Wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za Ubadhirifu wa fedha za Sakosi ya walimu Singida

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,300
5,434
Mahakama ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, imefunguliwa kesi Ecc.52/2022 .

Washtakiwa ni Cladius Linusl na Leah Roman Mnyipanduka
ambao kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya ofisi, ubadhirifu na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Tsh. 10,000,000/= mali ya Manyoni Teachers Saccoss.

Claudius Linus Kaje alikuwa Meneja wa Manyoni Teachers Saccos na Bi. Leah Roman Mnyipanduka alikuwa mmoja wa watia saini wa Manyoni Teachers Saccos.

Baada ya kuwasomea Hati ya Mashtaka wamekana makosa yao.

Pia wamepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
 
Back
Top Bottom