Wafu Miongoni Mwa Waliorodheshwa kustaafu Kariakoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafu Miongoni Mwa Waliorodheshwa kustaafu Kariakoo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Apr 17, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAFANYAKAZI waliokufa inadaiwa kuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa Shirika la Masoko Kariakoo walioorodheshwa kustaafu wakati wowote kuanzia sasa.

  Habari kutoka katika shirika zinadai kuwa, jumla ya wafanyakazi 66 kutoka vitengo mbalimbali vya shirika hilo watastaafishwa.

  Baadhi ya vitengo vitakavyoathirika ni ulinzi pamoja na ukusanyaji wa ushuru.

  Habari zinadai kuwa, jumla ya wafanyakazi 66 tayari wameorodheshwa kustaafu ambapo miongoni mwa majina ya wafanyakazi hao wapo waliokufa na wengine walistaafu kipindi cha nyuma.

  Walipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo, hakuna kiongozi yeyote wa Shirika hilo aliyekuwa tayari kuzungumzia.

  Kwa siku mbili mfululizo mwandishi wa Nifahamishe alifika katika shirika hilo kutaka kujua ukweli wa madai hayo, viongozi wa shirika hilo akiwemo Meneja wake Mkuu Kuboja NgÂ’ungu hawakuwa tayari kuzungumzia chochote.

  Kulingana na chanzo cha Nifahamishe, suala hilo hivi sasa limeibua mvutano baina ya Chama cha Wafanyakazi sokoni hapo (TUICO) na uongozi.

  Hali hiyo inadaiwa kutokea kutokana na kutokuwepo kwa fedha za kuwalipa wafanyakazi watakaopunguzwa kazi katika shirika hilo.

  Kwa upande wake TUICO inataka suala la kupunguzwa wafanyakazi liende sanjari na stahili zao.

  Habari zaidi zinadai kuwa, hii ni awamu ya pili kwa shirika la Masoko Kariakoo kutaka kupunguza wafanyakazi baada ya zoezi hilo kugonga mwamba hapo awali kutokana na Bodi ya Wakurugenzi kukataa kutokana na kutokuwepo kwa fedha za kuwalipa wafanyakazi watakaopunguzwa.

  Kulingana na chanzo cha habari cha hii, hivi sasa uongozi wa shirika hilo unakusudia kukopa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kulipa stahili za wafanyakazi watakaopunguzwa.

  Source: Nifahamishe.com
   
Loading...