Wafuasi wa CCM wampiga m/kiti wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafuasi wa CCM wampiga m/kiti wao

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtoboasiri, Nov 16, 2010.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wafuasi wa CCM wampiga m/kiti wao Send to a friend Mwananchi: Monday, 15 November 2010
  Joyce Joliga, Songea

  MWENYEKITI wa CCM wa Kata ya Bombambili, katika Manispaa ya Songea, Alphonce Haule (51) amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na mawe, fimbo na makopo.

  Habari zilisema kitendo hicho kimefanywa na wafuasi na wanachama wa chama hicho, ambao pia walimkimbiza Katibu wa tawi hilo, Athuman Ngangilo.
  Tukio hilo lilitokea saa 4:00 asubuhi ya jana na habari zilisema wanachama na wafuasi hao, wamekerwa na matokeo ya uchaguzi, katika eneo hilo.

  Kwa mujibu wa habari zilizopatikana katika eneo hilo, wanachama na wafuasi wa chama hicho, wanawatuhumu viongozi hao kuwa wamekisaliti chama chao na kushiriki katika kuipigia kampeni Chadema.
  Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, wanachama hao waliokuwa na jazba, walisema kuwa kitendo kimesababisha kata hiyo kuchukuliwa na upinzani.

  Walisema viongozi hao ni wasaliti wakubwa na ambao walikuwa na lengo la kukuhujumu chama, ili kukose ushindi kama ilivyojitokeza.Mmoja wa wanachama hao, Apronia Miti, ambaye ni mkazi wa Bombambili, aliwaambia waandishi wa habari kuwa haiji akilini kwa kata hiyo kuchukuliwa na Chadema kwa urahisi mno.

  Alisema kitendo kilichofanywa na viongozi hao, kimewaudhi na kuwakera wanachama na wafuasi wa CCM na ndiyo maana wameamua kuwashambulia kwa mawe.
  Kwa Mary Komba, alisema kimsingi wanachama wa CCM katika kata hiyo, wamechoshwa na uongozi wa kuanzia ngazi ya wilayani hadi katika kata yo hata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

  Alisema mara kadhaa wamewasilisha wilayani, malalamiko kuhusu watu wanaokihujumu chama, lakini viongozi wa wilaya, walishindwa kuchukuwa hatua.

  Kwa upande wake, Haule alikiri kutokea kwa vurugu zilizoambatna na kumshambulia na kwamba tayari ametoa taarifa polisi.Alisema amejeruhiwa kichwani na kwamba alikwenda katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
  hatua za kisheria.atibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya ya Songea Mjini, Zongolobe Zongo, alikiri kupokea taarifa za vurugu hizo .
   
 2. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizo piga piga zitakuwa nyingi sana kwenye hii miaka mitano maana kuna watu wamejilazimisha kuwa viongozi wa wananchi.

  CCM wanafikiri watanzania watakuwa wajinga milele, sasa waTZ wameamka huwezi kuwapangia waongozwe na nani.

  Kama wananchi wako tayari kuchanga hela na kumpinga kiongozi fulani madarakani wewe unafikiri wakimpata huyo kiongozi watamfanyaje.

  Amkeni waTZ mafisadi ni wabaya, ukitaka kujua hilo baada tu ya uchaguzi wamepandisha bei ya vitu bila sababu, maana waliichangia sana ccm na lazima hela yao irudi.

  Matokeo yake wanapandisha bei ya vitu kama unga, mafuta, bidhaa zote za madukani zimeongezeka bei kwa kati ya 100/= na 3000/= this is very bad.
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  na bado
   
 4. lufunyo

  lufunyo Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namkumbuka Nyerere alishasema Wapinzani wa kweli watatoka ccm! Enyi ccm nani kawaroga? nani kawambia hao viongozi wenu wanawahujumu? tumieni akili kidogo kugundua kuwa hata baadhi ya viongozi wenu wamegundua kuwa ni wakati muafaka wa kuangalia mustakabali wa taifa na siyo chama tena! Fungueni milango ya ubongo wenu na siyo madirisha pekee. Mtapigana saaaaaaaana mwaka huu. :yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield:
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukiona moshi ujue............na mwaka 2015 hawatapiga wa kata tu, watapiga hadi wa taifa na bila shaka wakati huo mkwere bado atakuwa kitni na atakuwa ndie mhujumu mkuu wa chama. WAIT AND SEE
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wangejua wasubiri siku Kikwete atakapokwenda Songea wafanye kama walivyofanya wenzao wa Mbeya. Wamtupie mawe kuonyesha kutoridhika kwao. Yeye ndiye kasababisha nchi nzima madiwani wa CCM wameshindwa vibaya. Kumpiga mwenyekiti wa mtaa ni kumuonea tu. Shida iko taifani kwa Jakaya na Makamba.
   
Loading...