Wafikishwa mahakamani kwa wizi wa zaidi ya Tsh. milioni 500

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imewafikisha mahakamani watuhumiwa nane kwa makosa 480 ya udanganyifu na kujipatia zaidi shilingi milioni 500 kutoka Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) kilichopo mjini Iringa

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Iringa,- Mweli Kilimali amesema watuhumiwa hao wametenda makosa hayo kati ya mwaka 2014 na 2019, wakifanya kazi ya kufundisha RUCU huku wakijua ni waajiriwa wa serikali, hivyo kupata mishahara miwili kinyume na sheria za utumishi

Chanzo: TBC
 
Madaktari wa hospital za umma wanapiga part time jobs kwenye hospital binafsi tena nyingine wanazimiliki wao,
Je nao huwa wanachakuliwa hatua?

Chonde-chonde mimi ni mtumishi wa umma ila usiku ni meneja wa night club.
Kama wanafanya muda baada ya kazi yao sio tatizo ila tatizo ni kutumia muda wa mwajiri ambaye ni serikali kufanya kazi zako binafsi.
 
Hili suala la Part Time mbona lipo kila mahali. Inamaanisha hawataki watu wajiongeze kwenye kutafuta kipato?
 
Tatizo ni mishahara miwili si muda.
Wafanyakazi wa serikali wengi wana kazi mbili, mfano katibu wa wizara ya habari pia ni msemaje wa serikali. Nchi za mbali watu wanafanya kazi sehem tofauti hadi usiku huku kwetu imekuwa shida hapo hapo tunasema hapa kazi tu. PCCB inabidi wahusike na rushwa na siyo mambo ambao mtu anajitahidi kufanya kazi ili aweze kukidhi mahitaji yake.
 
Hiki kitengo kimekuwa cha ovyo bora hata Polisi. Kwa hiyo hao walimu wanaotumia taaluma yao kujiongezea kipato ndo mafisadi?
 
Mwongozo wa Waziri Shelukindo wa mwaka 1992 uliruhusu watumishi wa uma kufanya pia private jobz in their free times unless mwajiri amekalamika. TAKUKURU hapo wamekosa weledi.
 
Kama wmekiuka maadili Wa kuwashitaki ni waajiri wao na sio takukuru,swali muajiri amelalamika kuwa mtumishi wake hajafika kibaruwani? Kwa miaka mi5 hiyo ameshitakiwa malangapi kwa kosa la kutohudhuria kazi zake kwa wakati? Kama hakuna basi Kuna kutafuta Kiki,kuonea wanyonge ama kutengeneza mazingira ya Kula rushwa kutoka kwa hao waalimu
 
Kangi yukowapi Kama mnatenda haki? Achaneni na wapiga kura wetu wampitishe chuma October banaaaaaaa😁😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom