Elections 2010 Wafuasi wa chadema tumieni busara kunusuru uchaguzi kufutwa ubungo!!!

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Nikiwa njiani kutoka nyumbani (Ukonga) kuja kazini (Ubungo) yalipita magari matano ya FFU yakielekea Ubungo. Bahati nzuri kiti nilichokaa alikuwepo mwanaharakati wa Chadema, akawa akapigiwa simu na "Jamaa toka Usalama wa Taifa" akimtuma ajaribu kuwahi kwenda ubungo na amweleze mgombea wa ubungo wa Chadema ajaribu kwa kila hali kuwasihi wanachama wasifanye fujo yoyote ile wawe watulivu na wayasubiri matokeo bila kufanya fujo. Yule bwana akamwambia kuwa mbinu inayotumika sasa ni kuchelewesha kutangaza matokeo haya ya ubungo, kwa lengo la kuwafanya vijana wa chadema washindwe kuvumilia waanze fujo, na polisi waingilie kwa mabomu na uchaguzi ufutwe. Sasa hizi ndio njama zinazotumika. Viongozi wa Taifa Chadema mnatakiwa kujaribu kuwazuia vijana wasifanye fujo na hapohapo toeni tamko rasmi kwa tume.
 
Tuko ktk hatua ya kutangazwa na Tume sasa hivi. HATUNA WASI TUNASUBIRI TAMKO RASMI TU, BASI!
 
PLZ naomba muwe watulivu wakose cha kufanya mana kila njia wanayotaka kutumia haiwatoshi.Viongozi wa chadema tunaomba muwahimize ndugu zetu watulie .
 
nikiwa njiani kutoka nyumbani (ukonga) kuja kazini (ubungo) yalipita magari matano ya ffu yakielekea ubungo. Bahati nzuri kiti nilichokaa alikuwepo mwanaharakati wa chadema, akawa akapigiwa simu na "jamaa toka usalama wa taifa" akimtuma ajaribu kuwahi kwenda ubungo na amweleze mgombea wa ubungo wa chadema ajaribu kwa kila hali kuwasihi wanachama wasifanye fujo yoyote ile wawe watulivu na wayasubiri matokeo bila kufanya fujo. Yule bwana akamwambia kuwa mbinu inayotumika sasa ni kuchelewesha kutangaza matokeo haya ya ubungo, kwa lengo la kuwafanya vijana wa chadema washindwe kuvumilia waanze fujo, na polisi waingilie kwa mabomu na uchaguzi ufutwe. Sasa hizi ndio njama zinazotumika. Viongozi wa taifa chadema mnatakiwa kujaribu kuwazuia vijana wasifanye fujo na hapohapo toeni tamko rasmi kwa tume.

ungetusaidia sana kama ungequote na kifungu cha sheria inayoruhusu kufutwa kwa uchaguzi.
 
Wakati mwingine actions zinahitajika ili kubadilisha mifumo ya ukandamizaji
 
ungetusaidia sana kama ungequote na kifungu cha sheria inayoruhusu kufutwa kwa uchaguzi.

Panapotokea fujo na hasa polisi wanapotumia mabomu na kumwaga maji ya kuwasha, ni rahisi kwao kusema kuwa kuna masanduku ya kura yameibiwa. Katika hali kama hiyo huitaji kifungu cha sheria kufuta matokeo!!!!
 
TAYARI MYIKA YUKO MJENGONI,UBUNGO AMEIKOMBOA NA SASA IVI YUKO Live Itv by alfred masako Itv. Ee Mungu sasa naweza kwenda kulala kabla sijaamia Kawe kurudisha jimbo. Halima mdee usiofu tunakuja! Asante wanaJF kwa sauti zenu!
 
Back
Top Bottom