Wafuasi CHADEMA wadai mabadiliko ya katiba ya chama kwanza

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,250
2,000
Ndugu zangu,

Siku zinaenda kasi sana
===

VIONGOZI WA CHADEMA WAPINGANA VIKALI NA MBOWE KUHUSU DAI LA KATIBA MPYA.

Viongozi na Wanachama wa CHADEMA wakiongozwa Mkuu wa Kanzidata ya CHADEMA-Kanda ya Kati Ndugu Mackdeo Shilinde wamepingana vikali na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuhusu madai yake ya Katiba Mpya. Viongozi na Wanachama hao wamedai kwamba mabadiliko ya Katiba yaanze kwanza ndani ya Chama chao cha CHADEMA kwa kubadirisha Katiba yao.

Kwenye mkutano huo wamesisitiza kuwa katiba ya chama chao ina mapungufu mengi na kusema ifanyiwe marekebisho kabla hata hawajadai katiba mpya ya Tanzania

Wamesema katiba inayotumika sasa inakinzana kabisa na chama chao kinachojinasibu kuwa chama cha demokrasia

Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 26, 2021 wanachama hao wamesema Katiba ya sasa ya CHADEMA haina uhai na haibebi misingi ya demokrasia.

Sambamba na hilo, Wanachadema hao wameeleza kuwa katiba ya Chadema ina mapungufu kwenye suala la kuhoji mapato na matumizi ambapo inawapa mamlaka watu wachache kujua matumizi ya chama.

"Tubadili kwanza Katiba yetu ndio tupiganie Katiba ya nchi. Alisema Kiongozi wao Mackdeo Shilinde.


 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,440
2,000
Hawa ni vibaka wa uvccm
FB_IMG_1627310183346.jpg
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,408
2,000
Kwenye mkutano huo wamesisitiza kuwa katiba ya chama chao ina mapungufu mengi na kusema ifanyiwe marekebisho kabla hata hawajadai katiba mpya ya Tanzania

Wamesema katiba inayotumika sasa inakinzana kabisa na chama chao kinachojinasibu kuwa chama cha demokrasiaMaendeleo hayana vyama

Kazi iendelee
 

HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
3,198
2,000
Kuna mijutu mipumbavu sana... Kwa utandawazi huu yanadhani nani wa kumdanganya? Halafu chadema hawana mmbunge hata mmoja, Mbowe wamemfunga, wanashindana nao yann? Kuna nn ndani ya chadema mpaka kijani wakose usingizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom