Wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wakamatwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, July 21, 2012

  [​IMG]

  Na Mohammed Mhina | Jeshi la Polisi - Zanzibar


  ZAIDI ya wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana kwenye eneo la Darajani mjini Zanzibar. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa mawe, vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.

  Kamanda Aziz amesema kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa kikundi hicho waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo zilizokuwa nimeendelea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar. Amesema wafuasi hao walitumia mawe, chupa na vipande vya mbao kuwarushia Polisi lakini amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa nane usiku wa kuamkia leo, Hata hivyo Kamanda Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi wa kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.

  Amesema vurugu hizo ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu hadi saa 8.00 usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika maeneo mbalimbali wakifanya vurugu. "Tunawatafuta viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na kujisalimisha wenyewe Polisi." Alisema Kamanda Aziz.

  Mara baada ya kuanza kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za Darajani na mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, ilikuwa haia hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama. Hata hivyo biashara mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku watumishi wa Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji wa mawe, matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.

  Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma za kuanzisha ghasia.

   
 2. Collins

  Collins Senior Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa watu kama wameanza kuleta virugu hata usiku basi inaonyesha dhahiri ni magaidi
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  uzao wa binamu nyama ya hamu si wazima kiakili.Zenj ni nursery ya ugaidi na uamsho ni vi-piglets.Kwa muonekanao CCM waakuja jutia sana hii habari nasi tukianza wawachia moto hawa waislam siku wanaingia kubaya.Na hali ikifikia huko viongozi waliojionyesha kuwa wajinga katika serikali watakuwa wameshchoshwa na kuwekwa katik mazingira ya kuwa halal.Mwinyi alionja, muthihiri aliwahi chapwa na Mama wa bendi.Soon hawa jamaa ccm wataanza fia kwa vimada
   
 4. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hawa watu walimpiga kibao hadi Mzee Mwinyi.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  zanzibar one day itageuka somalia...na vile ilivyo kisiwa sijui watafanya nini
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Raymond Kaminyoge na Salma Said, Zanzibar

  JESHI la Polisi linawashikilia watu 43 kwa tuhuma za kufanya vurugu zinazodaiwa kuchochewa na viongozi wa taasisi za kidini na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki).


  Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo mjini humo jana zilieleza kuwa, pamoja na kuwashikilia watu hao linaendelea kuwasaka viongozi wa Jumiki, wanaodaiwa kukimbilia kusikojulikana baada ya polisi kuingilia kati vurugu hizo juzi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohamed aliwataja viongozi wanaotafutwa kuwa ni Msemaji wa Taasisi za Kidini Farid Hadi Ahmed, Kiongozi wa Uamsho, Mselem Ali Mselem, Naibu Kiongozi wa Uamsho, Azan Khalid Hamdan na Mhadhiri wa Uamsho, Mussa Juma Issa.

  Kamanda huyo alidai kuwa katika vurugu hizo za juzi, ambazo viongozi wa Uamsho wamekana kuhusika, vijana hao walikata miti iliyokuwa pembeni mwa barabara, kuvunja vioo vya nyumba na magari pamoja na kuweka mawe na vitu vizito barabarani kuzuia magari yasipite.

  Kamanda Juma alisema kuwa, viongozi hao waliomba kibali cha kufanya mikutano kwenye Uwanja wa Mzalendo ili kuwaombea dua waliofariki kwa ajali ya Meli ya Mv Skagit Jumatano wiki iliyopita, lakini polisi ilikataa kutokana na amri ya Serikali kuzuia mihadhara.

  Alisema kutokana na kundi hilo la Uamsho kufahamika kwa ubishi, jeshi hilo lilipeleka askari wake kwenye Uwanja wa Mzalendo ili kuzuia mkusanyiko wa wafuasi hao wa Uamsho.

  “Polisi waliwahi kuwazuia wafuasi hao wasikusanyike kwenye viwanja hivyo, lakini viongozi wa Uamsho waliwatangazia wafuasi wao wakiwataka wakusanyike kwenye Viwanja vya Msikiti wa Mbuyuni karibu na eneo la Malindi,” alisema Kamanda Aziz.

  Alifafanua kwamba, muda wa kuomba dua ulipofika viongozi hao waliingia msikitini lakini watu wengi zaidi walikuwa nje ya msikiti huo.

  Alisema kuwa kilichoendelea kwenye msikiti huo ni viongozi hao kukashifu viongozi wa Serikali na kuwataka wafuasi wao kutounga mkono Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Alibainisha kuwa wakati hayo yakiendelea, wafuasi wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu, kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi.

  Kamanda huyo alisema kuwa kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha.

  Kiongozi Jumiki ajibu

  Akijibu tuhuma hizo, Naibu Kiongozi wa Uamsho, Hamdan alisema kuwa vurugu hizo zimesababishwa na polisi wenyewe kwani wao walikuwa msikitini wakiwaombea dua waliofikwa na maafa ya ajali ya Mv Skagit.


  “Tunasikitika sana viongozi wa dini kuhusishwa na vurugu zilizotokea jana (juzi), kwa kweli sisi hatuhusiki na vurugu hizo na tumeshangazwa na Jeshi la Polisi kuvamia msikitini na kuanza kuwatawanya waumini waliokuwa wakifanya ibada,” alisema.

  Alisema baada ya sala hiyo walitoa mawaidha ya kuwataka waumini wao wasiilaumu Serikali katika tukio la ajali hiyo ya meli bali wachukulie kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mungu.

  Hamdani alisema kuwa hata kama vijana hao walibeba bendera za Uamsho wao, lakini hawana uhusiano wowote na jumuiya yao.

  “Bendera ni kitambaa ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho, isichukuliwe kila mwenye Bendera ya Uamsho ni mwanachama wa jumuiya hiyo,” alisema.

  Alishangazwa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kwa kurusha mabomu hadi mitaani, hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanaomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao waliopotea katika ajali ya meli.40 mbaroni vurugu Z
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mchelea mwana kulia...
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie manjagu ya nyinyiemu, mlishawakamata wale waliochoma makanisa? Mnakaa mnakamata watu ovyo bila mpangilio bila kutumia akili zenu ila tu kwa amri ya mabwana zenu.

  Mmeshindwa hadi sasa kuwakamata waliochoma makanisa? Inathibitisha uchomaji huo ni nyinyi tu, mlitumika. kama vile kwa Ulimboka -- hatimaye mkamkamata chizi!!!!
   
 9. m

  mkataba Senior Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAO Polisi ni wahuni tu, mimi nawashangaa sana wanaposema wanawatafuta viongozi wa Uamsho wakati wanatembea, wapo majumbani kwao wala hawana wasiwasi.

  Sasa hapo Muamsho wamevunja sheria wapi na walikuwa Msikitini kwao ? na kwa kawaida misikiti mingi kukiwa na swala au dua basi waumini wanafurika mpaka nje ya Misikiti takriban sehemu nyingi.

  Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanza, Muamsho endeleeni na harakati zenu mpaka kieleweke waacheni Watanganyika na upuuzi wao na CCM na ufisadi wao.
   
 10. m

  mkataba Senior Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wewe erevuka tafuta Tanganyika yetu wacha tongo na utomvu Wako Wa macho,

  MUAMSHO ENDELEA NA HARAKATI KAMA KAWA WALA MSITISHWE NA KELELE ZA HUKU TANGANYIKA, HUKU NI MAFISADI WATUPU NA UKAFIRI MWINGI.
   
 11. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakuuliza MMKJ: Hivi kwa nini bado huamini kwamba uchomaji wa makanisa ulikuwa ni mpango wa TISS? Saa nyingine huwa unanishangaza sana!
   
 13. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  bucho

  Ndio nini hiyo, alikuwa anapata daku?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakweli wakati mwingine TISS mnawaonea bure,waarabu wale wafuga ndevu na suruali fupi waliokuwa wanachoma makanisa na wao wameajiriwa TISS! wale ni alshababu au alkaida sema tu baadhi ya viongozi ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa wanawaunga mkono.
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  UAMUSHO ni sawa na AL QAEDA. Naamini Nchimbi atawateketeza hao.
   
 16. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Na hao wamechochewa na chadema inchi isitawalike maana kila mnapokwama sehem utasikia chedema wanamkono wao,wakati mkifanya siasa za udini na ubaguzi mlkuwa hamfaham madhara yake baadae sasa ndiyo haya
   
 17. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,285
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hawa uamsho mkapa ndio alikuwa saizi yao, na aliwamudu barabara!
  hawa dhaifu watachezewa mpaka watakoma.
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Polisi wanacheza nao hawa wawape kibano kitakatifu ili wasirudie badala yake waelekeze nguvu kwenye kazi za ujenzi wa taifa!
   
Loading...