Developer IOS
JF-Expert Member
- Jun 20, 2017
- 1,457
- 1,409
Habari wakuu,
Wafuasi wa CHADEMA na viongozi wao wameibuka na kumshambulia Rais na Serikali yake kwa kudai Serikali inaminya demokrasia kisa wamekatazwa kufanya mikutano na maandamano yenye lengo la uvunjifu wa amani nje ya majimbo yao.
Lakini lengo langu sio kuzungumizia hilo bali ni kuzungumzia unafiki au kutojielewa kwa wafuasi na viongozi wa CHADEMA wanaodai wanapigania demokrasia.
Je, demokrasia wanayoitaka ni ipi?
Kwasababu me navyoelewa demokrasia inahusisha kuthamini mawazo ya mtu hata kama mmepishana mawazo na kubishana kwa hoja sio kejeli wala matusi.
Tumeshuhudia tukianzia kwenye bodi watu CHADEMA wakijipa legitimate kuwa wao ndo wapo sahihi na yeyote atakayepingana mawazo yake atashambuliwa kwa matusi kejeli na kuonekana anajipendekeza.
Yeyote atakayeripoti mambo mazuri ya Serikali ambayo ni mengi na yanaonekana atashambuliwa.Upinzani sio tu kukosoa Serikali upinzani dhabiti unapaswa kupongeza pale Serikali inapopatia.
Tukirudi kitaifa tujikumbushe pale Lazaro Nyalandu,Lowassa na wengine wengi walipohama chama tawala na kujiunga nao walishangilia na kuona ile ni demokrasia lakini wakina Mtolea,Waitara na wengine walipoenda chama tawala wakasema wamenunuliwa na waliwashambulia kwa matusi na kejeli.
Wakina Kakobe walipokosoa Serikali walikuwa mashujaa lakini walipoenda kumueleza matatizo yao Rais Magufuli mkawatukana.
Je, mlitaka shida na kero zao nani kama sio Rais.
Je, mlitaka wapingane na maandiko yanaowataka waheshimu mamlaka?