ya sababu za mgomo ni kutaka Zuberi atimuliwe kwa kuwaita watu panya. Angalau ameshtakiwa na polisi wanamchunguza. Kwahiyo kuna mafanikio flan kwenye mgomo wa jana.

Kuhusu kesi, mm nadhan hakimu mwenye akili timamu ataitupilia mbali. Sababu waliokamatwa ni vijana wa eneo la december ambapo vifodi vinavyopita ni vinavyopita barabara ya dodoma tu. Vifodi ya sakina, ngaramtoni, ngulelo, tengeru, usa, njiro, kijenge, mwanama, moshono, unga ltd hazipiti december na zilikuwa zimegoma. Sasa vijana wa pale wanahusika vp na kugoma kwao!? Hiyo ni kesi ya kipuuzi kabisa na kwakuwa ipo kwa hakimu "mkazi" atakuwa analifahamu jiji vzuri na ataitupilia mbali! Labda awe influenced na magamba!
 
Sijuhi kwa nini wakazi wa mjini wa Arusha wamekuwa na Akili finyu kiasi hiki, uwezi kukubali mawazo mfu ya huyu kijana Lema
 
Hakuna mabadiliko yanayoweza kupatikana kirahisi garama ya kupata mabadiliko mara nyingi huwa kubwa sana chamsingi ni sisi kutokukata tamaa kazi ni moja tu kusonga mbele hakuna kurudi nyuma ccm wameshazingirwa pande zote na sasa hawana pa kutoke ni sawa na Gadafi siku zake za mwisho kama ni meli baharini ni dhahiri imesha zama nusu tumieni hao mapolisi ,jwtz lakini mjue lazima mtang'oka tu hata iweje iwe kwa hiari ama kwa nguvu mtaondoka
 
Kwa ujumla walikamatwa watu 46 jana,22 wakaachiwa kutoka kituo cha polisi,na 24 wamefunguliwa mashtaka mawili,la kwanza Uharibifu wa mali,na kushusha watu kwenye daladala,kati ya 24 waliofikishwa mahakamani 22 tumeweza kuwadhamini na 2 ilishindikana baada ya hakimu kudai amechoka,ilikuwa majira ya saa kumi na moja kasoro,hivyo tunategemea kuwatoa kesho kwa remove order.Eneo ambalo wanadaiwa kuharibu daladala ni Sabena,wakati hakuna hata mmoja aliyekamatiwa sabena,wengi ni wa December tena wamekamatiwa kwenye maduka yao
Hiki ndicho tunachokipinga,kimsingi polisi wanafanya kazi ya siasa,na kwa maelekezo,pamoja na vitisho vyote bado umma wa Arusha umeendelea kuwa na mshikamano mkubwa,Nawapongeza sana kwa kuja mahakamani kwa wingi
Kamwe hatutarudi nyuma,wala hatutaogopa..
 
Poleni Nanyaro ,si wataumbuka hivi mahakimu nadhani pia hawajisikii vizuri kutwa kujaziwa mikesiisiyo na kichwa wala mkia
 
Hapa wamesahau kwamba wanawapitisha wapiganaji kwenye tanuru la moto..basi kama hawajatambua, kitakachotoka ni chuma imara cha pua!! kitakuwa chachu ya kuutokomeza kabisa utawala huu wa kidhalimu tunaoshuhudia kwa sasa.
Mkuu Nanyaro na wapiganaji wote Arusha ni kukaza buti tuu..mpaka kieleweke
 
Sijuhi kwa nini wakazi wa mjini wa Arusha wamekuwa na Akili finyu kiasi hiki, uwezi kukubali mawazo mfu ya huyu kijana Lema

Asante sana kwa kututukana wakazi wa Arusha. Ni kweli tuna akili finyu kiasi. Lakini ni akili FINYU hizi hizi zilizomchagua Chaguo La Mungu 2005...At least Lema stands for something whether you like it or not, Rais wetu ana stand for what? Chama chake kina stand for what zaidi ya kutetea na kuficha madhambi ya waliomuweka madarakani. Hakuna marefu yasiyo na ncha ndugu yangu. Sisi tutaendelea kuwa mufisili wa akili, lakini atleast tuna msimamo.
 
Hata wkikamata CDM yote haisaidii, dawa ni kujua kwamba maandamano sio dhambi. Na CCM sio Mungu. Na wao ni walinzi wa amani sio wachochezi wa fujo, matusi na dharau kwa wabunge.
 
Wanaume watakununulia mtandio wewe.
Nao ni mchango pia.
Hivi kupiga watu na mawe na kushusha watu kwenye daladala ndo mnachokishabikia? Kisa mnataka kuwalazimisha watu wote wawe chadema na lema?
Ndo maana na sema hivi, wakati mwengine kukubaliana na mawazo ya wanachadema lazima ufikirie kwa kutumia makalio na ubongo uupeleke likizo kwanza.
 
Kwa ujumla walikamatwa watu 46 jana,22 wakaachiwa kutoka kituo cha polisi,na 24 wamefunguliwa mashtaka mawili,la kwanza Uharibifu wa mali,na kushusha watu kwenye daladala,kati ya 24 waliofikishwa mahakamani 22 tumeweza kuwadhamini na 2 ilishindikana baada ya hakimu kudai amechoka,ilikuwa majira ya saa kumi na moja kasoro,hivyo tunategemea kuwatoa kesho kwa remove order.Eneo ambalo wanadaiwa kuharibu daladala ni Sabena,wakati hakuna hata mmoja aliyekamatiwa sabena,wengi ni wa December tena wamekamatiwa kwenye maduka yao
Hiki ndicho tunachokipinga,kimsingi polisi wanafanya kazi ya siasa,na kwa maelekezo,pamoja na vitisho vyote bado umma wa Arusha umeendelea kuwa na mshikamano mkubwa,Nawapongeza sana kwa kuja mahakamani kwa wingi
Kamwe hatutarudi nyuma,wala hatutaogopa..
mkuu kama ni kweli wamewakamata watu wasiohusika naungana na wewe kuwashutumu hawa polisi kwa kutumika kisiasa.
 
Sijuhi kwa nini wakazi wa mjini wa Arusha wamekuwa na Akili finyu kiasi hiki, uwezi kukubali mawazo mfu ya huyu kijana Lema

rev.robinson aliyepo itally ni shoga, sijui wote wenye majina hayo ni mashoga? kana tuhuma mkuu.
 
Nao ni mchango pia.
Hivi kupiga watu na mawe na kushusha watu kwenye daladala ndo mnachokishabikia? Kisa mnataka kuwalazimisha watu wote wawe chadema na lema?
Ndo maana na sema hivi, wakati mwengine kukubaliana na mawazo ya wanachadema lazima ufikirie kwa kutumia makalio na ubongo uupeleke likizo kwanza.

Hivi unadhani ilikuwa na furaha sana pale mahakamani Zuberi alipowaita watu panya. Au unafikiri ni jambo la kawaida kwa kamanda wa polisi kusema Lema anataka kuwateka familia yake na yupo hatarini? Au unadhan ni sawa tu kwa kamanda huyu kumtishia Lema kwamba lazima amweke ndani tu?

If that is wat U think, lazima kunakitu kimeingia kwenye masaburi yako!
 
Kwa ujumla walikamatwa watu 46 jana,22 wakaachiwa kutoka kituo cha polisi,na 24 wamefunguliwa mashtaka mawili,la kwanza Uharibifu wa mali,na kushusha watu kwenye daladala,kati ya 24 waliofikishwa mahakamani 22 tumeweza kuwadhamini na 2 ilishindikana baada ya hakimu kudai amechoka,ilikuwa majira ya saa kumi na moja kasoro,hivyo tunategemea kuwatoa kesho kwa remove order.Eneo ambalo wanadaiwa kuharibu daladala ni Sabena,wakati hakuna hata mmoja aliyekamatiwa sabena,wengi ni wa December tena wamekamatiwa kwenye maduka yao
Hiki ndicho tunachokipinga,kimsingi polisi wanafanya kazi ya siasa,na kwa maelekezo,pamoja na vitisho vyote bado umma wa Arusha umeendelea kuwa na mshikamano mkubwa,Nawapongeza sana kwa kuja mahakamani kwa wingi
Kamwe hatutarudi nyuma,wala hatutaogopa..

Mkuu asante kwa taarifa. Hongereni kwa kufanikiwa kuwatoa hao 20. Najua hata hao 2 wataachiwa tu maana "wao wana pesa, sisi tuna Mungu!". Mapambano yanaendelea na hakuna kulala hadi kieleweke!
 
Nisomapo, nisikiapo na hata kuona mambo yanavyotendeka humu nchini, nakumbuka historia ya ukandamizaji wa dini uliotokea miaka ya 1880s wakati wa Utawala wa Kabaka Mutessa II, akiwaua na kuwafunga watu hata kuwachoma moto na hadi leo kwa wale wakristu wanatambua Mashahidi wa Uganda waliokubali kuchomwa moto huku wakimwomba Mungu wao kwa kusema: Tumeamua kuifia dini yetu, kamwe hatuko tayari kuona unyanyasaji wa Kabaka ukiendelea kwa waganda wenzetu waislamu kwa wakristui.

Mwisho wa Kabaka ulikuwa mbaya. Alitolewa madarakani kwa nguvu, akakimbilia kwa wazazi, walezi na marafiki ya wale aliowaua. Mwisho alikufa kifo kibaya na kuzikwa kama Mbwa. Hii ndio stahili kwa utawala wa kimabavu kwa viongozi wa sasa, hasa CCM. Tumeona Libya, amezikwa kichakani. Tumeona Misri, amepelekwa mahakamani kwenye machela! Tumwombe Mungu awatokee ndotoni Watawala wafumbuke wajue kuwa mwisho unakaribia.
 
Wana JF,

Kwa Mujibu wa Mwana harakati aliyeko arusha kani juza kuwa wale wanachama wa CHADEMA waliokamatwa na Police Mtaa wa DECEMBER jana mchana wakiwa kwenye shughuli zao bianafsi na kuswekwa rumande(Police) kwa sasa wako mahakamani.

NB;
Na yasemekana M/Kiti wa BAVICHA hayomo kwenye kundi Hilo bali ameonekana na yupo akifanya utaratibu wa kuwawekea mdhamana wanachama hao

Kwa walio Arusha mtujuze zaidi

Natamani ningekuwepo. Ningehamasisha wote tukatae mdhamana. Ndugu zetu wangekuja kutukomboa, wakawakamat, wakaingizwa mahakamani, nao wakakataa mdhamana. Huku mikoani tungeandamana, wangetukamata, wakatupeleka mahakamani, tungekataa mdhamana. Mwisho ungekuwaje? Tafakari!!
 
Back
Top Bottom