Wafuasi CHADEMA wadai mabadiliko ya katiba ya chama kwanza

Tuanze na katiba ya nchi kwanza hii ya Chadema haihitaji Suluhu kuiunda upya.
Unaanzaje kusafisha uso wakati mikono yako michafu?!! matokeo yake utapakaza uchafu tu!
CDM wanapaswa kwanza wasafishe uchafu walio nao ili angalu wapate uhalali wa kuzungumzia mambo ya kitaifa.
charity begins at home. inakuwaje nafasi ya mwenyekiti inakuwa ya kudumu?! Demokrasia iko wapi hapo jamani?!
kama ni kweli katiba ya chadema iko hivyo basi tuone aibu.
 
Unaanzaje kusafisha uso wakati mikono yako michafu?!! matokeo yake utapakaza uchafu tu!
CDM wanapaswa kwanza wasafishe uchafu walio nao ili angalu wapate uhalali wa kuzungumzia mambo ya kitaifa.
charity begins at home. inakuwaje nafasi ya mwenyekiti inakuwa wa kudumu?! Demokrasia iko wapi hapo jamani?!
Tujadili swala liiloko mezani kwanza.
 
kuna kipindi angalu nilisikia CCM inajivua gamba lkn Chadema tangu izaliwe sijawahi kusikia inajivua gamba!! kulikoni?
naishauri chadema ianze na kurekebisha katiba yake kwanza.
Gamba lipi lilivuliwa? Magamba yote mpo nayo
 
Tujadili swala liiloko mezani kwanza.
wanachama wanalalamika kuwa Katiba ya CDM haizingatii misingi ya kidemokrasia. tuanzie hapo kwanza, tusafishe mikono yetu kwanza ili tuweze kuaminika kwa wananchi.
tuondowe kibanzi kwenye jicho letu kwanza.
 
Ndugu zangu,

Siku zinaenda kasi sana
===

VIONGOZI WA CHADEMA WAPINGANA VIKALI NA MBOWE KUHUSU DAI LA KATIBA MPYA.

Viongozi na Wanachama wa CHADEMA wakiongozwa Mkuu wa Kanzidata ya CHADEMA-Kanda ya Kati Ndugu Mackdeo Shilinde wamepingana vikali na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuhusu madai yake ya Katiba Mpya. Viongozi na Wanachama hao wamedai kwamba mabadiliko ya Katiba yaanze kwanza ndani ya Chama chao cha CHADEMA kwa kubadirisha Katiba yao.

Kwenye mkutano huo wamesisitiza kuwa katiba ya chama chao ina mapungufu mengi na kusema ifanyiwe marekebisho kabla hata hawajadai katiba mpya ya Tanzania

Wamesema katiba inayotumika sasa inakinzana kabisa na chama chao kinachojinasibu kuwa chama cha demokrasia

Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 26, 2021 wanachama hao wamesema Katiba ya sasa ya CHADEMA haina uhai na haibebi misingi ya demokrasia.

Sambamba na hilo, Wanachadema hao wameeleza kuwa katiba ya Chadema ina mapungufu kwenye suala la kuhoji mapato na matumizi ambapo inawapa mamlaka watu wachache kujua matumizi ya chama.

"Tubadili kwanza Katiba yetu ndio tupiganie Katiba ya nchi. Alisema Kiongozi wao Mackdeo Shilinde.

View attachment 1869267
View attachment 1870485
Wakanye. Wamevimbiwa hao.!
 
Back
Top Bottom