Wafasiri na wakalimani tanzania

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Ndugu wana JF,
Ninafanya utafiti kuhusu wafasiri na wakalimani Tanzania kwa lengo la kufahamu ukubwa wa soko la ajira au huduma hizi hapa nchini. Kusudio kuu la utafiti huu ni kuandaa mtaala wa fani ya tafsiri kitaalamu kwa kiwango cha digrii.
Kwa hiyo ninaomba kama mtu ni mfasiri na/au mkalimani, au kama unamfahamu yeyote yule tuweze kewasiliana kwa kubadilishana mawazo.
Mchango wowote utathaminiwa sana.
Asanteni
 
Mama.100 ;

Heshma sana!!

Samahani..kabla ya kusonga mbele.. Wakalimali ninawaelewa ...Wafasiri ni nani...

Mfano nikitaka kujua maana ya neno fisadi...Ninamtafuta nani?
 
Unaweza kuwasiliana na wataalmu ambao mnaweza kusaidiana kitaalam zaidi nakushauri waone Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam, Tanzania: TUKI au BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania), nadhani ofisi zao zipo pale mlimani chuo kikuu. (Sina uhakika)
 
Mama.100 ;
Heshma sana!!

Samahani..kabla ya kusonga mbele.. Wakalimali ninawaelewa ...Wafasiri ni nani...
Mfano nikitaka kujua maana ya neno fisadi...Ninamtafuta nani?
Mfasiri na mkalimani hawatofautiani sana, ila mfasiri yeye anatumia maandishi yaani kuandika kile anacho kitafsiri, kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine, kama vile kutafasiri kitabu au makala.
 
Mfasiri ni yule anayefasiri maandishi kama vile hati, vitabu na aina mbali za nyaraka wakati mkalimani anafasiri kauli kama vile hotuba, mikutano, majadiliano n.k. Kwa hiyo ikiwa neno fisadi limeandikwa kwenye karatasi, mtafute mfasiri, ikiwa limesemwa kwa lugha moja mkalimani hulisema kwa lugha nyengine.
 
Asante sana kwa maelekezo yako, nitafanya hivyo. Hata hivyo,ikiwa unawaelewa wengine wowote, naomba kuwasiliana nao.
 
Kwa bahati ghafi mimi nipo nje ya Afrika, ningekuwa uko ulipo ningekusaidia kwa karibu sana.
 
Back
Top Bottom