babayah67
JF-Expert Member
- Mar 28, 2008
- 493
- 79
Nikiwa njiani kutoka nyumbani (Ukonga) kuja kazini (Ubungo) yalipita magari matano ya FFU yakielekea Ubungo. Bahati nzuri kiti nilichokaa alikuwepo mwanaharakati wa Chadema, akawa akapigiwa simu na "Jamaa toka Usalama wa Taifa" akimtuma ajaribu kuwahi kwenda ubungo na amweleze mgombea wa ubungo wa Chadema ajaribu kwa kila hali kuwasihi wanachama wasifanye fujo yoyote ile wawe watulivu na wayasubiri matokeo bila kufanya fujo. Yule bwana akamwambia kuwa mbinu inayotumika sasa ni kuchelewesha kutangaza matokeo haya ya ubungo, kwa lengo la kuwafanya vijana wa chadema washindwe kuvumilia waanze fujo, na polisi waingilie kwa mabomu na uchaguzi ufutwe. Sasa hizi ndio njama zinazotumika. Viongozi wa Taifa Chadema mnatakiwa kujaribu kuwazuia vijana wasifanye fujo na hapohapo toeni tamko rasmi kwa tume.